Sitanii

Rais Magufuli naomba uniazime sikio

Wiki iliyopita nimesikia mambo mengi, ila mawili yaliniingia akilini. La kwanza ni hotuba ya Rais John Pombe Magufuli akiadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambayo kwa mara ya kwanza yameadhimishwa upande wa Tanganyika.  Hii ni historia ya pekee, ambayo haitakaa ifutike. Watanganyika wamethibitisha kwa dhati kuwa wanathamini kilichotokea Zanzibar Januari 12, 1964. Sitanii, katika maadhimisho haya yaliyofanyika katika ...

Read More »

Sherehe zimekwisha, tuchape kazi

Mpendwa msomaji, Heri ya Mwaka Mpya 2017. Leo nimeona niandike mada inayohusiana na maisha. Nafahamu kuwa mwezi uliopita ulikuwa wa mapigo. Kwa wenzangu na mimi wanaofanya biashara za kubangaiza, umekuwa mwezi mgumu kuliko maelezo.  Mwezi huu ndiyo usiseme. Kwa watu wengi kodi za nyumba zinaisha. Ada za watoto ziko mlangoni, na hakuna pa kupata mkopo. Benki nyigi zimesitisha ukopeshaji. Baa ...

Read More »

Vyombo vya habari binafsi

Kwa wiki mbili sasa sijaonekana katika safu hii. Niwie radhi msomaji wangu sikuchagua kutokuwapo, bali kutokana na kazi nzito ya kuchunguza magendo mpakani huko Tunduma, ilinipasa nisiwe mshika mawili. Leo nimerejea. Salamu za heri huwa hazichachi. Msomaji wangu nakutakia heri ya Krismasi na Mwaka Mpya, 2017, nikitaraji mwaka huu pamoja na magumu yake utaumaliza salama, na mwakani utajipanga sawa sawa. ...

Read More »

Tunduma Uchumi ni kilio

Kwa muda wa wiki sasa nimekuwa hapa katika Mji wa Tunduma. Mji huu ni mji unaoongoza kwa kuwa na benki nyingi, idadi ya watu si haba na miundombinu yake baada ya kujengwa Barabara ya Tunduma Sumbawanga, si haba. Kwa sasa kuna upanuzi wa barabara unaendelea na maduka yaliyokuwa barabarani yamevunjwa na kusogezwa nyuma, kimsingi unakuwa na sura mpya. Hata hivyo, ...

Read More »

Majaliwa asante la Makonda

Wiki iliyopita kwa mshangao mkubwa nimesoma maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda. Makonda amesema mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa lipo kundi la watu 10 lilitaka kumhonga Sh 5,000,000 kila mmoja kwa maana ya Sh milioni 50 kwa mwezi asiendelee na mpango wa kuzuia uuzaji wa dawa za kulevya aina ya Shisha. Makonda amewatuhumu ...

Read More »

Sheria imepita, upotoshaji umetawala

Wiki iliyopita hatimaye Serikali imehitimisha safari ya miaka 23 ya mchakato wa kutunga Sheria ya Huduma za Habari (MSB). Sheria hii inajihuisha zaidi na utendaji wa vyombo vya habari na wanahabari. Mchakato huu ulianza rasmi mwaka 1993 na umehitimishwa mwaka 2016. Waliouanzisha mchakato huu baadhi wamefariki dunia kabla ya kuona hitimisho lake, akiwamo Dk. William Shija aliyefariki mwaka 2014. Niseme ...

Read More »

Maswali ni mengi Bukoba

Nakaribia wiki mbili sasa nikiwa hapa Bukoba. Naendelea na ukarabati wa nyumba ya mama yangu iliyosambaratishwa na tetemeko. Hata hivyo, pamoja na kuwa katika ujenzi huu, haimaanishi kuwa kazi yangu nimeiweka kando. Naendelea kuzungumza na wananchi, nafuatilia kinachoendelea na jinsi misaada inavyotolewa kwa wahanga wa tetemeko. Angalau sasa watu baadhi wamepewa magodoro, wengine wamepewa mablanketi, sukari kilo 2 kwa familia, ...

Read More »

Rais Magufuli Bukoba wanakutania

Nikiwa jijini Accra, Ghana katika toleo Na. 260 la Gazeti la JAMHURI, niliandika makala yenye kichwa hiki: “Poleni Bukoba, tuchunge wapigaji!” Hili ni toleo lililochapishwa Jumanne ya Septemba 20, 2016. Nilianza kupata wasiwasi kuwa huenda wakajitokeza watu wa kutumia janga la tetemeko la ardhi kujitengenezea utajiri hewa! Kabla wino haujakauka yametokea. Serikali imesisitiza mara kadhaa kuwa inafungua akaunti ya maafa ...

Read More »

Poleni Bukoba, tuchunge wapigaji!

Leo imepita karibu wiki moja tangu lilipotokea tetemeko la ardhi mkoani Kagera, hasa Wilaya ya Bukoba. Tetemeko hili limeacha majonzi makubwa.  Taarifa nilizosoma kwenye mtandao zinaonesha kuwa watu wapatao 17 wamepoteza maisha, zaidi ya 200 wamejeruhiwa na nyumba zaidi ya 5,000 zimeathirika ama kwa kubomoka au kupata nyufa kubwa. Nitangulie kusema bayana hapa kuwa hata mimi nimekuwa mhanga wa tetemeko. ...

Read More »

Afrika inamheshimu Rais Magufuli

Leo naitafuta wiki ya pili tangu nifike hapa Accra, Ghana. Naendelea na mafunzo juu ya mafuta, gesi na madini. Mafunzo haya yanalenga kuwapa utaalam watu mbalimbali; waandishi, makarani wa bunge, maafisa wa serikali, vyama vya kijamii, viongozi wa jadi na wengine wengi. Mafunzo haya yamelenga katika kutufundisha nchi zetu zinavyoweza kufaidika na wawekezaji wakafaidika. Wanatupatia ujuzi jinsi ya kusoma na ...

Read More »

Samahani Mheshimiwa Rais Magufuli

Naandika makala hii dakika chache baada ya kufika jijini Accra, Ghana. Nimetoka Dar es Salaam jana na juzi nilisikia maneno aliyozungumza Mheshimiwa Rais John Pombe Mafuguli, alipopata fursa ya kutembelea Pemba kushukuru wapigakura. Nikiri kwanza kwamba Rais wetu anafanya jambo zuri sana. Kwa wanadamu tulio wengi, ni rahisi mno kuomba. Tukiishapata, huwa hatukumbuki kurejea kushukuru. Natumia fursa hii kumpongeza Mhe. ...

Read More »

Asante Lukuvi, umeokoa wanyonge Bukoba

Mpendwa msomaji, niwie radhi wiki hii nalazimika kuandika SITANII ndefu kidogo, na SITANII ya leo itakuwa na vionjo tofauti na zilizotangulia. Nitangaze maslahi pia, kuwa katika hili ninayo maslahi nitakayoyaeleza punde, lakini nitangulie kusema nampongeza na kumshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. Sitanii, Agosti 16, 2016 nilikuwa Dodoma. Ilikuwa saa 6:00 mchana, nikapokea simu ya ...

Read More »

Rais Magufuli anamjenga Lissu

Wiki iliyopita vyombo vya habari vimetangaza habari nyingi za kukamatwa, kusafirishwa, kushikiliwa polisi, kufunguliwa kesi mahakamani, kesi kuendelea hadi saa 3:00 usiku na kisha Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kujidhamini. Binafsi sina nia ya kurejea matamshi ya Lissu, lakini nitaangalia nguvu kubwa inayotumiwa na dola kumdhibiti Lissu. Kabla sijaendelea kudadavua suala la jinsi gani Rais Magufuli anamjenga Lissu, ...

Read More »

Mauaji, hukumu ya Mwangosi

Naandika makala hii muda mfupi baada ya kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Iringa. Nimekuja hapa Iringa kusikiliza hukumu dhidi ya muuaji wa Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi, aliyeuawa na askari Pacificus Cleophace Simon Septemba 2, 2012 akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa. Niliamua kuja Iringa, baada ya kusikia mizengwe ya polisi katika kesi hii. Sitanii, pengine nisije kusahau ...

Read More »

Rais Magufuli umemsikia Kikwete!

Wiki iliyopita Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemchagua Rais John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wake. Uchaguzi huu umehitimisha minong’ono iliyokuwapo kitambo kuwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete alikuwa na nia ya kung’angania madarakani. Rais Magufuli amepigiwa debe kuomba kura kati yao akiwamo Katibu Mkuu (mstaafu) wa CCM, Luteni Yusufu Makamba. Makamba alitumia maandiko ya vitabu vitakatifu, ikiwamo Biblia ...

Read More »

Kila la kheri Rais Magufuli

  Wiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ukiacha ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, ambao aliupata kwa kuwa Mbunge wa Biharamulo Mashariki kabla ya Jimbo hilo kuitwa Chato. Hajapata kugombea nafasi yoyote ya kisiasa ndani ya chama chake. Rais Magufuli kabla ya kuchaguliwa kuwa ...

Read More »

Tunayeyusha kiwango cha uvumilivu

Hivi karibuni naona mwelekeo usio na afya kwa taifa letu. Nimewaona polisi wakipiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, nimeona vyama vikitoa matamko ya nia ya kukabiliana, nimesikia baadhi ya vijana ndani ya vyama wakihamasishana kwenda Dodoma kuzuia mkutano wa wapinzani wao na nimeshuhudia Serikali ikizuia mikutano ya Bunge live. Sitanii, naomba mniruhusu kusema ninachokiwaza. Napata tabu kidogo. ...

Read More »

Uingereza wamechagua kunywa sumu

Moja ya hotuba za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere zinazowakuna Watanzania ni ile ya Dhambi ya Ubaguzi. Mwalimu Nyerere aliwaonya Watanzania kuepuka dhambi ya ubuguzi. Alituasa Watanzania kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukiishaanza hauachi. Mwalimu aliwaonya Watanzania kujiepusha na dhambi hii. Alitwambia kuwa tutafanya kosa kubwa mno iwapo siku moja tutaamka tukavunja Muungano. Akatumia ...

Read More »

CCM acheni majungu, jengeni nchi

Leo naandika makala hii nikiwa hapa jijini Accra, nchini Ghana. Ghana ni nchi iliyokuwa ya kwanza kupata uhuru barani Afrika.  Nchi hii ilitutangulia miaka minne kupata uhuru kwa maana ya kupata uhuru Machi 6, 1957 ambapo Dk. Kwame Nkrumah alitangazwa kuwa Waziri Mkuu, cheo alichoshika hadi mwaka 1960 Ghana ilipotangazwa kuwa Jamhuri na hivyo Nkrumah akachaguliwa kuwa Rais wa kwanza ...

Read More »

Tusiibeze bajeti, tusiishangilie

Juni 9, mwaka huu, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, aliwasilisha bajeti ya Serikali bungeni kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bajeti hii imeficha siri nzito yenye mwelekeo wa kuliondoa Taifa letu katika aibu ya kuwa ombaomba. Ni kweli, bajeti imerejea maeneo yale yale ya kuongeza kodi kwenye soda, vinywaji baridi, bia na vinywaji vikali. Hata hivyo, kwa maeneo ...

Read More »

Rais Magufuli wekeza upate kodi

Wiki iliyopita niliandika makala juu ya kijana aliyefuga kuku huko Singida. Nimebaini kuwa ufugaji ule umekuwa kivutio kikubwa kwa wengi waliosoma makala yangu. Hata hivyo, ingawa wengi walitaka kuwasiliana naye awafundishe, kijana huyo anasema yeye alifundishwa na mwalimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro, hivyo anawasihi wengi kutafuta wataalam kutoka SUA. Kijana huyu haonekani kuwa tayari kuwasiliana na ...

Read More »

Rais Magufuli epuka ushauri huu!

Wiki iliyopita nilikuwa katika kipindi cha ‘Malumbano ya Hoja’ kinachorushwa ‘live’ na ITV. Mjadala kadiri ulivyoendelea nilipata shida kidogo. Niliwaona baadhi ya wachangiaji wakizungumza lugha ya hatari, ambayo ninaisoma katika baadhi ya magazeti. Wanasema Rais John Magufuli anahujumiwa.  Sitanii, neno hili linaweza kuonekana dogo, lakini tunakoelekea lisipokemewa linaweza kudumaza maendeleo ya nchi. Kwa sasa nchi ina tatizo la sukari. Sukari ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons