Habari za Kimataifa

Wahamiaji waandamana Israel

Mamia ya wahamiaji wa Kiafrika waishio nchini Israel wameandamana huku wakiendelea na mgomo wa kutokula wakipinga sera mpya ya Israel yenye utata ya kutaka ama kuwafunga na kisha kuwarejesha makwao. Wahamiaji hao walitembea umbali mfupi kutoka kituo cha wazi cha Holot hadi gereza la Saharonim, wakipaza sauti na kutoa ishara za kutaka kuachiwa kwa wafungwa wenzao ambao wapo magerezani nchini ...

Read More »

WACHUNGAJI 6 WA MAKANISA RWANDA WAKAMATWA NA POLISI

  Polisi nchini Rwanda imetangaza kuwatia kizuizini wachungaji 6 na viongozi wa makanisa kutoka baadhi ya makanisa yaliyofungwa kwa amri ya serikali ya nchi hiyo. Wiki iliyopita serikali ya nchi hiyo iliamrisha kufungwa kwa makanisa zaidi ya 700 kwa madai ya kutotimiza kanuni za ujenzi wa makanisa yao. Miongoni mwa waliokamatwa ni kasisi Askofu Innocent Rugagi, kiongozi wa kanisa la ...

Read More »

BENJAMIN NYETANYAHU AKUTANA NA TRUMP KUJADILI TISHIO LA IRAN

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu yuko mjini Washington kukutana na Rais Donald Trump kutafuta njia za kuzuia jeshi la Iran kuongeza himaya yake Mashariki ya Kati. Mazungumzo hayo yamekuja wakati Trump anajaribu kupima iwapo ni busara kwa Marekani kujiondosha katika mkataba wa kimataifa uliosainiwa na Iran wenye kusudio la kuzuia nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia, makubaliano ambayo Netanyahu ...

Read More »

BAADHI YA WAUGANDA WAMKOSOA RAIS MUSEVENI KWA HATUA ALIYOICHUKUA, YA KUWAFUKUZA IGP NA WAZIRI WA ULINZI

Habari za kufukuzwa kazi Jenerali Kale Kayihura katika nafasi ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na Luteni Jenerali HenryTumukunde kama waziri wa ulinzi zimepokelewa kwa hisia tofauti na wasomaji wa mitandao nchini Uganda. Wengi wa wachangiaji katika mitandao ya jamii wamemkosoa Rais Museveni katika hatua yake ya kuwafukuza viongozi hao na wengine wamewafurahia na kusema ilikuwa ikitegemewa kuwa hilo litatokea ...

Read More »

RIPOTI MAALUM YABAINI KIKUNDI CHA ADF KILIHUSIKA NA MAUAJI YA ASKARI WA TANZANIA NCHINI DRC RC

Kikundi cha waasi wa Alliance of Democratic Forces (ADF) kimetajwa na ripoti maalum ya uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuwa kilihusika na mauaji ya askari wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UN, ushahidi uliopatikana unaonyesha ADF ndio walifanya shambulizi hilo la kushtukiza na kusababisha vifo vya askari hao waliokuwa wakilinda ...

Read More »

Manowari ya Marekani yatia nanga Vietnam

Mamowari ya Marekani Carl Vinson inafanya ziara ya kihistoria nchini Vietnam kwa mara ya kwanza kwa meli ya aina hiyo kuzuru Vietnam tangu vita kumazilika. Manowari hiyo inayotumia nishati ya nyuklia itatia nanga katika bandari wa Danang ambapo wanajeshi wa Marekai walitua kwanza wakati wa vita. Hii inamaana ya kuonyesha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo. Lakini wadadisi wanasema ...

Read More »

Mtu Mmoja Ajitandika Risasi Nje ya Ikulu ya Marekani

Mwanamume mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani ya White House mjini Washington, kikosi cha kumlinda rais kimesema Kikosi hicho kilisema kuwa mwanamume huyo alikaribia ua unaozunguka Ikulu katika barabara ya Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa. Hakuna mtu aliyejeruhiwa, kulingana na polisi. Rais Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu. Yuko katika kasri lake ...

Read More »

BAADA YA RAIS TRUMP KUTOA KAULI TATA, KUHUSU BARA LA AFRIKA, SASA WAZIRI WAKE REX TILLERSON KUJA AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson, anatarajiwa kufanya ziara ya siku nane barani Afrika kuanzia Jumanne wiki ijayo. Hii itakuwa ziara yake ya kwanza kwenye bara hilo kama waziri. Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani Alhamisi ilisema kuwa Tillerson atazuru Kenya, Ethiopia, Djibouti, Chad na Nigeria, kwenye safari ambayo itakamilika tarehe 13 mwezi huu. ...

Read More »

WAFANYABIASHARA WAKUBWA WAKERWA NA RAIS DOLD TRUMP

Washirika wakubwa wa biashara wa Marekani wamekasirishwa na tangazo la Rais wa nchi hiyo Donald Trump juu ya mpango wa kutoza ushuru kwa bidhaa za chuma na aluminiam zinazoingizwa. Umoja wa Ulaya na Canada kwa pamoja zimesema zitafanyia kazi uamuzi huo, kupingana na tamko hilo. Rais wa Tume ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema uamuzi huo wa Marekani wa kutoza ...

Read More »

HUYU HAPA KAMPENI MENEJA WA DONALD TRUMP KWENYE UCHAGUZI WA 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amemtaja meneja wa kampeni zake za urais mwaka 2020. Brad Parscale mtaalam wa mitandao, alifanya kazi katika kampeni za Trump 2016 na alisifiwa sana kwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri jambo linalotajwa kumpa ushindi Trump. Parscale atatumika katika kampeni za uchaguzi mdogo baadae mwaka huu. Trump anasema Parscale ni mtu sahihi na amekuwa akifanya kila ...

Read More »

Korea Kaskazini ‘inaisaidia Syria na silaha za kemikali’

Korea Kaskazini imekuwa ikiwatumia vifaa Syria ambavyo vinaweza tumika katika kutengeneza silaha za kemikali, ripoti ya chombo cha habari Marekani imesema kikinukuu ripoti kutoka Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa ripoti ya UN ambayo haijatolewa, wataalam wa bakora Pyongyang wameonekana katika viwanda vya kutengenezea silaha nchini Syria, gazeti la New York Times imesema. Shutuma hizo zinakuja baada ya ripoti mpya ...

Read More »

MKE WA JACOB ZUMA ATEULIWA KUWA WAZIRI WA OFISI YA RAIS AFRIKA KUSINI

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri. Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo. Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen. Palipotokea anguko la thamani ya randi alilazimika kumfukuza Rooyen na kumchagua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia ...

Read More »

SYRIA WAPUMZIKA KUPIGANA KWA MUDA, KUWAPA KUOKOA ROHO ZA RAIA

Rais wa Urusi Vladmir Putin ameagiza usitishwaji wa mapigano kwa takriban saa tano katika mashambulizi yanayofanywa na serikali ya Syria katika maeneo ya mashariki mwa eneo la Ghouta linalodhibitiwa na waasi. Usitishwaji huo wa mapigano unaanza leo Jumanne na utajumuisha kuundwa kwa kile kinachoitwa ” Njia ya Hisani” kuwawezesha raia kuondoka katika eneo hilo lenye mapigano makali. Waziri wa Ulinzi ...

Read More »

Serikali ya Nigeria yaomba radhi utekwaji wasichana

Kumekuwa na ongezeko la hali ya hasira kwa wazazi wa wasichana wanaodaiwa kutekwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram ambao siku ya jumatatu wamevamia shule moja ya wasichana katika mji wa Daptch nchini humo. Wazazi wa wanafunzi hao waliokuwa waliokuwa bweni shule Dapchi wamesema kuwa hadi sasa hawaelewi mahala walipo watoto wao. Serikali ya Nigeria imetoa kauli ya kuomba ...

Read More »

DONALD TRUMP: WALIMU WARUSIWE KWENDA NA BUNDUKI MASHULENI

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule kama lile lililowaua watu 17 wiki iliopita mjini Florida. ”Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja”, alisema. Bwana Trump alitoa pendekezo hilo huku manusura wa shambulio hilo la tarehe 14 mwezi Februari wakimtaka kuhakikisha kwamba shambulio kama hilo halitokei tena. Rais ...

Read More »

BAADHI YA WAZANZIBAR WAPAMBANA KUUVUNJA MUUNGANO WA TANZANIA NA TANZANIA BARA

  Kundi la wanaharakati lenye wafuasi zaidi ya elfu arobaini kutoka visiwani Zanzibar wamefungua kesi katika mahamaka ya Afrika Mashariki wakitaka Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar uvunjwe kwa madai kwamba hauna uhalali. Rashid Salum Adiy ambae ni mmoja wa wanaharakati waliofungua kesi hiyo, amesema kwamba, wamekwenda katika mahakama hiyo ya Afrika Mashariki baada ya mahakama kuu Zanzibar kushindwa kuisikiliza ...

Read More »

Cyril Ramaphosa Achaguliwa Kuwa Rais Mpya wa Afrika Kusini, Achukua Nafasi ya Jacob Zuma

Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril Ramaphosa amepishwa kuwa rais wa Afrika Kusini baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu. Rais huyo mpya alikuwa mtu wa pekee aliyeteuliwa siku ya Alhamisi huku uteuzi huo ukiungwa mkono kwa shangwe bungeni. Bwana Zuma alikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa chama chake cha ANC kilichomtaka ajiuzulu la sivyo akabiliwe ...

Read More »

MWANAFUNZI AWAMIMINIA RISASI WANAFUNZI WENZAKE NA KUWAUA 17, MAREKANI

  Watu 17 wameuawa katika mauaji ya watu wengi yaliyofanywa katika shule moja huko Florida Marekani. Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa huyo ametajwa kwa jina la Nikolaus Cruz mwenye umri wa miaka 19 na kwamba alikuwa mwanafunzi katika shule hiyo aliyoishambulia. Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa amebeba bunduki ya kisasa, alianza kushambulia bila ya mpangilio nje ya shule hiyo kabla ya ...

Read More »

TANZIA: Kiongozi Mkuu wa Upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai Afariki

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini. Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri wa 65, na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo. Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters ...

Read More »

RAIS WA AFRIKA KUSINI, JACOB ZUMA ANG’ATUKA MADARAKANI

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake. Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC. Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni. Zuma mwenye umri wa miaka 75 ...

Read More »

Korea Kaskazini Yaonyesha Nguvu za Kijeshi

Siku moja kabla ya kufunguliwa kwa michezo ya Olympiki ya Majira ya Baridi nchini Korea Kusini, Korea Kaskazini imefanya gwaride kubwa la kijeshi kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa jeshi la nchi hiyo. Afisa wa Korea Kusini ambaye hakutaka kutajwa jina, amesema kiasi ya wanajeshi zaidi ya 13,000 walishiriki katika gwaride hilo lililokuwa na lengo la kuonesha nguvu ya kijeshi ...

Read More »

Jacob Zuma Apewa Masaa 48 Kung’atuka Madarakani

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo. Kwa mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC. Duru zinasema ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons