Habari za Kimataifa

RIPOTI YA EU YAWAKERA WAKENYA

Serikali ya Kenya imekasirishwa na ripoti iliotolewa na kiongozi wa Muungano wa Ulaya kuhusu uchaguzi mkuu wa urais mwaka uliopita. Marietje Schaake alitoa ripoti mapema siku ya Jumatano katika mji mkuu wa Ubelgiji , Brussels baada ya kusema kuwa serikali ya Kenya haikuwa tayari kukutana naye. Taarifa kutoka ubalozi wa Kenya mjini Brussels inasema kuwa madai hayo sio ya ukweli ...

Read More »

Mamia ya Wahamiaji Wahofiwa Kuzama Libya

Mamia ya watu wanahofiwa kupotea baada ya boti iliyobeba wahamiaji kuzama pwani ya Libya. Walinzi wa majini wa Libya wanasema kuwa watu mia tatu wameokolewa kutoka boti nyingine tatu zilizopata dhoruba. Walioopona katika ajali hiyo ya majini wanasema kuwa walitumia masaa kadhaa ndani ya maji kabla ya kuokolewa. Tukio hili ni la karibuni Zaidi kutokea tangu kuanza kwa mwaka mpya. ...

Read More »

MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YASABABISHA VIFO VYA WATU 80 NIGERIA

Takribani watu 80 wameuawa nchini Nigeria katika jimbo la Benue tangu kuanza kwa mwaka huu mpya. Hiyo ni kwa mujibu wa ofisa wa wakala wa dharura. Mapigano kati ya wafugaji wa jamii ya Fulani na wakulima yamekuwa yakiongezeka tangu mwaka ulipita yaani 2017 na huku maafisa wanasema mashambulizi bado yanaendelea. Milipuko ya vurugu imekuwa ikitokea katika eneo la kati la ...

Read More »

Meli ya Kubeba mafuta Yateketea kwa Moto Pwani mwa China

Hali mbaya ya hewa inatatiza juhudi za kuzima moto na kufuja kwa mafuta zaidi ya saa sitini. Meli ya mafuta ya Iran inateketea kwa moto baada ya meli mbili kugongana kusini mwa bahari ya China. Meli hiyo kwa jina Sanchi imebeba tani 136,000 za mafuta. Waokoaji sasa wamepanua shughuli ya utafutaji wa wahudumu 31 wa meli ambao hawajulikani waliko. Ni ...

Read More »

Zimbabwe Yachunguza Shahada ya Uzamifu ya Grace Mugabe

Mamlaka ya kukabiliana na ufisadi nchini Zimbabwe imeanzisha uchunguzi kuhusu shahada ya udaktari iliopewa mkewe Robert Mugabe, Grace Mugabe kulingana na ripoti ya AFP. Phyllis Chikundura ,msemaji wa tume ya kukabiiana na ufisadi nchini humo alithibitisha kuwa kulikuwa na uchunguzi uliokuwa ukiendelea. ”Tumethibitisha kuwa kuna ripoti kama hiyo na kwamba kuna uchunguzi kama huo pia”, alisema. Bi Mugabe alidaiwa kupata ...

Read More »

Mfumko wa bei wasababisha maandamano Tunisia

Mtu mmoja amekufa na wengine watano kujeruhiwa katika maandamano ya kiuchumi katika mji mkuu wa Tunisia, tunis. Maandamano hayo yameenea katika maeneo mengine kumi nchini humo. Uchumi wa nchi hiyo umekua ukitetereka tangu mwaka 2011 wakati kiongozi wa kipindi hicho Zine El Abdine Ben Ali akiondolewa madarakani. Kwa sasa fedha ya Tunisia imeshuka zaidi ikilinganishwa na Uero, Miongoni mwa sababu ...

Read More »

KOREA KASKAZINI NA KOREA KUSINI ZAANZA MAZUNGUMZO

Mkutano huo unaofanyika katika kijiji cha Panmunjom ambapo mazungumzo yao yanahusu uwezekano wa Korea Kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatakayofanyika Korea Kusini mwezi wa pili. Waziri wa muungano wa Korea Kusini , Cho Myoung-Gyon amesema mazungumzo hayo yanajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo ...

Read More »

Jumba la Trump New York Lawaka Moto

Maafisa wa kuzima moto wameitwa katika jumba la Trump Tower katika kisiwa cha Manhattan jijini New York kuzima moto uliokuwa umezuka kwenye ghorofa ya juu ya jengo hilo. Idara ya kuzima moto ya New York imesema moto huo ulidhibitiwa na kwamba hakukuwa na majeruhi. Shirika la habari la CBS News limesema moto huo ulizuka mwendo wa saa moja asubuhi saa ...

Read More »

Mauaji Yaongezeka Yemen

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeua raia 109 katika mashambulizi tofauti ya ndege katika kipindi cha siku 10, wakiwemo watu 14  wa familia moja na kuacha simanzi kubwa katika familia hiyo. Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamie McGoldrick amesema mapigano yanayoendelea nchini humo ni ya hatari na kuhuzunisha kiasi cha kuhitaji msaada kutoka jumuiya za ...

Read More »

KOREA KASKAZINI YAFUNGUA MAWASILIANO YA SIMU NA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini imefungua tena mawasiliano ya simu na Korea Kusini ili kuanzisha mazungumzo kuhusu kushiriki kwake katika mashindano ya msimu wa baridi. Korea Kusini imethibitisha kuwa ilipata simu kutoka Kaskazini leo Jumatano. Hii ni baada ya Kim Jong un kusema kuwa ataanzisha mazungumzo na Korea Kusini kuhusu kutumwa timu kwa mashindano ya msimu wa baridi huko Korea Kusini. Mataifa hayo ...

Read More »

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau Ajitokeza Tena

Kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram Abubakar Shekau, ameonekana kwenye video mpya karibu saa ishirini na nne baada ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa mara ingine kutamka hadharani kuwa kikundi hicho kimesambaratishwa. Huu ni mkanda wa video wa kwanza kutolewa na Shekau baada ya kimya cha miezi kadhaa iliyopita, naye ni mongoni mwa viongozi wanaosakwa kwa hamu ...

Read More »

AJALI: WATU 34 WAUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA KENYA

Habari kutoka Kenya zasema kuwa watu 34 wamefariki katika ajali nyingine mbaya ya barabani, iliyotokea mapema Jumapili asubuhi. Watu 16 wamejeruhiwa wengi wao wakiwa katika hali mahututi, baada ya Basi moja la abiria kugongana ana kwa ana na lori la mizigo, katika maeneo ya barabara ya Sachangwan/ Salgaa, takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Nairobi. Afisa mkuu wa idara ya ...

Read More »

UMOJA WA MATAIFA WALAANI MAUAJI YA RAIA YANAYOFANYWA NA MAJESHI YA SAUDI ARABIA NA WASHIRIKA WAKE NCHINI YEMEN

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeua raia 109 katika mashambulizi tofauti ya ndege katika kipindi cha siku 10, wakiwemo 54 katika soko lenye shughuli nyingi na 14 wa familia moja waliokuwa shambani. Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamie McGoldrick ameyaelezea mapigano yanayoendelea nchini humo kuwa yasiofaa na ya kuhuzunisha. Ikitaja ripoti za awali kutoka ofisi ...

Read More »

Robert Mugabe Kupewa Stahiki Zake Kama Rais Mstaafu

Serikali ya Zimbabwe imeeleza kuwa itampa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo. Robert Mugabe nyumba ya kuishi, magari pamoja na ndege binafsi ya kusafiria ikiwa ni sehemu ya stahiki wanazopatiwa watumishi wa serikali waliostaafu. Pamoja na hayo, pia atapewa watumishi 20, wakiwemo walinzi wake 6 watakaokuwa wanalipwa na serikali ya nchi hiyo, kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald. Rais ...

Read More »

BREAKING: George Weah Ashinda Kiti cha Urais

Mwanasoka bora wa Dunia mwaka 1996, George Weah ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais nchini Liberia baada ya kukamilika kwa duru ya pili ya uchaguzi.

Read More »

Krisimasi Ilikuwa Chungu kwa Waasi ADF, Wachapwa Kutokea Uganda

Jeshi la Wananchi la Uganda (UPDF) limewashambulia waasi wa kikundi cha Allied Democratic Forces (ADF) cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). ADF wanahusishwa na shambulizi la Desemba 7, mwaka huu lililofanyika kwenye kambi ya askari hao ya Simulike, Mashariki mwa DRC na kusababisha vifo vya askari 15 na wengine 44 kujeruhiwa. Gazeti la Daily Monitor la Uganda limemkariri Msemaji ...

Read More »

Hali ni Tete Sudan Kusini

Tangu serikali ya Sudan Kusini kuikamata kambi ya waasi Kusini Magharibi mwa nchi hiyo wiki iliyopita, mamia ya wakimbizi wameendelea kukimbilia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Miongoni mwao huenda wamo waasi, na jeshi la Kongo ambalo linahofia kusambaa kwa vita na kuingia nchini mwao, linakamata watu wote wanaoshukiwa kuwa wapiganaji. Wakimbizi hata hivyo wanasema kuwa vijana wasiokuwa ...

Read More »

Wabunge Walaani Kuchomwa kwa Nyumba ya Kabila

Wabunge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumatatu walilaani kitendo cha kuchomwa kwa nyumba ya rais Joseph Kabila. Katika taarifa ya pamoja, wabunge hao walikiita kitendo hicho kuwa cha kinyama na kutoa wito kwa raia kuotojihusisha na vitendo ambavyo vingechangia kuzorota kwa amani na maendeleo katika baadhi ya maeneo ya nchi. Mapema Jumatatu, washambuliaji walichoma nyumba ya rais katika shamba ...

Read More »

BALOZI WA VENEZUELA ATIMULIWA CANADA

Canada imetangaza kumfukuza balozi wa Venezuela Wilmer Barrientos Fernández Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Chrystia Freeland alisema hatua hiyo ni jibu kwa kufukuzwa kwa mwanadiplomasia wake wa cheo cha juu kutoka Venezuela mwishoni mwa wiki. Venezuela iliilaumu Canada kwa kuingilia masuala yake ya ndani. Cadana ilikuwa imeilaumu serikali ya Rais Nicholas Maduro kwa ukiuja wa haki za binadamu. ...

Read More »

AJALI: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Apata Ajali ya Gari

AJALI: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Juma Kilimba amepata ajali ya gari lake kupinduka leo akiwa na familia yake, mke wake na watoto wawili wamepewa rufaa. Yeye bado na watoto wawili bado wako hospital ya Wilaya Kiomboi ambapo mtoto mmoja hawezi kusafirishwa hali yake sio nzuri, tumuombee  

Read More »

Catalonia Yashinda Uchaguzi ya Kutaka Kujitoa na Uhispania

Vyama vinavyounga mkono jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania vimeshinda uchaguzi wa jimbo la Catalonia. Ikiwa kura zote zinakaribia kukamillika kuhesabiwa Katika rekodi ya wapiga idadi ya wapiga kura ambao wamejitokeza vyama hivyo vinaonekana kushinda jambo kimepunguza kidogo idadi ya viti bungeni. Matokeo hayo kwa vyovyote ni habari mbaya kwa waziri mkuu wa Hispania,Mariano Rajoy ambaye aliingilia kati jimbo hilo ...

Read More »

Rais wa Ujerumani Ahimiza Ujenzi Taasisi Imara

Rais wa Ujerumani, Frank- Walter Steinmeir, amehitimisha ziara yake katika bara la Afrika kwa kuhimiza masuala ya demokrasia na maendeleo ya kiuchumi.  Katika ziara yake hiyo, Rais Steinmeir  amehimiza uimarishwaji vita dhidi ya ufisadi  na  mapambano imara juu ya  uhamiaji unaoendelea kuwa tishio kwa maisha ya binadamu hasa katika kipindi hiki. “Mataifa yote yanapaswa kuungana ili kukabiliana na janga hili linaloendelea ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons