MCHANGANYIKO

Mchakato wa Katiba haukuandaliwa vizuri

Kama tujuavyo Bunge la Mabadiliko ya Katiba limekumbwa na vurugu na misukosuko kiasi cha kutia aibu Taifa letu.

Nashindwa kusema Bunge hilo liliendelea kujadili Rasimu ya Katiba kwa ukaidi wa nani. Maana wakati wote magenge mbalimbali  ya watu waliendelea kudai Bunge hilo lisitishe shughuli zake, hasa baada ya wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia Bunge hilo.

Read More »

ongezi JWTZ kwa kutimiza miaka 50   -2

Juma lililopita, nilitoa pongezi kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa Septemba Mosi, 1964.  Ukweli Jeshi hili liliasisiwa baada ya Jeshi la Tanganyika (Tanganyika Rifles-TR)  kuasi Januari  20,1964.

Read More »

Pongezi ‘JAMHURI’, Maimuna Tarishi mapambano ya mauaji ya tembo

Tunaomba kukupongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, na baadhi ya wadau kwa kufungua baadhi ya fahamu za Watanzania wazalendo na wanyonge, na huo ndiyo uongozi bora kwa  viongozi wapenda maendeleo ya nchi yao.

Read More »

Mheshimiwa Sitta acha kututania!

Wiki iliyopita zilichapishwa habari nyingi, ila nimejikuta na shindwa kujizuia nashawishika kuandika jambo juu ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mheshimiwa sana, Samuel Sitta, ‘Mzee wa Kasi na Viwango.’ Mheshimiwa huyu ametoa kauli kuwa Bunge Maalum la Katiba lazima liendelee na kura zipigwe.

Read More »

Nyalandu aanza kulipa ndege aliyofadhiliwa

Mara baada ya Balozi Khamis Kagasheki kujiuzulu kutokana na shinikizo la wabunge kadhaa, baada ya taarifa ya James Lembeli juu ya Operesheni Tokomeza kuwasilishwa bungeni Novemba, mwaka jana; Lazaro Nyalandu, wakati huo akiwa ni Naibu Waziri katika Wizara ya Maliasili na Utalii, alisafiri sana huku na kule nchini.

Read More »

‘Hatuchukui tena makapi ya CCM’

Niliposoma maneno hayo katika Gazeti la Mwananchi toleo Na. 5098, Jumanne, Julai 8, 2014, ukurasa wa mbele (na maelezo uk. 4: Siasa) nilipigwa na butwaa!  
Lakini nilitaka nijiridhishe na kile nilichokisoma kwa kuwapigia simu wahusika -- Gazeti la Mwananchi. "Haya mliyoandika mna hakika yametamkwa na Dk. Wilbrod Slaa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)?"

Read More »

Operesheni saka wachawi yatikisa Geita

Vikongwe waauwa

Operesheni haramu ya mauaji ya kinyama dhidi ya wanawake vikongwe, inayofanywa na kikundi cha Chinja Chinja isipodhibitiwa mkoani wa Geita, kuna hatari ya hazina hiyo muhimu kwenye Taifa kumalizika kwa kuuawa bila hatia.

Read More »

Mwanamke aliyenusurika kifo kisa dini

Meriam Yahia Ibrahim Ishag au Maryam Yahya Ibrahim Ishaq ni raia wa Sudani kwa anayeishi nchini Marekani katika Jimbo la Philadelphia kwa sasa, kutokana na kukimbia nchini kwake baada ya kupona hukumu ya kifo kwa madai ya kuasi dini yake.

Read More »

Ijue historia ya Kombe la Dunia

Katika kipindi hiki cha kuelekea fainali za soka za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil kuanzia Juni 12, mwaka huu, JAMHURI imeona vema kuwakumbusha mashabiki, wapenzi na wadau wa soka kwa jumla, historia ya mashindano hayo.

Read More »

MANU DIBANGO: Gwiji la saxophone lililotimiza miaka 80

Manu Dibango ni gwiji wa kupuliza chombo adhimu katika ulimwengu wa muziki, kilichobatizwa kwa jina la 'midomo ya bata' (saxophone) na watu wa 'mujini', aliyejizolea sifa kemkem barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

Nguli huyo Februari 10, 2014 alitimiza miaka 80 ya kuzalikwa kwake.

Jina lake halisi ni Emmanuel Dibango, ambaye, pamoja na kupuliza saxophone, pia ni mtunzi na mwimbaji mahiri mwenye sauti nzito. 

Read More »

Biashara ni wateja, tuwajali

Siku moja nilikuwa mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo katika mkoa wa Iringa. Nikiwa hapo niliingia kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi nikiwa na lengo la kununua vifaa kadhaa vyenye thamani ya takriban shilingi laki tatu.

Katika duka hilo nilimkuta mama mmoja ambaye wakati akinipokea alionekana kuwa bize kubonyeza simu yake ya kiganjani. Nilipomsalimia hakujibu, na baada ya kuinuka kutoka katika kuitazama simu yake akaniuliza, “Nikusaidie nini?” Mimi nikamjibu kwa kumueleza vifaa ninavyovihitaji na kumuomba anitajie bei zake kimoja kimoja.

Read More »

GERALD NYAISSA: Kijana msomi anayependa kujiajiri

 

*Hutumia makaburi kumwomba Mungu

Wiki iliyopita JAMHURI ilifanya mahojiano maalum na kijana msomi aliyehitimu elimu ya chuo kikuu katika fani ya utawala wa biashara. Huyu si mwingine yeyote bali ni Gerald Nyaissa, mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Mahojiano haya yalijikita zaidi katika suala zima la kuchangamkia fursa za kujiajiri na kujijenga kiuchumi, badala ya kusubiri kuajiriwa serikalini na kupata misaada kutoka kwa wahisani. Yafuatayo ndiyo mahojiano yenyewe:

Read More »

Rais azibe pengo la wana UKAWA

Kuna haja ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, kuangalia uwezekano wa kuziba pengo lililoachwa wazi na wanachama wa unaoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika Bunge Maalum la Katiba.

Read More »

Tumeshindwa kulinda heshima ya Tanzania

Kama tunavyokumbuka Februari 5, 1977, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilizinduliwa Zanzibar. Siku hiyo Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM, Mwalimu Julius Nyerere, alitaja kazi mbili za chama hicho.

Mwalimu Nyerere alisema kwamba kazi ya kwanza ya CCM ni kujenga Ujamaa Tanzania. Kazi yake ya pili ni kulinda heshima ya Tanzania. Kadiri siku zinavyokwenda, inaonesha kwamba CCM imeshindwa kufanya kazi zote mbili.

Read More »

Yah: Kizazi hiki baada ya miongo mitano 

Nadhani kuna wakati kufikiria ndoto za Alinacha kwa maana za mchana kweupe, ni sawasawa na uendawazimu, lakini ndoto hizo hizo kuwaza kwa nia njema kunasaidia kuchukua hadhari kwa siku zijazo. 
Leo nimeamka na ndoto ambayo kwa kila atakayeguswa na wazo langu, ajaribu kufanya kama anaota ili aone jinsi ndoto yangu inavyoweza kuwa na ukweli ndani yake na avute taswira halisi ya wakati huo na athari ambayo inaweza kuwa imejitokeza. 

Read More »

Bandari yaishitaki JAMHURI, Mhariri

*Kipande adai fidia Sh bilioni 5.85, aomba lizuiwe kuiandika Bandari

*Mahakama yasitisha kumfukuza Mkurugenzi, Njowoka kushitakiwa

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mzee Madeni Kipande (58) na mtu aliyejiita Katibu wa Shirika la TPA, Christian Chiduga, kwa pamoja wamelifungulia kesi Gazeti Jamhuri mahakamani na Mhariri Mtendaji, Deodatus Balile, wakidai fidia ya Sh bilioni 5.85.

Pia wawili hao walifungua kesi nyingine Mahakama Kuu chini ya Hati ya Dharura mbele ya Jaji Sheikh iliyotarajiwa kuitishwa Jumatatu jana, wakiomba Mahakama itoe amri ya zuio kwa JAMHURI isiendelee kuandika habari zinazohusu Bandari.

Read More »

Lembeli: Mbunge mahiri au muuza nchi?

Vyombo kadhaa vya habari vimeandika taarifa za Mjumbe wa Bodi ya African Parks Network (APN), James Lembeli, kuwashitaki wanahabari na wahariri wa vyombo kadhaa vya habari.

Kwenye orodha hiyo, jina la Manyerere Jackton limo. Pamoja nami, kuna makomredi wengine walioamua kwa haki kabisa kusimama kidete kulinda rasilimali za nchi yetu. Wito wangu kwa wote -- tusikate tamaa.

Hadi naandika makala haya, sijapokea barua yoyote kutoka, ama kwa Lembeli au katika Mahakama ikinieleza bayana suala hilo. Kwa sababu hiyo, bado taarifa hizi nazichukulia kama taarifa nyingine zisizo rasmi, ingawa lisemwalo lipo, na kama halipo, laja.

Read More »

Ujumbe wa Pluijm uzingatiwe

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Hans Van Der Pluijm, ametema nasaha nzito kwa timu hiyo, ambazo zinastahili kuzingatiwa pia na klabu nyingine za soka hapa Tanzania. Akizungumza katika hafla ya kumuaga iliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki iliyopita baada ya kuifundisha Yanga kwa kipindi cha miezi minne, Pluijm aliwaasa viongozi wa ...

Read More »

Mameneja Tanesco wanolewa kuhusu Mazingira

Kutokana na upungufu wa umeme unaoikabili nchi yetu ya Tanzania, tunategemea kuwa uwekezaji katika sekta ya nishati utaongezeka, hivyo kuibua changamoto nyingi za kimazingira, kiuchumi na kijamii.

Haya yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira Wizara ya Nishati na Madini, Gedion Kasege, hivi karibuni wakati akifungua semina ya siku tano iliyowahusisha mameneja wa Tanesco nchini ili kujifunza masuala ya uhifadhi wa mazingira  (Strategic Environmental Impact Assesment), utwaaji wa ardhi, Sheria ya Mazingira na masuala ya jinsia katika sekta na jinsi ya kukabiliana nayo kuweza kufikia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Read More »

Tukatae ukatili dhidi ya albino (2)

Juma lililopita nilizungumzia chimbuko na dhana potofu zinazoendelea miongoni mwa jamii yetu kuhusu watu wenye ualbino.  Leo naangalia masuala ya utu, afya, haki, matatizo na usalama wao.

“Watu wenye ualbino” kama wanavyotaka wao wenyewe kuitwa, na wasiitwe albino au zeruzeru kwa sababu majina hayo yanadhalilisha utu wao. Binafsi sioni kama kuna udhalilishaji juu yao.

Maneno hayo mawili ya Kiswahili na Kiingereza yote yanatoa maana ile ile moja ya kukosa rangi kamili ya mwili. Ni vyema ndugu zangu wayakubali majina hayo. Nasema ninawaomba wayakubali majina hayo.

Read More »

Ugaidi Kenya utuimarishe kiulinzi

 

Wimbi la matukio yanayohusishwa na ugaidi limeendelea kuitesa nchi ya Kenya kwa kuua na kujeruhi watu, kuharibu mali mbalimbali na kuisababishia hasara kubwa.

Wiki iliyopita watu zaidi ya 10 waliripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa wakati wa milipuko miwili iliyotokea katika soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi.

Huo ni mfululizo wa matukio kadhaa yanayohusishwa moja kwa moja na ugaidi likiwamo lililoshambulia kituo cha maduka ya kifahari cha Westgate jijini Nairobi.

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons