Sitanii

Lipumba anachoma nyumba aliyomo!

Naandika makala hii nikiwa hapa jijini Tanga. Nashiriki mkatano wa mwaka wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na wanahabari. Nimepata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Msitu wa Amani. Msitu huu ulioko Muheza ni wa aina yake. Msitu uko kwenye bonde na kingo za milima. Msitu umehifadhiwa na unayo miti iliyokomaa usipime. Miti hii inakua, inazeena na kuanguka au kuangushwa ...

Read More »

Rubani wa Precision Air atuzwe (marudio)

Wiki iliyopita makala hii ilichapishwa. Hata hivyo, kimakosa kuna aya mbili zilikatika na kuifanya makala hii kupoteza maana ya kwa nini imeandikwa. Kutokana na wasomaji wengi kunipigia simu kuuliza ilihusu nini, naomba kuirudia makala hii. Pia naomba radhi kwa usumbufu uliotokana na kukatika kwa aya hizo. Endelea na nakala iliyosahihishwa sasa… Wiki iliyopita (wiki mbili sasa) rubani wa ndege ya ...

Read More »

Rubani wa Precision Air atuzwe

Wiki iliyopita rubani wa ndege ya Shirika la Precision inayoruka kutoka Nairobi kuja Dar es Salaam, Rizwan Remtura amelifanyia taifa letu kazi ya kupigiwa mfano. Rubani huyo amefanya tukio ambalo hakuna aliyepata kuliwaza na ni tukio ambalo likitazamwa kwa mapana yake linaweza kuwa chimbuko la faida kubwa kwa taifa letu. Sitanii, mwaka 2004 niliposafiri kwenda nchini Misri nilipata fursa ya ...

Read More »

Kila upande hautaki kusikia haya!

Leo naandika Sitanii ngumu. Ni ngumu kwa misingi kwamba kila atakayesoma makala hii ya leo, kuna mambo ataburudika hadi atamani kunipigia simu ya pongezi, lakini pia, kuna mambo atasoma kama si mvumilivu, atatamani kunipigia simu kunitukana. Nitatahakiki suala hili la madini kwa mawanda mapana. Hakika sitatasiliti, bali nitatashtiti. Sitanii, msamiati uliotangulia katika aya ya kwanza nausitisha kidogo, kuepusha usisome makala ...

Read More »

Magufuli madini historia haitakusahau

Wiki iliyopita Serikali imepeleka bungeni miswada mitatu kwa hati ya dharura. Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms)] Bill, 2017]. Muswada wa Marekebisho ya Sheria, 2017 na Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya ...

Read More »

Kodi za majengo, mimba za utotoni

Kwa muda wa wiki mbili sasa sijaandika katika safu hii. Nimepata simu nyingi, na ujumbe mfupi, wengi wa wasomaji wangu wakidhani kuna maswahibu yamenisibu. Nawahakikishia niko salama bin salimin na buheri wa afya. Sikuweza kuandika katika kipindi cha wiki mbili zilizopita kwa sababu kuu mbili. Ya kwanza tulikuwa katika mafunzo endelevu mjini Dodoma yaliyolenga kutuandaa kubadili mwelekeo wa kampuni yetu ...

Read More »

Rais Magufuli ulimchelewesha Muhongo

Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli shikamoo. Leo nakuandikia waraka huu mfupi kupitia safu yangu ya Sitanii. Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu kukupongeza na kukushukuru kwa hatua ya kudhibiti wizi wa madini yetu na pia kumwondoa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo. Unaweza au baadhi ya wasomaji wanaweza kushangaa kwa nini nifurahie kuondolewa kwa Muhongo. Sitanii, kwanza ...

Read More »

TEF inatetea uhuru wa habari

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na baadaye, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yusuf Makamba, alipata kusema hivi: “Mti wenye matunda ndiyo unaorushiwa mawe.” Wiki iliyopita nimethibitisha kauli ya Luteni Makamba. Nimeithibitisha baada ya kutia saini tamko la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa wadhifa wangu kama Makamu Mwenyekiti wa TEF, lililoikumbusha jamii kuwa Televisheni ...

Read More »

Rais Magufuli muulize Mkapa kodi

Leo naandika makala hii baada ya Taifa kuwa limepata mapigo makubwa mawili. Pigo la kwanza ni vifo vya wanafunzi 32 wa Shule ya Msingi St. Lucky Vincent, walimu wawili na dereva mmoja. Sina hakika siku ya mazishi ya kitaifa ya watoto hao mwenzangu wewe unayesoma makala hii ilikuwaje, ila mimi nilijikutana machozi yananibubujika. Sitanii, hakika huu umekuwa msiba wa kitaifa. ...

Read More »

Waandishi tujimulike kielimu

Wiki iliyopita yametokea matukio mawili makubwa. Wanahabari tumeadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari. Siku hii inaadhimishwa kimataifa na kitaifa imeadhimishwa jijini Mwanza. Kaulimbiu ya siku ya mwaka huu imekuwa ni Fikra Yakinifu, Jukumu la Vyombo vya Habari katika Kudumisha Amani, Usawa na Jamii Jumuishi. Katika maadhimisho haya zilitawala hoja kuu tatu. Usalama wa wanahabari, weledi kwa waandishi dhidi ...

Read More »

ACP Awadhi anaipa heshima polisi

Wiki iliyopita kulitokea sintofahamu kati ya dereva wa gari la Gazeti la JAMHURI na mmoja wa matrafiki. Baada ya tukio hilo nilibaini chembe chembe za uonevu na nikaamua kuchukua hatua za kisheria kupitia mkondo wa utawala dhidi ya askari aliyekamata gari hilo. Jeshi la polisi lilisikiliza maelezo yetu na muda mfupi baada ya kutoka polisi niliandika kwenye mitandoa ya kijamii ...

Read More »

Rais Magufuli umeokoa elimu

Jumamosi Aprili 15, 2017 imekuwa ya burudani kwangu. Nimeburudishwa na hotuba aliyoitoa Rais John Magufuli wakati akizindua mabweni ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  Kwanza ameniburudisha kwa kujenga mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 kwa gharama ya Sh bilioni 10. Hii ina maana majengo 20, kila jengo limejengwa kwa gharama ya Sh milioni 500. Hakika, gharama ...

Read More »

Wabunge wetu, kodi ya nyumba

Leo najua Taifa linakabiliwa na matatizo mengi. Kuna wenzetu waliopotea kwa kusema ukweli. Sina uhakika kama kwa mwenendo huu nchi yetu itabaki salama. Wanaopotelewa na ndugu zao wakiungana, tutakuwa na jeshi kubwa la kupinga upoteaji. Sina uhakika pia kama kwa kuandika makala hii nami sitapotea siku moja. Sitanii, kwa muda nimekuwa nikisikia habari za watu kupotea katika nchi jirani za ...

Read More »

Dk. Mwakyembe karibu kwa wanahabari

Wiki iliyopita, Rais John Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri. Mabadiliko aliyofanya ni kumwondoa kwenye Baraza la Mawaziri, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kumteua Dk. Harrison Mwakyembe kuziba pengo hilo. Dk. Mwakyembe amehamishwa kutoka Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba. Nafasi yake imechukuliwa na Prof. Palamagamba Kabudi. Katiba ya Jamhuri ya ...

Read More »

La Lissu Wanasheria wamezungumza!

Wiki iliyopita Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameshinda urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika. Ushindi wa Lissu umetokea baada ya matukio kadhaa, ikiwamo kukamatwa na kufikishwa mahakamani saa 24 kabla ya uchaguzi. Si hiyo tu, Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli japo alionya bila kutaja majina alisema TLS isiingizwe kwenye siasa. Sitanii, Waziri wa ...

Read More »

La Lissu Wanasheria wamezungumza!

Wiki iliyopita Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameshinda urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika. Ushindi wa Lissu umetokea baada ya matukio kadhaa, ikiwamo kukamatwa na kufikishwa mahakamani saa 24 kabla ya uchaguzi. Si hiyo tu, Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli japo alionya bila kutaja majina alisema TLS isiingizwe kwenye siasa. Sitanii, Waziri wa ...

Read More »

Ni hatari kuua biashara

Leo nimeona niandike mada inayogusa maisha ya kila Mtanzania –  biashara. Naandika mada hii kutokana na mwenendo usioridhisha unaoonesha kuwa biashara nyingi hapa nchini zinakufa.  Kwa muda mrefu tumekuwa tukiambiwa kuwa Tanzania ni taifa la wakulima na wafanyakazi. Ni kwa bahati mbaya, hao wakulima na wafanyakazi wanastahili heshima, ila uchumi una misingi yake. Kwa siku za karibuni wafanyabiashara wengi hapa ...

Read More »

Uzuiaji viroba sawa, mifuko ya plastiki nayo iunganishwe

Serikali imepiga marufuku utengenezaji na usambazaji pombe maarufu kwa jina la ‘viroba’ kuanzia Machi mosi, mwaka huu. Uamuzi huu umetokana na ukweli kuwa matumizi ya ‘viroba’ yalishavuka mipaka; na hivyo kuwa chanzo cha maovu na misiba nchini kote. Hatua hii, licha ya ukweli kuwa imechelewa, bado inastahili kupongezwa kwani inafungua ukurasa mpya kwa afya za Watanzania, hasa vijana. Matumizi ya ...

Read More »

Mwakyembe hawezi kuifuta TLS

Wiki hii nchi imeingizwa katika mjadala mrefu usio na tija. Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe nadhani amehemka tu, akasema ikibidi atakifuta Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS). Kauli ya Dk. Mwakyembe imetoka muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kuwataka wanasheria wanachama wa TLS kujiepusha na siasa. Rais Magufuli Februari 2, alionya hatari ya TLS ...

Read More »

Katika hili Makonda amepatia

Leo nipo Makao Makuu ya nchi, Dodoma. Nimekuja kuendeleza uenezaji wa ujumbe wa haki ya kupata habari. Tumepata fursa ya kuendesha semina kwa wabunge na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa wabunge kufanya kazi pamoja na vyombo vya habari. Suala la ‘Bunge Live’ limeibuka kwa nguvu katika semina hii. Imeandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ...

Read More »

Hakika Lukuvi anawezesha Watanzania

Mwaka 2004 aliyekuwa Rais wa Tanzania , Benjamin Mkapa alimleta nchini mtaalam wa uchumi, Prof. Hernando de Soto Polar (75 – sasa) kuzungumza jinsi ya kuwaondoa Watanzania katika lindi la umaskini. Nilipata fursa ya kuwapo kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam. Prof. de Soto alizungumza kwa angalau saa 3 hivi, ukichanganya na maswali, ila sijawahi ...

Read More »

Trump ameapishwa, Jammeh Ehe!

Nchini Marekani, mwezi Novemba, 2016 walifanya uchaguzi wa Rais. Aliyekuwa mgombewa wa Chama cha Republican, Donald Trump alishinda katika mazingira yaliyoshangaza wengi. Alimshinda aliyekuwa mgombea wa Democrat, Hillary Clinton. Ingawa Clinton alishindwa katika kura za majimbo, aliibuka mshindi katika kura za wananchi. Sitanii, hiyo ndiyo Marekani. Si lazima anayechaguliwa na wananchi ndiye awe Rais. Baada ya hapo tulishuhudia kelele za ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons