Sitanii

CCM iruhusu ushindani wa haki urais

Kwa wiki takribani nne hivi, sijaonekana katika safu hii. Sikuonekana kutokana na matatizo ya msiba, lakini pia nikalazimika kufanya kazi mikoani. Huku niliko nakumbana na tunachopaswa kupambana kukiondosha. Sehemu nyingi za mikoani hakuna huduma ya data (Internet), simu zipo ila ukitaka kuingia kwenye Internet ili utume barua pepe ni sawa na kushuka mchongoma. Yapo baadhi ya maeneo kuna mtandao, lakini ...

Read More »

Bandari Bagamoyo, kifo cha Bandari Dar

Imenichukua miaka miwili kufikiri juu ya hiki kinachoitwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Ujenzi huu ulianza kutajwa mwaka 2010, na ilipofika Machi 2013, Rais wa China, Xi Jinping, akatia saini mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo. Mkataba ukasema bayana kuwa ujenzi huu utatengewa dola bilioni 10. Nilisubiri kusikia Watanzania wanasema nini, ila muda wote naona kimya. Mkoa wa Mtwara kidogo ...

Read More »

Kikwete ana mgombea wake kwenye koti

Kwa muda sasa nimefuatilia kinachoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nimefuatilia kwa karibu kitu kinachoitwa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia chama hicho kikongwe. Bila kuuma maneno, nasema mchakato umejaa mizengwe. Bila kupepesa macho nasema inawezekana Rais Jakaya Kikwete ana mgombea wake kwenye koti.   Nimeyasikia maelezo ya Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya ...

Read More »

Kova futa agizo lako, ajali zinatumaliza

Wiki mbili zilizopita, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, amemaliza mgomo wa madereva.    Kova alimaliza mgogoro huo baada ya madereva kukataa kwenda tena darasani kila baada ya miaka mitatu, na akaagiza tochi zote za mwendo kasi ziondolewe barabarani na kusema ukaguzi utafanyika kwenye vituo vya mizani pekee. Baada ya agizo hili la ...

Read More »

Amani Tanzania inatuponyoka taratibu

              Kwa muda sasa nimefuatilia matukio yanayoendelea nchini. Nimesoma habari mbalimbali zinazoonesha askari polisi wakiuawa kwa risasi na kunyang’anywa bunduki katika maeneo kadhaa hapa nchini. Tumesikia ‘magaidi’ katika mapango ya Amboni Tanga.  Vituo vya polisi vimetekwa. Tumeshuhudia wafanyabiashara wakigoma na kuipa amri Serikali. Nikumbushie kidogo tu kuwa mwezi uliopita, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Ndogondogo, Joseph ...

Read More »

Tukicheza hakuna uchaguzi Oktoba

“Mheshimiwa Rais, Kenya imewachukua miaka saba kuandika Katiba yao, baada ya mvutano wa miaka 20. Je, sisi Tanzania unadhani tunaweza kuandika Katiba yetu ndani ya miaka miwili?” Hili ni swali nililomuuliza Rais Jakaya Kikwete tukiwa Ikulu, siku ya Ijumaa, Aprili 6, 2012. Hii ndiyo siku alipotangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, ikiongozwa na Jaji Joseph Sinde ...

Read More »

Kardinali Pengo, Askofu Gwajima wasamehe wenye dhambi muuone ufalme wa mbingu

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, wiki iliyopita alitoa tangazo la kumtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi,  Dar es Salaam kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kashfa na matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. ...

Read More »

Chadema la Zitto sawa, hamtambui Mahakama?

Wiki iliyopita ilikuwa ni historia nyingine katika siasa za Tanzania. Tulishuhudia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe akiachia ngazi baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumfukuza uanachama. Zitto amefukuzwa uanachama ukiwa mwendelezo wa harakazi na misigishano ya ndani kwa ndani, kubwa likiwa ni kugombea madaraka. Zilianza kama tetesi, baadae ikathibitika kuwa Zitto akiwa na kundi lake la ...

Read More »

‘Nchi yetu haina dini’

Nchi yetu haina dini. Haya ni maneno maarufu katika masikio ya Watanzania. Mwasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake maneno haya aliyasema mara kwa mara. Katika moja ya hotuba zake, alisema: “Siku moja nikiwa Zanzibar, kuna masheikh, wamevalia baragashia, nikawa nimealikwa kama mgeni rasmi. Nilipowaona wale masheikh nikasema hapa nitarudia ile ile… nikasema, nchi ...

Read More »

CCM inaanguka polepole kama dola ya Warumi

Mwaka 476 kabla ya Kristu kuna historia ya pekee katika dunia ya sasa. Mwaka huu, dunia ilishuhudia kuanguka kwa Dola Kuu ya Warumi (Rome Empire) iliyokuwa imetawala siasa za Ulaya kwa millennia moja, yaani miaka 1,000. Dola hii ilikuwa ikiongozwa kwa imani za miungu (polytheistic) na inaelezwa kuwa iliangushwa na ujio wa dini ya Wakatoliki waliokuwa wakiamini katika Mungu mmoja ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons