JAMHURI YA WAUNGWANA

Miaka 35 bila Sokoine

Alasiri ya Aprili 12, 1984 wakati huo nikiishi Kurasini Highway, nilivuka barabara kwenda Kurasini Shimo la Udongo kuchukua picha zangu za passport kwenye studio moja. Jina la hiyo studio silikumbuki, maana miaka 35 ni mingi, lakini nakumbuka ilikuwa karibu na duka maarufu la ndugu mmoja aliyeitwa King Nose, jirani na Mti Mpana. Nilipovuka barabara na kuyakaribia maduka ya eneo hilo, ...

Read More »

Hongera Ridhiwani, umeonyesha njia

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amefanya jambo lenye manufaa makubwa kwa wanafunzi wa kike jimboni mwake na kwa taifa. Amesimamia ujenzi wa mabweni ya wasichana katika Shule ya Sekondari Mboga, iliyopo Kata ya Msoga mkoani Pwani. Amesukumwa na azima yake ya kuona mtoto wa kike anasoma kwa bidii katika mazingira mazuri ili afikie ndoto alizojiwekea. Tumeambiwa kuwa mabweni hayo yatahifadhi ...

Read More »

Rais Magufuli wasaidie wanyonge hawa

Jumamosi iliyopita nilikuwa jijini Arusha. Nikiwa nimeegesha gari kwa ajili ya kupokea simu, nikamwona mama aliyeonekana mwenye mawazo mengi. Hakuwa na furaha usoni. Hapa ni jirani na Uwanja wa Ndege wa Kisongo. Sikuhitaji kumuuliza maswali mengi. Nilichofanya baada ya kumtazama, nilimwita. Akasogea akionekana mwenye shaka nyingi. Nilimuuliza anakokwenda. Akajibu kuwa anakwenda Soko la Kilombero ambako anauza mbogamboga. Kwa namna nilivyomwona ...

Read More »

Kenya wametutega nasi tumeingia

Sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ambayo ni sheria ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tumeiridhia na imeshaanza kutumika. Maelezo ya wakubwa ni kwamba sheria hii inalenga kupunguza uzito wa shehena inayopakiwa kwenye malori, lengo kuu likiwa ni kulinda barabara zetu. Hii ndiyo sababu kuu kati ya sababu zote zilizowashawishi viongozi wetu kutunga sheria hii. Sheria ilipaswa ...

Read More »

Siasa zisiwagawe mama zetu

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake yalifikia kilele wiki iliyopita. Shamrashamra zilikuwa nyingi karibu maeneo yote ndani na nje ya nchi. Wanaotambua na kuthamini utu wa mwanamke, kwao hadhi ya mwanamke iko palepale muda wote. Hawasubiri siku maalumu kulitambua au kulionyesha hilo. Mkoani Geita kuna tukio lililonishawishi kuandika haya ninayoandika leo. Si jambo zuri kwa umoja na mustakabali wa mama zetu. ...

Read More »

Tusishangilie kuua upinzani

Nichukue fursa hii kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki wa Ruge Mutahaba, pamoja na Watanzania wote walionufaishwa na kipawa cha mzalendo huyu. Umati wa watu waliojitokeza na wanaoendelea kujitokeza kumlilia Ruge unadhihirisha wazi aina au muundo wa kibinadamu wa Ruge. Kama asingekuwa mtu mwema, kwa hakika asingeliliwa kwa namna tuliyoiona. Tunaweza kusema mambo mengi, lakini lililo muhimu kutoka kwa Ruge ...

Read More »

Kufungwa Malkia wa Tembo si mwisho wa ujangili

Malkia wa Tembo amefungwa jela miaka 15. Hii ni habari njema kwa wahifadhi. Sijasikia wanaobeza hukumu hiyo, japo wapo wanaoona ni ndogo ikilinganishwa na tembo 430 waliotoweka kutokana na mwongozo wake. Kwenye kesi hii waliofungwa ni wawili. Huu ni “utani”. Haiwezekani tembo 430 wauawe na watu wawili tu. Hatujaambiwa madereva, walenga shabaha, wapagazi, wasafirishaji na wengine wote kwenye mtandao huu ...

Read More »

Semina elekezi zisipuuzwe

Rais John Magufuli alipoingia madarakani alionyesha wazi kutoshabikia suala la ‘semina elekezi’ kwa wateule wa ngazi mbalimbali. Alipotangaza Baraza la Mawaziri alisema wazi kuwa hana mpango wa kuendelea na semina elekezi, bali lililo muhimu ni kwa wateule kuchapa kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni. Bila shaka uamuzi wa rais ulilenga kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma kama ilivyopata ...

Read More »

Nani katuloga?

Wiki iliyopita Kampuni ya Mwananchi ilifanya jambo la maana sana. Iliandaa mjadala muhimu sana uliohusu athari za biashara na matumizi ya mkaa nchini. Nasikitika kutoshiriki mjadala huo. Hizi picha zinazoonekana hapa nilizipata wiki mbili zilizopita bila kujua kungekuwapo mjadala wa aina hiyo. Laiti kama ningejua, nina hakika ningepata nzuri zaidi. Picha hizi ni tone ndani ya bahari. Wote hawa wanaoonekana ...

Read More »

Tusiwe taifa la kuwaza mapumziko

Rais John Magufuli alipozungumza na viongozi wa dini, kwa chini chini kulionekana tofauti za hapa na pale. Tofauti hizo hazikuzungumzwa kwa mwangwi, na kwa maana hiyo ilisaidia kutoibua hisia za utengano. Kiongozi mmoja wa Kikristo alitoa maombi yaliyonikumbusha maneno niliyopata kuyaandika miaka kenda iliyopita na kuyarejea mwaka 2013. Katika safu hii niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari: ‘Wakati mwingine Wakristo ...

Read More »

Rais nakuomba utafakari upya (2)

Ndugu Rais, sehemu ya kwanza ya waraka huu niliishia kwenye maneno ya hekima ya uhifadhi yaliyotolewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Agosti 10, 1975. Kwa ufupi Mwalimu alieleza matokeo ya dhambi ya kuteketeza wanyamapori na misitu iliyotendwa na Wazungu katika mataifa yao. Mwalimu alituasa tusitende dhambi hiyo. Ndugu Rais, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ...

Read More »

Rais nakuomba utafakari upya (1)

Ndugu Rais, niruhusu nianze kwa kumnukuu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu alisema: “Kudumisha uhai wa wanyamapori wetu ni suala linalotuhusu sana sisi sote katika Afrika. Viumbe hawa wa porini pamoja na mapori wanamoishi si tu kwamba ni muhimu kama mambo ya kustaajabisha na kuvutia, bali pia kwamba ni sehemu muhimu ya maliasili yetu na ustawi wa maisha yetu ...

Read More »

Wamarekani, Waafrika Kusini watuache

Taifa linahitaji fedha. Haya mambo makubwa ya kimaendeleo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano yatawezekana tu endapo ari ya kubuni, kuendeleza na kusimamia vyanzo vya mapato ya ndani vitatambuliwa na kulindwa kwa nguvu zote. Kama ambavyo Rais John Magufuli amekuwa akisema mara kwa mara, Tanzania ni tajiri kiasi kwamba tukijipanga vema tunaweza kujitosheleza kwa mapato yetu. Dalili zimeanza kuonekana. ...

Read More »

Wavamizi hawa si wa kuchekewa

Nimesoma tamko la serikali linalohusu uamuzi ‘mgumu’ ilioamua kuuchukua dhidi ya wavamizi wa hifadhi mkoani Kigoma. Tathmini iliyofanyika mkoani humo imeonyesha hifadhi za misitu na mapori ya akiba yamevamiwa kwa shughuli za kilimo, ufugaji, ukataji miti na baadhi ya vijiji vimesajiliwa ndani ya maeneo hayo. Uvamizi huu umesababisha athari nyingi zikiwamo za kupotea kwa uoto wa asili na viumbe hai, wakiwamo ...

Read More »

Wanyama wanamalizwa Loliondo

Hadi naandika makala hii, mizogo ya tembo wanane imeonekana katika Kijiji cha Maaloni, Arash, Ngorongoro mkoani Arusha. Miezi miwili, katika Kitongoji cha Karkamoru, Loliondo pekee twiga wanane wameuawa. Watuhumiwa wa ujangili wamekwisha kukamatwa, japo kuna taarifa kuwa wahusika wenyewe bado wamo mitaani. Mauaji hayo ya twiga ni tofauti na haya ya tembo. Tembo wanakufa kwa namna inayotia shaka. Mizoga hii ...

Read More »

Uongozi Hospitali ya Amana haukumtendea haki marehemu

Kumetokea jambo ambalo nimejitahidi nibaki nalo moyoni lakini nafsi imegoma kabisa. Nafsi imegoma kwa sababu naamini kulinyamazia kutahalalisha matukio mengine mengi ya aina hii yaendelee kufanywa. Wiki iliyopita tulipata taarifa ya msiba wa mtu tunayemfahamu. Hana umaarufu, lakini ni binadamu mwenzetu. Huyu alikuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Jina lake ...

Read More »

Mbowe: CCM wamevuruga Uchaguzi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Uchaguzi Mdogo wa Madiwani 43 uliofanyika Jumapili umevurugwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimkakati, hivyo baadhi ya maeneo wamemua kujitoa ikiwamo Mkoa wa Manyara. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (pichani) ameliambia JAMHURI kuwa zamu hii CCM wametumia mbinu ya kuanzisha utaratibu wa kuwapa barua maalum za utambulisho mawakala wa vyama, ambapo wale wa ...

Read More »

 Serikali ikiwa mbaya, CCM itakuwaje nzuri?

Vinara wawili, kati ya wale wanaotuhumiwa kuifanya Loliondo isitawalike, wamewatumia wanasheria wao kuniandikia barua wakitaka ‘nisiwaguse’ kwa chochote kinachoendelea Loliondo. Edward Porokwa na Maanda Ngoitiko, wanaamini kwa kuninyamazisha mimi na Gazeti la JAMHURI, ‘sifa na utukufu’ wao katika Loliondo, vitaendelea kudumu! Maandishi ya wanasheria wao yameandikwa kwa lugha ya mbwembwe nyingi, lakini sikuona mahali walipokanusha yaliyoandikwa juu ya Loliondo na ...

Read More »

Sioni faida za kuwakamata

Wale wanaofanya rejea ya hali ya kisiasa nchini mwetu watakumbuka Augustino Mrema alivyokuwa na nguvu kubwa kisiasa mwaka 1995. Wapo ambao wanaamini hadi leo kuwa kama si mbinu na ushawishi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, historia ya leo ya nchi hii ingekuwa tofauti. Mrema alikuwa na nguvu kubwa kisiasa. Alipendwa na alipata wafuasi wengi kuanzia kwa makabwela ...

Read More »

Funzo kutoka kwenye kodi ya majengo

Mamia kwa maelfu ya wananchi, wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kulipa kodi ya majengo. Muda uliopangwa ulipungua. Umeongezwa kwa wiki kadhaa, lakini bado idadi ya watu wanaojitokeza kulipa ni kubwa mno. Maombi ya wananchi ya kuomba kuongezewa muda yameitikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Muda wa malipo bila faini umeongezwa hadi Julai 31, mwaka huu. Nchini kote kumeripotiwa misururu ya ...

Read More »

Tumuunge mkono Waziri Mkuu Majaliwa

Akiahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julai 5, mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na mambo mengine, alizungumzia sekta ya wanyamapori. Kwa wahifadhi wengi, kauli ya Waziri Mkuu imewapa matumaini mapya yenye kuwawezesha kuona mwanga katika suala zima la uhifadhi nchini. Kama alivyosema, asilimia 28 ya eneo la nchi yetu limetengwa ...

Read More »

Walijaribu ushoga wakafeli, wamegeukia mimba za wanafunzi

Rais John Magufuli ameutolea uamuzi mjadala wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaopata mimba. Rais Magufuli, akiwahutubia wananchi mkoani Pwani, amesema bayana kuwa hayuko tayari kuona wanafunzi wanaotiwa mimba wakiendelea na masomo katika shule za Serikali. Akayaambia mashirika yasiyo ya Serikali kwamba kama yanatetea hao ‘wazazi’ kuendelea na masomo, basi yawaandalie shule, lakini yeye hatokuwa tayari. Msimamo huo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons