MCHANGANYIKO

Man. United ipo kazi mwaka huu

Tangu kuanza kwa Ligi Kuu England, Manchester United ilipata ushindi wa pili katika mchezo wake wa Jumamosi iliyiopita dhidi ya West Ham United.

Read More »

MK Group ilivyotesa miaka ya 1990

Bendi ya MK Group ilikuwa maarufu kwenye miaka 1990, iliyokuwa imejikita kupiga muziki  katika hoteli za kitalii hapa nchini. Lakini kabla ya kuanzishwa kwake, kulikuwa na bendi ya mama, ya  African Stars iliyoanzishwa Julai 1, 1994, katika Hoteli ya  Bahari Beach Dar es Salaam.

Read More »

Unyonge wa Mwafrika – 2

Juma lililopita nilizungumzia kwa ufupi unyonge wa Mwafrika, ambao Mwalimu Julius Nyerere amesema unyonge huo uko wa aina mbili.  Unyonge wa kwanza amesema ni unyonge wa MOYO, unyonge wa ROHO.  Unyonge wa pili ni unyonge wa UMASKINI.

Read More »

Yah: Tumalizeni, lakini kumbukeni wapigakura wenu

Sasa ni miaka kama kumi hivi tangu Serikali ilipotangaza ajira za vijana wapigakura na wenye uchu na maisha bora kama nafasi milioni moja, katika ajira hizo bila kufanya utafiti wa kina naweza nikasema robo tatu ya ajira hizo ni udereva wa pikipiki.

Read More »

Watanzania tuchimbe madini yetu wenyewe

Awali ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye kwa rehema zake nyingi anatuwezesha kuendelea kuwapo katika uso wa dunia hii.

Binafsi natambua kuwa nayaweza haya yote niyatendayo kila siku kwa sababu yupo mwenye uwezo kuliko wangu, na ndiye anitiaye nguvu na kuniwezesha ipasavyo kulingana na mapenzi yake.

Read More »

Tanzania ijitoe Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Katika toleo lililopita la gazeti hili, nilizungumzia hali halisi ya ujirani wa Tanzania na nchi nne nyingine zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania.

Nilisisitiza kwamba katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania haina majirani wazuri. Nilitoa mfano wa Kenya ambayo imekuwa ikihujumu Tanzania na kuifanyia mambo ya uhasama yanayodhoofisha umoja na ushirikiano  wa Afrika Mashariki.

Read More »

Kennedy Ndosi: Kina Ridhiwani wananivutia kuwania ubunge

 

Joto la Uchaguzi Mkuu mwakani, litakalohusisha ngazi ya urais, ubunge na udiwani, limepamba moto. Mmoja wa vijana, ambao wanaelekea moja kwa moja kuhitaji kulitumikia Taifa kisiasa ni Kennedy Elimeleck Ndosi, mtaalamu wa Ununuzi na Ugavi. Sifa kubwa ya Ndosi ni kutokukubali kushindwa kwa urahisi. Ni mpambanaji. Hii ni kwa sababu mtaalamu huyo wa ununuzi na ugavi ni mchapakazi. Ndosi ana ndoto za kuwa mbunge, na katika makala hii anajibu maswali katika mahojiano na mwandishi wa makala hii yaliyofanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam...

Read More »

Tibaijuka: Nawapigania wasichana

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameweka hadharani misaada na michango anayokusanya kwa ajili ya kuwakomboa watoto wa kike.

Read More »

Ninachokumbuka kuhusu mradi wa maji Ziwa Victoria

Katika dunia kuna mambo yakitokea unajiuliza kwa nini yametokea. Unajiuliza ni hivi hivi au kuna msukumo, ila yote kwa yote nimejiwekea utaratibu wa kusimamia ukweli. Mara zote naamini ukweli unamweka mwanadamu huru, na hapa leo kama nifanyavyo siku zote nitajaribu kueleza ukweli ninaoufahamu.

Read More »

Malengo ya kazi (2)

Lazima wahakikishe kwamba kazi zote zinaendeshwa barabara, na pamba ya aina itakiwayo inapatikana na wakati ule ule inapoatakiwa; wahakikishe kwamba hakuna kipingamizi  kutoka hatua moja hata nyingine; kwamba kuna uhusiano baina ya kazi mbalimbali, na kwa sababu hiyo hakuna mfanyakazi anayekaa bure kungojea mwenzake amalize kazi yake.

Wakubwa wa kazi hawana budi kuhakikisha kwamba wananunua pamba ya kutosha, na kwamba wana mahali pa kuuzia nguo  zinazotengezwa; kwamba mishahara inalipwa bila ya kuchelewa;  kwamba hesabu ya fedha zinazowekwa sawa sawa; kwamba mitambo inakaguliwa ipasavyo; na mambo mengine kadha.

Read More »

Tugeukie mabadiliko ya Katiba, maandamano tuwe macho

 

Kumbukumbu zinanionesha sasa kuwa Watanzania wengi wanaamini kuwa suala la Katiba Mpya haliwezekani tena chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Ametafuta pa kutokea na kuamua kuelewana na wapinzani kupitia Kituo cha Demokrasia (TCD) na wakubwa hawa wakakubaliana yafanyike mabadiliko ya 15 ya Katiba.

Read More »

‘Utatu wa Maliasili’ ni wa ulaji

Watanzania tuna ugonjwa mmoja mbaya sana. Ugonjwa wa kutokuhoji lolote. Hatuna utamaduni wa kuhoji vitendo na kauli tata za viongozi na watawala wetu. Tumeridhika kuwa liwe liwalo; au yote maisha.

Kutokana na hali hiyo hatuna na hatuoni sababu za kuwawajibisha viongozi waongo, wazushi, matapeli na mafisadi. Matokeo yake viongozi na watawala hawa wamekuwa wakitumia udhaifu wetu wa kutokuhoji kufanya watakavyo.

Read More »

Tanzania ijitoe Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Bila shaka sisi sote tunajua kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Umoja wa Nchi za Afrika Mashariki unaojumuisha nchi tano za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania.

Watu husema ‘umoja ni nguvu’ kwa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni umoja, basi watu wanalazimika kumshangaa mtu anayewahimiza wenzake wajitoe kwenye umoja. Ni kweli umoja ni nguvu. Lakini inategemea unafanya umoja na mtu wa aina gani. Hii ni kusema kwamba wakati mwingine umoja ni udhaifu na unaweza kumletea mtu madhara makubwa.

Read More »

Unyonge wa Mwafrika – 1

Naikumbuka vyema Jumamosi ya Mei 30,1969 nilipohudhuria Sherehe za Vijana wa Tanzania zilizofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga, Dar es Salaam na kuhutubiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Read More »

Yah: Ugwadu na utamu wa tunda aujuae mlaji?

Nimesikiliza hotuba nyingi  na za viongozi wengi walionona sura zao kwa maisha ya hali bora, wakijaribu kutuzungumzia walaji wa matunda ya umaskini na jinsi  tunavyoteseka. Wote nawakubali lakini ni vema nikatoa tahadhari kuwa hayo maisha magumu wanayotuzungumzia wamehadithiwa hawayajui kabisa.

Read More »

Yanga iwe makini ili isimpoteze Jaja

Na Robert Mwandumbya

 

Genilson Santos Santana 'Jaja', ambaye kwa sasa ametawala vichwa vya vyombo vya habari, ameifungia Yanga mabao manne katika mechi tano alizocheza. Lakini taarifa nyingine zinasema kwamba katika mazoezi yaliyopigwa Uwanja wa Bandari, Loyola na kule Zanzibar, nyota huyo amefunga mabao zaidi ya 40.  

Read More »

Wenye akili wapo Ikulu!

Rais Jakaya Kikwete alipoamua kuleta suala la Katiba mpya kupitia ilani yake ‘mbadala’, wapo waliomshangaa.

Nakumbuka niliandika makala iliyosema, “Nitakuwa wa mwisho kuishabikia Katiba mpya”. Hiyo haikuwa na maana kwamba sikutambua wala kuthamini matamanio ya Rais wetu kuwaachia Watanzania Katiba nzuri!

Read More »

KWA HILI LA OKWI Yanga inahadaa mashabiki wake

Edgar Aggaba, mwanasheria wa Emmanuel Okwi, nyota wa soka wa kimataifa kutoka Uganda, hakufika Dar es Salaam kusimamia kesi ya mchezaji huyo wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilipojadili mkataba na usajili wake katika klabu ya Yanga.

Read More »

Lovy Longomba Gwiji aliyetokea katika familia ya wanamuziki

“Mtoto wa nyoka ni nyoka.” Usemi huu wa wahenga unajionesha wazi kwa baadhi ya familia zilizojaaliwa kuwa na vipaji vikubwa.

Vipaji hivyo vinaweza kuwa vya kucheza mpira, muziki, kucheza sarakasi, riadha, ndondi n.k.

Read More »

Warioba, Spika Sitta wateketeza Sh 100bil

MPAKA Jumamosi ya Oktoba 4, mwaka huu, Bunge Maalumu la Katiba Mpya litakuwa limetumia zaidi ya Sh 100 bilioni bila kupatikana kilichotarajiwa.
Fedha hizo, ni hesabu kuanzia Mei mosi, 2012 siku ambayo Tume ya Marekebisho ya Katiba ambayo ilikuwa na kazi ya kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya ilipoanza kazi rasmi.

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons