page za ndani

Maisha ya Maria na Consolata

Baada ya kuwapo sintofahamu juu ya nini hasa kilichowua watoto mapacha Maria na Consolata, Gazeti la Uchunguzi la JAMHURI limeamua kutafuta ukweli wa chimbuko la kifo cha mapacha hawa, ambao hatimaye sasa umefahamika. Mapacha hao Maria na Consolata, walifariki dunia Jumamosi, Juni 2, 2018, saa 02:00 usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kuugua kitambo. Uchunguzi ...

Read More »

Felix Wazekwa alitumia ndumba kuvuta mashabiki wa muziki

MOSHY KIYUNGI Félix Wazekwa ni mwanamuziki mwenye mbwembwe wakati akiwa jukwaani, akiimba huku akiongoza safu ya wanenguaji. Mtindo wa unenguaji wanaoutumia ni wa aina yake, ambao haulingani na mitindo mingine yoyote ya wanamuziki wa huko Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC). Majina yake kamili anaitwa Feleix Nlandu Wazekwa S’Grave. Alizaliwa Septemba 1, 1962 katika jiji la Kinshasa, (DRC). Alianza kujiingiza ...

Read More »

Viatu havibani, havipwayi vinatosha Na Angalieni Mpendu “Kweli nimeomba nipumzike kwa sabab

Na Angalieni Mpendu “Kweli nimeomba nipumzike kwa sababu, nimekitumikia chama changu muda mrefu, nimeona niachie damu mpya. Nimependa nipumzike, lakini hayo mengine yanayoandikwa ni ya kupuuza.” Ni kauli thabiti iliyojaa hiari na uungwana; na iliyoshiba haki usawa na ahadi kutoka moyoni mwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (2012- 2018), Abdulrahman Kinana, alipozungumza na gazeti JAMHURI, wiki iliyopita. Kupenda ...

Read More »

NYERERE 349

Sehemu ya 7 Kama shule iko kijijini (na katika shule mpya zitakazojengwa siku zijazo) itawezekana kwamba shamba la shule liwe karibu karibu na shuleyenyewe. Lakini katika miji na katika shule za zamani zilizo katika vijiji vyetu vyenye watu wengi, huendaisiwezekane kuwa hivyo. Katika hali hiyo shule inaweza kutilia mkazo kazi zingine zenye kuleta uchumi, au inawezekana katika shule za mabweni ...

Read More »

Ndugu Rais nguzo imeanguka paa litashikiliwa na nani?

Ndugu Rais, Abdulrahman Kinana ametuacha! Anataka kupumzika. Mwanadamu ana siku moja tu ya kupumzika. Siku Muumba wako atakayokwita ukasimame mbele ya haki! Siku hiyo utakuwa umelala peke yako! Nawe utakuwa na mapumziko ya milele kwenye nyumba yako ya milele! Hapa duniani pambana na hali yako, Abdulrahman, mahali pa kupumzika hakuna! Ukatibu Mkuu hukuuachia kwa nguvu zako mwenyewe. Tuaminio tunaamini kuwa ...

Read More »

Mafanikio yoyote yana sababu (24)

Padre Dk Faustin Kamugisha Kuwajali wateja ni sababu ya mafanikio. Mteja ni kama damu muhimu kwa uhai wa biashara yako au shughuli yako. Kanuni ya msingi kwa yeyote anayehudumia mteja ni mteja kwanza. Mteja ni mfalme. Inaweza kukuchukua miezi kumpata mteja na sekunde moja kumpoteza. Usipowajali wateja wako, mtu mwingine atawajali. Yatafakari maneno ya Mahatma Gandhi: “Mteja ni mgeni muhimu ...

Read More »

Mapya yabainika St. Florence

*Imejengwa na kuziba barabara ya mtaa *Mmiliki, wanafunzi waishi eneo moja   NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM   Shule ya St. Florence Academy iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, ambayo mwalimu wake anatuhumiwa kuwadhalilisha kingono wanafunzi wa kike wanne, inadaiwa imejengwa kwenye barabara na hivyo kufunga mtaa. Mwalimu huyo ambaye vyombo vya dola vinamsaka, anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati ...

Read More »

Bandari ni salama njoo tukuhudumie

Na Mwandishi Maalum Makala ya mwisho katika mfufulizo wa makala za Bandari tuliona jinsi Bandari ya Mwanza ilivyo kiungo muhimu kwa uchumi na biashara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, nchi za Afrika Mashariki na maeneo mengine. Leo katika makala hii tutaona umuhimu wa kufanya biashara katika bandari zenye usalama na mazingira rafiki na yanayovutia wateja. Katika utekelezaji wa shughuli ...

Read More »

Balozi: Tanzania inapoteza mabilioni

Na Angela Kiwia Balozi John Chagama amesema Tanzania inapoteza mabilioni ya shilingi kutokana na viongozi wachache wenye uchu wa utajiri kuatamia fursa ya soko la mtandaoni. Mwaka 2012, Balozi Chagama na wenzake, walianzisha Kampuni ya Tanzania Commodity Exchange (TCX) iliyopaswa kufanya kazi ya ya biashara kupitia soko la mtandaoni, lakini kampuni hiyo inahujumiwa. “Mwaka 2012 tulianzisha TCX, Rais pamoja na ...

Read More »

Somo la Mazingira ni Gumu Sana

Ningekuwa mbunifu mahiri wa kuandika hadithi, ningeandika hadithi ya vyura wa Kihansi kushangaa ni kwa kiasi gani binadamu wajinga mpaka kuwasafirisha vyura wenzao kwenda kuishi Marekani kwa muda. Mradi wa kuzalisha umeme wa Kihansi ulipoanza, mwaka 2000, ulipunguza kiwango cha maji yaliyokuwa yakitiririka kwenye eneo walipokuwa wanapatikana vyura ambao uhai wao ulitegemea sana mvuke wa maji yaliyotokana na maporomoko ya ...

Read More »

Afrika iligomea kombe la dunia Moscow, Urusi

Safari ya Afrika katika kushiriki michuano ya kombe la dunia imekuwa ya milima na mabonde, lakini sasa Afrika inaelekea kuvunja ilichopanda kwa dalili zilizopo. Mwaka 1966 katika fainali za kombe la dunia zilizofanyikia nchini Uingereza na wenyeji kuwa mabingwa, Bara la Afrika halikuwa na mwakilishi katika michuano hiyo kutokana na upendeleo wa wazi kwa nchi za Ulaya na Marekani kupewa ...

Read More »

Afrika kupeta Urusi Moscow, Urusi

Kombe la dunia linaanza siku tisa zijazo kuanzia leo. Afrika inawakilishwa 5 katika mashindano hayo yanayochezwa nchini Urusi na wachambuzi wanasema Afrika inayo nafasi zamu hii. Leo tunakuletea makundi ya timu hizi na wiki ijayo tutakuletea ratiba yote ya michuano ya kombe la dunia 2018 kwa ajili ya kumbukumbu yako. Kundi A Kundi hili lina mwenyeji wa mashindano nchi ya ...

Read More »

Sudan Kusini kuwekewa vikwazo

JUBA Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezipa muda wa mwezi mmoja pande hasimu zinazogombana nchini Sudan Kusini kufikia makubaliano vinginevyo nchi hiyo ijiandae kukabiliana na vikwazo. Mchakato huo uliongozwa na Marekani ndani ya Umoja huo ulipata ushindi mdogo wa kura 9 katika baraza hilo lenye nchi wanachama 15 na huku kukionekana na kuwepo kwa hali ya ubishani miongoni ...

Read More »

Bomu la watu laja Afrika – mwisho

Balile

Na Deodatus Balile Mwezi uliopita nimefanya mapitio ya kitabu kiitwacho “Making Africa Work”. Tafsiri isiyo rasmi ya jina la kitabu hiki ni “Mbinu za Afrika kujikwamua kiuchumi.” Kimeandikwa na Greg Mills, Olusegun Obasanjo (Rais mstaafu wa Nigeria), Jeffrey Herbst na Dickie Davis. Kimechapishwa na Taasisi ya Brenthurst Foundation ya Johannesburg, Afrika Kusini. Rais (mstaafu) Benjamin Mkapa ameshiriki uzinduzi wa kitabu ...

Read More »

Waziri Mkuu Matatani

UKWAPUAJI MALI ZA CCM   Waziri Mkuu yumo *Anunua shule ya Chama, abanwa, airejesha chapuchapu *Yeye, Dk. Bashiru Ali wakwepa waandishi wa JAMHURI *Wajumbe NEC wataka achunguzwe mali anazomiliki *Wamlinganisha Rais Magufuli na Nyerere kwa uadilifu     NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM   Kamati ya Kufuatilia Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), imegundua madudu ya kutisha katika jumuiya ...

Read More »

Uchochezi wa Oakland Institute na wenzake Loliondo

Hivi karibuni taasisi ya Oakland imetoa taarifa yenye kichwa cha habari: “Loosing the Serengeti: The Maasai land that was to run forever”, na kutangazwa na mashirika kadhaa ya habari ya kimataifa duniani kote. Serikari ya Tanzania imeshutumiwa kwa uongo kwamba inakandamiza haki za Wamaasai wanaoishi Wilaya ya Ngorongoro inayopakana na Hifadhi ya Taifa Serengeti. Taarifa hiyo inakwenda mbali zaidi na ...

Read More »

Tusimamie utawala wa sheria

Katika maendeleo ya nchi na jamii msingi wa utawala wa sheria ndio hasa huleta ulinganifu kwa aliyenacho na asiyenacho. Hivyo ni msingi huo pekee haki huonekana imetengendeka. Kumekuwepo na kilio hasa kutoka kwa wanyonge pindi wanapoona hawajatendewa haki na mamlaka husika. Kilio kikubwa  kimekuwa kikielekezwa kwa Jeshi la Polisi. wamekuwa wakituhumiwa na wananchi kuwapatia ulinzi baadhi ya watu wasio wema. ...

Read More »

Waziri Mpina ziba masikio

Mjadala uliohusu vita dhidi ya uvuvi haramu ulitawala sehemu kubwa ya bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, bungeni jijini Dodoma, wiki iliyopita. Pengine kabla ya kuendelea, ni vizuri tukafahamu kazi za mbunge. Mbunge ana kazi nyingi, lakini zilizo kuu kwa mujibu wa Katiba yetu ni kuwawakilisha wananchi, kutunga sheria, na kuisimamia Serikali. Lakini tunaweza kuzinyambua kazi hizo na kuona ...

Read More »

Uongozi siyo kazi ya rais peke yake

Juma lililopita Rais John Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam iliyoibua masuala kadhaa. Madhumuni ya ziara yalikuwa kuhakiki iwapo mafuta yaliyohifadhiwa kwenye matangi hapo bandarini yalikuwa ghafi au la, ili kubaini ushuru sahihi wa kulipia mafuta hayo. Zipo sababu nyingi kwanini rais analazimika kwenda bandarini kukagua shehena ya mafuta, lakini ni moja ambayo ndiyo ya ...

Read More »

Ndugu Rais tumwache Akwilina apumzike kwa amani

Ndugu Rais, umebarikiwa wewe kwa sababu unatambua uwepo wa ukweli. Wakati wengine wakisema ukweli unauma, wewe umeihubiri kweli bila kuchoka. Mwenyezi Mungu akuimarishe ili uiishi hiyo kweli. Kweli ni dhahiri yaani bila uongo. Yako mengi yaliyosemwa juu ya kweli. Kamusi kuu ya Kiswahili imeandika, “Ni vizuri kusema ukweli hata kama utasababisha madhara kuliko kusema uongo”. Wacha Mungu wanasema, “msemakweli mpenzi ...

Read More »

Bandari ya Mwanza kiunganishi Maziwa Makuu

Na Mwandishi Maalum   Baada ya kuona jinsi Bandari ya Kyela inavyoing’arisha kiuchumi na kijamii Kanda ya Juu Kusini na nchi jirani za Malawi, Msumbiji na Zambia wiki iliyopita, katika makala haya tutaona jinsi Bandari ya Mwanza ilivyo kiungo muhimu cha uchumi na biashara kati ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, nchi za Afrika Mashariki na maeneo mengine. Bandari zilizo ...

Read More »

Jaji Warioba matatani

*Mtendaji TBA aagiza afukuzwe alikopanga *Yono wakabidhiwa kazi ya kumwondoa *Amri ya Mahakama inayomlinda yapuuzwa *Yeye asema hadaiwi, polisi wasita kumwondoa       NA MANYERERE JACKTON   Waziri Mkuu na Makamu wa Rais (mstaafu), Jaji Joseph Warioba, anafukuzwa kwenye nyumba alimopanga, mali ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), JAMHURI limethibitishiwa.   Jaji Warioba ambaye pia amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons