Blog Page

Wagombea msikiti aliojenga Nyerere

Waumini wa Kiislamu katika Kijiji cha Butiama na uongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mara wamo kwenye mgogoro kuhusu umiliki na uendeshaji wa msikiti uliojengwa kwa msaada wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kijijini hapo. Msikiti huo ulianza kujengwa wakati Mwalimu akingali hai, na ulifunguliwa rasmi na aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Omar Ali Juma, ...

Read More »

Mapya sakata la korosho

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mikoa ya Lindi na Mtwara, Zuberi Ally Maulid, amefichua kinachoendelea kuhusu wakulima kurudishiwa korosho zinazodaiwa ni mbovu. Kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye amewahi kuwa mbunge ndani ya Bunge la Tanzania, hali si shwari katika mchakato wa ununuzi na malipo ya korosho. Katika mazungumzo yake ...

Read More »

Gari la Polisi ladaiwa kuua bodaboda Segerea

Gari la Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadaiwa kuua dereva wa pikipiki, Cosmas Swai (42), kwa kumkanyaga kichwani akiwa amembeba mkewe, Anna Swai (39) pamoja na mwanawe, David Swai (11). Ajali hiyo imetokea Machi 12, mwaka huu, eneo la Segerea Mbuyuni, baada ya mashuhuda wa ajali hiyo kudai kuwa gari hilo ...

Read More »

Namna ya kukomesha ubambikaji kesi Polisi

Wiki iliyopita katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa miaka mingi, Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa miongoni mwa taasisi za kitaifa zilizothibitisha kuwa chombo hicho kimewahi kuhusika kubambikia baadhi ya wananchi kesi. Baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kudai kuwa Jeshi la Polisi kupitia kwa baadhi ya askari wake walimbambikia kesi mmoja wa wafanyabiashara mkoani Tabora, Jeshi la Polisi kupitia kwa ...

Read More »

NINA NDOTO (11)

Ukiamua kufanya, fanya kweli   Fanya mambo kwa ubora. Chochote unachokifanya hakikisha unakifanya vizuri  na kwa ubora wa hali ya juu; kiasi kwamba watu wakikiona wawe tayari kuwaambia wengine kuhusu wewe. Hata mimi nikiona kazi yako unaifanya kwa ubora nitakuwa tayari kuwaambia wengine na kutoa sifa bora juu yako wewe, hii imekuwa tabia yangu. Watu wanapenda ubora, watu wanapenda vitu ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (6)

Wiki iliyopita nilihitimisha makala hii kwa aya hii: “Kumbuka kuna biashara zina leseni zaidi ya moja, hivyo kama nilivyosema kabla ya kuanzisha biashara, unapaswa ufanye utafiti kufahamu aina ya biashara unayotaka kuifanya, eneo unalopaswa kufanyia, aina ya wateja, aina za kodi, leseni na mengine mengi. Ikumbukwe hapa nazungumzia mtu aliyechagua kuanzisha biashara kama mtu binafsi, hapa sijazungumzia jina la biashara ...

Read More »

Je, furaha ipo katika vitu?

Furaha ni mtihani. Si kila tabasamu ni ishara ya furaha na si kila chozi ni ishara ya huzuni. Si kila kicheko ni ishara ya furaha na si kila kilio ni ishara ya masikitiko. Kwa msingi huo, furaha ni mtihani. Si kila maneno, “karibu sana” ni ishara ya furaha na si kila maneno “kwaheri nitakukosa” ni ishara ya huzuni. Kwa msingi ...

Read More »

Ndugu Rais kwanini Nyerere mpaka leo?

Ndugu Rais, kwa pamoja tujifunge unyenyekevu mbele za Mungu kwa sababu Mungu wetu huwapiga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema yake. Tunyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari ili atukweze kwa wakati wake kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yetu. Awamu ya tano imekuja na historia yake tofauti na awamu zote zilizoitangulia. Haikubweteka hata kidogo. Imejaribu kadri iwezavyo ...

Read More »

Uhuru wa bila mipaka unahitaji ukarabati

Kama kuna mambo ambayo tuna hakika yatajirudia, tena na tena, ni matukio ya ugaidi katika sehemu mbalimbali duniani. Katika tukio la juma lililopita raia wa Australia, Brenton Harrison Tarrant, amefunguliwa mashtaka ya mauaji nchini New Zealand akituhumiwa kupanga na kutekeleza tukio la kigaidi dhidi ya misikiti miwili na kusababisha vifo vya watu 49. Idadi kama hiyo ya watu wamejeruhiwa. Tumezoea ...

Read More »

Utaratibu wa kisheria katika kununua ardhi

Tunazo aina kuu mbili za ardhi. Tunayo ardhi iliyosajiliwa na ardhi ambayo haikusajiliwa. Ardhi ambayo imesajiliwa ni ardhi iliyopimwa au maarufu ardhi yenye hatimiliki, wakati ardhi ambayo haikusajiliwa ni kinyume cha hiyo. Na ardhi tunamaanisha viwanja, nyumba au mashamba. Pamoja na hayo, makala ya leo itamulika ardhi iliyosajiliwa/iliyopimwa/yenye hatimiliki, wakati makala katika toleo lijalo itamulika utaratibu wa kununua ardhi ambayo ...

Read More »

Kenya wametutega nasi tumeingia

Sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ambayo ni sheria ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tumeiridhia na imeshaanza kutumika. Maelezo ya wakubwa ni kwamba sheria hii inalenga kupunguza uzito wa shehena inayopakiwa kwenye malori, lengo kuu likiwa ni kulinda barabara zetu. Hii ndiyo sababu kuu kati ya sababu zote zilizowashawishi viongozi wetu kutunga sheria hii. Sheria ilipaswa ...

Read More »

Narudi nyumbani

Rudi na nyumba ni maneno ya Kiswahili na kila moja lina maana na umuhimu wake katika matumizi. Unapoyatumia maneno haya katika matukio yako ni dhahiri shahiri una nia ya kufanya jambo ambalo kwako na kwa wenzako lina faida. Ni maneno yenye maana kubwa ya ustaarabu na uungwana mbele ya jamii. Neno rudi lina maana nne. Lakini leo nitazungumzia maana mbili ...

Read More »

Yah: Urasimu ni jambo jema, lakini si urasimu wetu

Kama ilivyo ada, sina budi kuanza na salamu za kiungwana kama Mtanzania mwenye kuheshimu mila na desturi zetu. Sisi Watanzania tulipandiwa mbegu hiyo na hatuna budi kuiheshimu na kuiendeleza, ndiyo maana ni rahisi zaidi kumjua Mtanzania halisi kwa kupitia salamu na jinsi anavyowaheshimu watu wengine. Katika hili kunaweza kukawa na baadhi ya wenzetu ambao wanaharibu taswira ya Utanzania, kwa kudhani ...

Read More »

‘Bravo’ Simba SC

Haikuwa rahisi kwa timu ya Simba SC kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Ni safari ya milima na mabonde lakini hatimaye Simba wamevuka na kuingia katika hatua ya robo fainali, na haikuwa safari ya usiku mmoja. Kauli mbiu mahususi ya ‘Do or Die’ (kufa au kupona) kama viongozi wa Simba walivyoinadi kwa mashabiki wao ilitimia, ...

Read More »

Magufuli kutua China

Rais Dk. John Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuvuka mipaka ya Bara la Afrika, kwa kuitembelea China kwa ziara ya kiserikali, Gazeti la JAMHURI limebaini. China imekuwa mdau muhimu wa maendeleo wa Tanzania, kupitia mkakati mahususi wa Tanzania ya viwanda, wawekezaji kadhaa kutoka nchi hiyo ya barani Asia wameitikia wito kwa kuanzisha viwanda kadhaa hapa nchini. Vyanzo vyetu vinasema ...

Read More »

Katavi, Tabora vipi?

Mpita Njia ameshitushwa na taarifa za hivi karibuni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshika nafasi ya tatu barani Afrika katika ndoa na mimba za utotoni. Hizi si tu ni taarifa za kushitua, bali ni taarifa za aibu katika wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano inajielekeza katika kuhimiza elimu kwa wote, kiasi cha kuondoa malipo ya ada. Hili ...

Read More »

Ajali ya ndege yaua abiria wote

Watu wote 157 waliokuwa safarini katika ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia,  Boeing 737, wamepoteza maisha baada ya ndege hiyo kuanguka. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kuelekea mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumapili iliyopita. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ethiopia, abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo ni 149 na watu wengine wanane ...

Read More »

Mjamzito afanya Mtihani wa Taifa, afaulu

Shule ya Filbert Bayi iliyopo Kibaha, mkoani Pwani, mwaka jana iliruhusu mwanafunzi mjamzito kufanya mtihani wa taifa wa kuhitimu Kidato cha Nne. Mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) alifanya mtihani huo kwa namba S 1437/0002 katika matokeo ya mtihani yaliyotangazwa Januari mwaka huu, alifaulu kwa kupata daraja la pili lenye alama 20 (Division II, 20). JAMHURI limeelezwa wakati anakutwa na mimba hiyo ...

Read More »

Wawekezaji wamchongea DC kwa Rais

Uamuzi wa wawekezaji wilayani Hai, Kilimanjaro kumshtaki mkuu wa wilaya (DC) hiyo kwa Rais John Magufuli umepongezwa na baadhi ya wafanyabiashara na kuonekana kuwa ni mwanzo wa kumaliza vitendo vya kunyanyaswa. DC wa Hai, Lengai ole Sabaya, anatuhumiwa na wawekezaji hao kuwa anawanyanyasa kwa kuwakamata, kuwaweka ndani na kuwaomba rushwa. Kilio chao kilichowekwa kwenye maandishi, kimewasilishwa kwa Rais Magufuli, ambaye ...

Read More »

Maji ni kichocheo cha maendeleo

Wiki ya Maji ni fursa maalumu ya sekta ya maji nchini kujitathmini kwa kujilinganisha na nchi nyingine duniani katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji. Maji ni kichocheo muhimu cha maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini, ikiwemo kilimo, biashara, utalii na viwanda. Katika kutambua umuhimu na thamani ya maji katika maisha ya binadamu na uchumi wa dunia ...

Read More »

Tanzania tunao wajibu wa kuziokoa Rwanda, Uganda

Fukuto la kutokea mfarakano na hata umwagaji damu linaendelea kati ya Uganda na Rwanda. Lakini pia kuna msuguano mkubwa wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Burundi. Mataifa haya matatu ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hii ina maana kwamba jambo lolote baya katika mataifa hayo lina athari kwa nchi wanachama, hasa Tanzania. Tanzania ni mwathirika mkuu kwa sababu tunapakana ...

Read More »

NINA NDOTO (10)

Maono humfanya dhaifu awe imara   Maono hubebwa katika vitu vitatu muhimu. Mosi, uwezo wa kuona mbele. Pili, uwezo wa  kuona kwa undani. Tatu, uwezo wa kuona nyuma. Uwezo wa kuona mbele ni sawa na kuona kwa kutumia darubini. Darubini ni chombo  kinachofanya vitu vilivyo mbali vionekane karibu. Kila mtu na uwezo wa kuona mbali, lakini ni wachache tu wameamua ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons