Habari za Kimataifa

Trump arudi nyuma katika sera yake ya kuzitenganisha familia

Rais Donald Trump wa Marekani amesitisha sera yake uhamiaji iliyokuwa inalazimu kuzitenganisha familia za wahamiaji wanaobainika kuvuka mipaka kinyume cha sheria na watoto wao. Pamoja na kulegeza msimamo huo kutokana na kulalamikiwa kwa sera hiyo ndani na nje ya taifa hilo, Trump amesisitiza kwamba bado ataendelea kuilinda mipaka yake. Rais Trump ambaye tangu kuingia kwake madarakani alionekana kuhitaji sheria kali ...

Read More »

Marekani yajitoa katika baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binaadamu

Marekani imejitoa katika baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa na kulitaja kuwa na ‘unafiki wa kisiasa na lenye upendeleo’. “Taasisi hiyo ya “unafiki na upendeleo inakejeli haki za binaadamu”, amesema mjumbe wa Marekani katika Umoja huo Nikki Haley. Bi Haley mwaka jana alilishutumu baraza hilo kwa kuwa na “upendeleo mkali dhidi ya Israel” na kusema Marekani inatafakari ...

Read More »

Mwanamuziki XXXTentacion auawa kwa kupigwa risasi Florida, Marekani

Mwanamuziki wa nyimbo za rap Marekani XXXTentacion, ambaye alipata umaarufu kwa haraka kupitia albamu zake mbili ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa na miaka 20. Alikuwa anaondoka kwenye duka la kuuza pikipiki kusini mwa Florida Jumatatu pale mtu mwenye bunduki alipomfyatulia risasi. Polisi katika tarafa ya Broward wanasema XXXTentacion, ambaye jina lake Jahseh Onfroy, alikimbizwa hospitalini lakini akathibitishwa kufariki. Alikuwa mara ...

Read More »

Ivan Dukee aibuka mshindi Urais Colombia

Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Colombia, Ivan Dukee amewahutubia wafuasi wake mjini Bogota. Bwana Dukee, mwenye umri wa miaka 41,aliahidi kufanyia marekebisho mkataba wa amani uliyofikiwa kati ya serikali na wapiganaji wa FARC. Alijizolea asilimia 54 ya kura ikiwa ni asilimia kumi na mbili zaidi ya mpinzani wake,Gustavo Petro ambaye ni mpiganaji wa zamani. Bwana Duque anatajwa kuwa ni ...

Read More »

Wahamiaji wakataliwa na nchi za Ulaya Hispania

Meli tatu zimeegesha nchini Hispania,zikiwa mamia ya wahamiaji waliokolewa majini wiki iliyopita wakitokea nchini Libya.Wameorodheshwa na kuendelea kupatiwa matibabu na misaada. Serikali ya Hispania imekubali kuwachukua,baada ya Italia na Malta kukataa meli hizo zilizowaokoa wahamiaji hao kuegesha katika bandari.Tukio hili limezua mjadala wa kisiasa Ulaya. Shrika la msalaba mwekundu,limezitaka nchi za jumuiya ya Ulaya,kuiga mfano wa Hispania kuonyesha mshikamano katika ...

Read More »

Marekani inaitaka Korea Kaskazini kuangamiza silaha ifikapo 2020

Marekani ina matumaini ya kuanza kuona shughuli ya kuangamizwa silaha nchini Korea Kaskazini ifikapo mwaka 2020, mwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Mike Pompeo. Matamshi yake aliyoyatoa alipofanya ziara nchini Korea Kusini, yanafuataia mkutano kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un. Walisaini makubaliano ya kufanya kazi katika kuangamiza kabisa silaha za ...

Read More »

Kim Jong-un na Trump waalika kwenye Nchi Zao

Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington. Kiongozi huyo alipewa mwaliko wakati wa mkutano wa historia baina ya wawili hao nchini Singapore Jumanne. Kim pia alimwalika pia Trump kutembelea Pyongyang. “Viongozi ao wawili wakuu walikubali mwaliko wa kila mmoja,” ...

Read More »

Donald Trump na Kim Jong Un wakutana na Kufanya Makubaliano

Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore. Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao. Mkutano huo ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya ...

Read More »

Trump na Kim Jong-un wawasili Singapore

Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wamewasili Singapore kwa ajili ya mkutano wao unaoelezwa kuwa wa kihistoria. Trump aliwasili saa chache tu baada ya Kim kuwasili na ujumbe wake. Mkutano wao ambao ni wa kwanza utafanyika siku ya Jumanne katika kisiwa cha Sentosa. Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa ...

Read More »

Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani

Mchungaji wa Kiprotestanti Docho Eshete aliyekuwa akibatiza watu katika ziwa Ayaba kusini mwa Ethiopia ameuawa na mamba. Mashambulizi yaliyo karibu na mji wa Arba Minch yanahusishwa na kupunguza idadi ya samaki ambacho ni chakula cha Mamba na hivyo kuanza kuvamia watu na kuwaua. Mchungaji, Docho, ndo kwanza alikuwa ameanza kumbatiza mfuasi wa kwanza kati ya themanini waliokwenda kufanyiwa huduma hiyo ...

Read More »

Kenya Yapiga Marufuku Kuwatembelea Watoto Shuleni

Wizara ya Elimu nchini Kenya imeivunjilia mbali bodi ya usimamizi wa shule ya Moi Girls na kutangaza kwamba ni marufuku kuwatembelea watoto shuleni baada ya mapumziko ya katikati ya muhula kwa shule zote za upili za umma. Hii ni kufuatia uchunguzi unaoendelea kubaini kesi ya ubakaji wa mwanafunzi katika shule hiyo. Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed alitoa agizo kwa ...

Read More »

Wakenya waandamana dhidi ya rushwa Kenya baada ya ufichuzi wa uporaji mkubwa

Raia wa Kenya wanafanya maandamano makubwa katika miji mikubwa ya nchi hiyo kulaani ufisadi wa mabilioni ya dola katika serikali. Mijadala juu ya kashfa za Ufisadi imetawala mitandao mbali mbali ya kijamii kupitia mada: #TakeBackOurCountry, #STOPTheseTHIEVES, #SitasimamaMaovuYakitawala na #NotYetMadaraka. Katika kampeni hiyo inayoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter Wakenya wanasema wamechoshwa na visa vya maafisa wa ...

Read More »

Mhubiri awaomba waumini wamnunulie ndege yake ya nne Marekani

Mhubiri mmoja wa Kiinjilisti nchini Marekani amewaomba waumini wake kuchanga pesa za kumsaidia kununua ndege yake ya nne. Amesema hata kama Yesu angekuwepo siku hizi, “hangekuwa anapanda punda”. Jesse Duplantis amesema Mungu amemwambia anunue ndege aina ya Falcoln 7X ambayo inagharimu $54m (£41m). Ameongeza kwamba alikuwa na shaka pia kuhusu kuendelea na ununuzi huo mwanzoni, lakini Mungu alimwambia: “Sikukwambia uilipie. ...

Read More »

RAIS WA MALI AMTAKA ALIYEMWOKOA MTOTO UFARANSA ARUDI NYUMBANI

RAIS wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta amemtaka kijana shujaa, mhamiaji kutoka nchini kwake, Mamoudou Gassama aliyemwokoa mtoto mdogo aliyekuwa amening’inia kwenye kibaraza cha ghorofa ya nne katika jengo refu jijini Paris, Ufaransa arudi nyumbani kwani amemwandalia kazi Jeshini.   Balozi wa Mali nchini Ufaransa, Toumani Djimé Diallo akizungumza na kijana huyo katika ofisi za ubalozi wa nchi hiyo na kumpa pongezi kutoka ...

Read More »

Mugabe Agoma Kwenda Bungeni Kuhojiwa

RAIS wa zamani wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe, amepuuza wito wa Bunge la nchi hiyo likimtaka afike mbele ya kamati yake inayochunguza mapato ya almasi. Mbunge anayeongoza kamati ya madini na nishati amesema Mugabe alikuwa amebakiwa na fursa moja tu ya kuripoti mbele ya kamati hiyo ili kujibu maswali husika.   “Tulimwandikia barua rais huyo wa zamani mara mbili ili ...

Read More »

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich apata uraia Israel

Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya England Roman Abramovich, amesafiri kwa ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata haki ya uraia wa Israel. Maafisa wa uhamiaji wamesema kuwa alihojiwa wiki iliyopita kwenye ubalozi wa Israel mjini Moscow. Alikabiliwa na tatizo la kupata upya viza nchini Uingereza katika kinachoonekana kuwa na uhusiano na mzozo ...

Read More »

Mhamiaji wa Mali Apongezwa kumuokoa Mtoto Ghorofani

Mhamiaji wa Mali amepongezwa kama shujaa baada ya kukwea sehemu ya mbele ya jengo la ghorofa mjini Paris kumuokoa mtoto aliekuwa kwenye uzio wa ubaraza wa ghorofa ya nne kwenye jengo refu. Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Alivuka kutoka kwenye ubaraza mmoja hadi mwingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto ...

Read More »

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla

  Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huo ndio wa pili kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un. Unafanyika wakati pande hizo zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Siku ya Alhamisi Rais wa ...

Read More »

Sheria mpya ya kulinda faragha yazinduliwa Ulaya

Sheria mpya ya kulinda faragha ya mtu Ulaya imeanza kutekelezwa leo Ijumaa, ikisimamia zama zinazo kusudia kulinda faragha ya raia na kurekebisha jinsi makampuni yanavyo kusanya, kutumia na kuhifadhi taarifa zao. Sheria hiyo mpya inaanza kutumika wakati ambapo kampuni kubwa ya mitandao ya jamii Facebook ikiwa inakosolewa nchini Marekani kwa kashfa ya kushindwa kulinda faragha za watu. Sheria ya Kulinda ...

Read More »

Watu 50 wafariki Dunia kwenye ajali ya boti DR Congo

Watu 50 wamefariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya boti kuzama kwenye mto kaskazini mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa Richard Mboyo Iluka, naibu gavana wa jimbo la Tshuapa, boti hilo lilikuwa limewabeba abiria wengi, wengi wao wafanyabiashara, waliokuwa wanasafiri kutoka eneo la Monkoto kwenda Mbandaka. Amesema watu wengine 50 wamenusurika. Gavana huyu amesema hadi sasa hawajafahamu chanzo ...

Read More »

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) LATILIA MKAZO SWALA LA KUUMWA NA NYOKA

Nchi wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia. Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka. WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani. ...

Read More »

Mwanamgambo aliyejaribu kumpindua Fidel Castro afariki

Luis Posada Carriles, mzaliwa wa Cuba na ajenti za zamani wa CIA ambaye alitumia miaka yake mingi akijaribu kuipindua serikali ya kikomunisti ya Cuba amefarikia huko Florida akiwa na miaka 90. Bw Posada Carriles alikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa rais wa zamani wa Cuba Fidel Casto. Alishiriki katika uvamizi ulioungwa mkono na Marekani mwaka 1961 na analaumiwa kwa kuiangusha ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons