Habari za Kimataifa

Mhamiaji wa Mali Apongezwa kumuokoa Mtoto Ghorofani

Mhamiaji wa Mali amepongezwa kama shujaa baada ya kukwea sehemu ya mbele ya jengo la ghorofa mjini Paris kumuokoa mtoto aliekuwa kwenye uzio wa ubaraza wa ghorofa ya nne kwenye jengo refu. Video ya Mamoudou Gassam akimuokoa mtoto ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Alivuka kutoka kwenye ubaraza mmoja hadi mwingine kwa muda wa chini ya dakika moja akamvuta mtoto ...

Read More »

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla

  Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huo ndio wa pili kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un. Unafanyika wakati pande hizo zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Siku ya Alhamisi Rais wa ...

Read More »

Sheria mpya ya kulinda faragha yazinduliwa Ulaya

Sheria mpya ya kulinda faragha ya mtu Ulaya imeanza kutekelezwa leo Ijumaa, ikisimamia zama zinazo kusudia kulinda faragha ya raia na kurekebisha jinsi makampuni yanavyo kusanya, kutumia na kuhifadhi taarifa zao. Sheria hiyo mpya inaanza kutumika wakati ambapo kampuni kubwa ya mitandao ya jamii Facebook ikiwa inakosolewa nchini Marekani kwa kashfa ya kushindwa kulinda faragha za watu. Sheria ya Kulinda ...

Read More »

Watu 50 wafariki Dunia kwenye ajali ya boti DR Congo

Watu 50 wamefariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya boti kuzama kwenye mto kaskazini mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa Richard Mboyo Iluka, naibu gavana wa jimbo la Tshuapa, boti hilo lilikuwa limewabeba abiria wengi, wengi wao wafanyabiashara, waliokuwa wanasafiri kutoka eneo la Monkoto kwenda Mbandaka. Amesema watu wengine 50 wamenusurika. Gavana huyu amesema hadi sasa hawajafahamu chanzo ...

Read More »

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO) LATILIA MKAZO SWALA LA KUUMWA NA NYOKA

Nchi wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia. Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka. WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani. ...

Read More »

Mwanamgambo aliyejaribu kumpindua Fidel Castro afariki

Luis Posada Carriles, mzaliwa wa Cuba na ajenti za zamani wa CIA ambaye alitumia miaka yake mingi akijaribu kuipindua serikali ya kikomunisti ya Cuba amefarikia huko Florida akiwa na miaka 90. Bw Posada Carriles alikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa rais wa zamani wa Cuba Fidel Casto. Alishiriki katika uvamizi ulioungwa mkono na Marekani mwaka 1961 na analaumiwa kwa kuiangusha ...

Read More »

Korea Kaskazini Wamtusi Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence

Afisa wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini amemlaumu Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kwa kuwa “mjinga” na kuonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatafeli. Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo. Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa. Korea ...

Read More »

Joyce Msuya ateuliwa naibu katibu mkuu wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira duniani, UNEP. Ofisi kuu za shirika hilo la UN lipo jijini Nairobi, Kenya. Bi Msuya atachukua nafasi ya Ibrahim Thiaw wa Mauritania, ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu. Hadi wakati wa kuteuliwa kwake Jumatatu, Bi Msuya ...

Read More »

RAIS WA GHANA ATOA AMRI YA KUKAMATWA KWA MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA SOKA LA GHANA

Rais wa Ghana Akufo-Addo amemrisha kukamatwa mwenyekiti wa shirikisho la kandanda la Ghana Kwesi Nyantekyi, ambaye pia ni makamu wa rais wa kwanza wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF. Hatua hiyo inafuatia makala moja ya uchunguzi ambayo inamhusisha Kwasi Nyantekyi na vitendo vya ulaghai. Inadaiwa kuwa alitumia jina la rais wakati akipanga na kutekeleza ulaghai huo. Uchunguzi huu uliofanywa ...

Read More »

RAIS DONALD TRUMP AHOFIA MKUTANO NA JONG-UN

Rais Trump ametilia shaka kufanyika mkutano adimu na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi june huko Singapore . Amesisitiza kuwa hata hivyo Korea kaskazini itapaswa kutimiza vigezo vilivyowekwa ambayo ni nadra kutokea. Korea Kaskazini ilikwisha sema kuwa inaweza kujiondoa katika mkutano huo iwapo Marekani inasisitiza suala la kuachana na mpango wa silaha za nyuklia. Rais Trump amezungumzia mkutano huo,mara ...

Read More »

Nicolas Maduro Ashinda Tena Uchaguzi Nchini Venuzuela

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro, ameshinda uchanguzi kwa awamu ya sita kwenye uchaguzi uliokubwa na ususiaji kutoka chama kikuu cha upizani kwa madai ya udanganyifu wa kura. Kutokana na upungufu wa chakula unaosababishwa na changamoto za kiuchumi , asilimia 46, ya wapinga kura ndio waliojitokeza na kupiga kura. Mpizani mkuu Henri Falcon , alipinga matokeo hayo punde tu baada ya ...

Read More »

Matokeo rasmi ya kura ya maoni kutangazwa leo Burundi

Tume ya uchaguzi nchini Burundi imesema itatangaza matokeo ya kura ya maoni baadaye hii leo licha ya kiongozi wa upinzani, Agathon Rwasa kusema kuwa hatakubali matokeo hayo. Rwasa ameitaka tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo na kuitisha kura upya kwa madai kuwa kura hiyo iligubikwa na udanganyifu na vitisho kwa wafuasi wake. Matokeo ya awali yalionyesha kuwa kura ya ‘ ...

Read More »

Trump ataka kujua kama FBI walichunguza kampeni zake

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anahitaji uchunguzi kufanyika ilikubaini kama shirika la upelelezi la FBI lilijipenyeza kuchunguza kampeni zake kwa maslahi ya kisiasa. Kupitia ukurasa wake wa tweeter,Trump amesema kuwa anahitaji kujua kama mtangulizi wake aliagiza kitu kama hicho kufanyika. Katika ombi ambalo hii leo siku ya jumatatu Trump anataka kulitoa rasmi,linakuja kufuatia baada ya vyombo vya habari ...

Read More »

Burundi wanapiga kura ya maoni leo kutoa maamuzi ya muda wa muhula wa Rais kukaa madarakani kutoka miaka tano hadi saba

Burundi inafanya kura ya maamuzi hapo inayopania kuongeza muhula wa rais kutoka miaka tano hadi saba. Marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda rais Pierre Nkurunziza akaongoza taifa hilo hadi mwaka wa 2034. Lakini kampeni hizo zimechafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo ya maamuzi huo na pia madai kwamba serikali imekuwa ikiwatisha wafuasi wa upinzani. Umoja wa ...

Read More »

Ukidanganya Kwenye Mtandao Kenya Adhabu dolla 50,000 za Kimarekani

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameidhinisha Mswada wa Sheria za Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni wa 2018 kuwa Sheria, hatua itakayotoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makossa ya mtandaoni. Sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya dola 50,000 za Marekani au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi. ...

Read More »

Kim Jong-un atishia kufuta mkutano wake na Trump

  Korea Kaskazini imesema huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia. Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni. Hayo yamejiri baada ya ...

Read More »

Marekani Kufungua Ubalozi Mpya leo Mjini Jerusalem

Marekani itafunguq ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa. Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner. Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria. Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo ...

Read More »

Chombo cha Satelaiti kilichoundwa Kenya kitarushwa katika anga za juu leo kutoka Japan

Wanasayansi wa anga za juu kutoka Kenya waliokiunda chombo hicho tayari wako katika makao ya Uchunguzi wa Sayansi ya Anga za juu nchini Japan, (JAXA) ambapo chombo hicho kitarushwa kutoka huko. Nchini Kenya kwenyewe raia wataweza kufuatilia shughuli hiyo moja kwa moja kwenye mtandao wa You Tube, na sherehe maalumu ya kushuhudia imeandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi. Satelaiti hiyo ...

Read More »

Donald Trump alijitungia barua kuhusu afya yake, daktari Harold Bornstein asema

Aliyekuwa daktari wa Donald Trump amesema kwamba si yeye aliyeiandika barua iliyomweleza mgombea huyo wa chama cha Republican wakati huo kuwa aliyekuwa na “afya nzuri ajabu”, vyombo vya habari Marekani vinasema. “[Trump] alitunga na kuamrisha kuandika kwa barua yote,” Harold Bornstein aliambia runinga ya CNN Jumanne. Ikulu ya White House haijazungumzia tuhuma hizo za daktari huyo. Bw Bornstein pia amesema ...

Read More »

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kulakiwa na Donald Trump Marekani

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la kutoka bara Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump White House atakapokutana na kiongozi huo kwa mashauriano rasmi mjini Washington baadaye leo. Marais wengine wa Afrika wamewahi kukutana na Bw Trump akiwa rais, wakiwemo Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, lakini nje ya Marekani. ...

Read More »

Wakimbizi 21 wa Congo wafikishwa kortini Rwanda kwa kufanya maandamano

Wakimbizi 21 kutoka kambi hiyo jana wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kuunda kundi la uhalifu na kufanya maandamano kinyume cha sheria. Wakati mvutano ukiendelea baina ya polisi wa Rwanda na wakimbizi kutoka Congo katika kambi ya Kiziba magharibi mwa Rwanda, mwendesha mashtaka anataka wapewe kifungo zaidi cha siku 30 ili kumpa muda wa kukusanya ushahidi zaidi. Wao wanasema wanazuiliwa kinyume ...

Read More »

Kim aahidi ‘historia mpya’ ya Korea mbili

Kim Jong-un ameahidi ‘historia mpya’ katika uhusiano na jirani yake wakati akiwa kiongozi wa kwanza wa Korea kaskazini kuingi Korea ksuini tangu kumalizika kwa vita vya Korea mnamo 1953. Katika hatua ilioshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina kiongozi wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa mikono katika mpaka huo. Kim amesema huu ni ‘mwanzo’ wa amani, baada ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons