Siku nilipoitwa ofisini kwa Mwalimu…

Mwalimu anaumwa? Ni swali linalotuumiza. Hatuamini. Walio karibu wanazo taarifa, lakini wanatakiwa wawe watulivu maana kusambaza taarifa za ugonjwa wa Mwalimu kungeweza kuibua taharuki kwa maelfu na kwa mamilioni ya Watanzania waliompenda. Mwalimu ametoka Butiama Septemba 23, 1999. Amewasili Msasani usiku. Amepumzika. Usiku wote ninawaza namna ya kufanya, maana tumenong’onezwa kuwa kesho atakwenda kwenye  matibabu…

Read More

Tusiache viwanja vya Jangwani vitoweke

Uwanja wa Jangwani jijini Dar es Salaam umebeba historia muhimu katika taifa letu. Mikutano kadhaa kipindi kile cha harakati za kudai Uhuru ilifanyika hapo. Jangwani imeendelea kujizoea umaarufu hata baada ya Uhuru. Mikutano mingi mikubwa imeendeshwa Jangwani. Mikutano ya kisiasa ya vyama mbalimbali imefanyika hapo. Mkutano mkubwa wa Baba Mtakatifu Yohane Paulo II ulifanyika Jangwani…

Read More

Kwa mfumo huu Rais ataendelea ‘kulia’

Baada ya panguapangua mkoani Morogoro iliyogusa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi na Mkurugenzi wa Maendeleo (DED) wa Wilaya ya Malinyi, nikakumbuka makala niliyoiandika takriban miaka miwili iliyopita. Kwenye makala hiyo nilisema Charles Keenja aliongoza vizuri sana Tume ya Jiji la Dar es Salaam. Alifanya mambo mengi, makubwa na mazuri ambayo…

Read More

Bado machozi ya wanyonge ni mengi

Wiki kadhaa zilizopita Rais John Magufuli alitoa kauli nzuri yenye kuleta matumaini kwa waliopoteza au walioelekea kupoteza matumaini. Julai 18, mwaka huu, akiwa Kongwa mkoani Dodoma, alitamka maneno haya: “Mlinichagua kwa ajili ya watu wote, hasa wanyonge wanaopata shida. Siwezi nikatawala nchi ya machozi. Machozi haya yananiumiza. Siwezi kutawala wanaosikitika, wako kwenye unyonge na unyonge wenyewe…

Read More

Tusibweteke kwa elimu bure

Julai 3, mwaka 1964 Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alizungumza na watoto katika Ikulu ya Dar es Salaam. Kupitia mazungumzo hayo, alizungumza pia na watoto wote nchini kwa njia ya redio. Aliwaeleza watoto wajibu walionao kwa wakati huo, ikiwa ni maandalizi ya wao wakiwa wakubwa kubeba mzigo mkubwa wa kuleta maendeleo ya taifa…

Read More