page za ndani

AFYA: Usizidharau dalili hizi

Hizi ni dalili mbalimbali zinazojitokeza kwenye miili yetu. Japo zinaweza zisiashirie tatizo, lakini kama ikitokea zinajirudia mara kwa mara ni vyema kupata vipimo na ushauri wa kiafya. Dalili ya kwanza ni udhaifu wa kwenye miguu na mikono kunakoambatana na ganzi. Ikiwa sehemu za mikono na miguu zinadhoofika, zinakosa nguvu na kupata ganzi na hasa dalili hizi zikitokea hadi usoni, inaweza ...

Read More »

Demokrasia iliyotundikwa msalabani

  Mwaka 2015 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa taifa letu la Tanzania, niliandika makala nyingi katika gazeti hili la JAMHURI. Makala zangu zilikuwa zinakosoa mwenendo wa chama tawala (CCM). Sihitaji kusimulia kilichonitokea lakini inatosha kudokeza kiduchu: ‘Niliambulia vitisho vya kuondolewa uhai wangu.’ Nilijiuliza maswali mengi sana. Je, ni kweli kwamba kuikosoa Serikali ni dhambi? Na kuisifia ni utukufu? Je, ni kweli ...

Read More »

Ndugu Rais dunia hadaa ulimwengu shujaa

Ndugu Rais, dunia tuliikuta na dunia tutaiacha. Niliwahi kusema kuwa kila mtu kila msiba anaohudhuria humkumbusha misiba yake iliyopita. Kama umefiwa na baba, mama, mtoto au ndugu aliyekugusa wakati wa msiba unakumbuka zaidi! Msiba umetokea na baba nilikuona. Msiba huu ulinikumbusha siku tulipokuwa tunauaga mwili wa Sir George Kahama katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Baba sikukuona ...

Read More »

Vyeti ‘feki’ vyaendelea kuitesa ORCI

NA CLEMENT MAGEMBE DAR ES SALAAM Sakata la kuwaondoa kazini watumishi waliokuwa na vyeti `feki’ linadaiwa kuitesa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) jijini Dar es Salaam, kwa wafanyakazi waliobaki kuzidiwa na utoaji huduma kwa wahitaji hususani wagonjwa. Taarifa zimedai kuwa kitengo kilicholemewa zaidi ni watumishi wa chumba cha maiti (mochwari) ambao wako wawili, baada ya wenzao watatu kuondolewa ...

Read More »

NEC itekeleze agizo la Waziri Mkuu

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutenda haki katika kutangaza washindi wakati wa uchaguzi.   Majaliwa ameyasema hayo Alhamisi iliyopita mjini Dodoma, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Devotha Minja, wakati wa kipindi cha ‘maswali kwa Waziri Mkuu.’ Minja akatoa mfano kuwa uchaguzi mdogo uliofanyika katika kata 43 Novemba ...

Read More »

TLS: Wampa kauli ngumu Rais Magufuli

Makala hii ni sehemu iliyokuwa imebaki wiki iliyopita katika risala iliyohaririwa ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Godwin Ngwilimi,  katika maadhimisho ya siku ya Sheria nchini, Endelea………………. Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia na kuboresha kiwango cha mienendo ya elimu ya sheria kwa Tasnia ya sheria nchini; kusaidia upatikanaji wa elimu ya sheria kwa wanachama wa jumuia ...

Read More »

Lala Salama ya Ubunge kwa Chadema, CCM

Na Waandishi Wetu Vyama vyenye ushindani mkubwa wa kisiasa nchini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vinaingia wiki ya mwisho kwa kampeni za uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam  na Siha mkoani Kilimanjaro. CCM imewasimamisha Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni) wakati wagombea wa Chadema wakiwa ni Elvis Mosi ...

Read More »

MAULI MTULIA: Kinondoni Nichaguei, Shughuli Yangu ni Ubunge

NA ANGELA KIWIA LICHA ya kuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kwa takribani miaka miwili, Maulid Mtulia hakuwa maarufu sana katika siasa za Tanzania, hadi Novemba 2, mwaka huu alipojiondoa katika chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hatua hiyo ililifanya jina la Mtulia likaanza kutajwa kwa kiwango kikubwa nchini, kama ilivyo sasa anavyoendelea kutajwa wakati ...

Read More »

Wabunge Wanapotangaza Hali ya Hatari

NA ANGELA KIWIA Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametangaza hali ya hatari nchini. Wametangaza ya kuwa maisha ya Watanzania si salama tena, tunaishi maisha yasiyo na uhakika wa kuiona kesho kutokana na vitendo vya uhalifu kushamiri nchini. Wakichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika Mkutano uliomalizika, wamebainisha kuwa hali ...

Read More »

Korea Kaskazini Yaonyesha Nguvu za Kijeshi

Siku moja kabla ya kufunguliwa kwa michezo ya Olympiki ya Majira ya Baridi nchini Korea Kusini, Korea Kaskazini imefanya gwaride kubwa la kijeshi kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa jeshi la nchi hiyo. Afisa wa Korea Kusini ambaye hakutaka kutajwa jina, amesema kiasi ya wanajeshi zaidi ya 13,000 walishiriki katika gwaride hilo lililokuwa na lengo la kuonesha nguvu ya kijeshi ...

Read More »

Mafanikio Yoyote Yana Sababu (9)

Na Padre Dk Faustin Kamugisha   Nia ni sababu ya mafanikio. Penye nia pana njia. Mtazamo wa “lazima nifanye kitu,” unatatua matatizo mengi kuliko mtazamo wa “kitu fulani lazima kifanyike.” Mtazamo wa kwanza una nguvu ya nia. “Nia yetu inaumba uhalisia wetu,” aliandika Wayner Dyer katika kitabu chake The Power of Intention. Yote ambayo umeyafanya kuna wakati uliyanuia. Mambo mengi ...

Read More »

Tusome Ishara za Nyakati Sehemu 2

Wiki iliyopita, makala hii ilianza kuchambua kwa kina baadhi ya mambo yanayotokea katika Tanzania na kuwataka Watanzania kusoma alama za nyakati. Leo, mwandishi anaendelea kuchambua kinachotokea na mwelekeo wa taifa la Tanzania. Endelea… Mungu hawawezi kuja mwenyewe kufanya unabii, la hasha, bali anawatumia wanadamu tena wadhaifu hasa viongozi wa dini.  Tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa dini waliojitoa mhanga kuufanya unabii ...

Read More »

Benedict Rasha Ndiye Aliyegundua Kuungua kwa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka

Na Albano Midelo Benedict Mapunda (Rasha) mwenye umri wa miaka 66 mkazi wa kijiji cha Ntunduwaro ndiye aliyegundua kuungua moto kwa mgodi wa madini ya makaa ya mawe Ngaka uliopo Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma mwaka 2006. Inakadiriwa moto huo uliowaka kwenye mgodi huo mwaka 2006 uliteketeza tani milioni sita za makaa ya mawe ndizo.Inaaminika Moto huo ulianza kuwaka ...

Read More »

Matumizi ya Gypsum Kwenye Ujenzi Yanazua Hofu

Mwaka 2011 nililala kwenye hoteli ya mjini Moshi, chumba kilirembwa na dari iliyonakshiwa kwa jasi inayojulikana zaidi kama gypsum. Ilikuwa ni jasi iliyokaa muda mrefu na ilikuwa inapukutika kwa urahisi. Siku iliyofuata niliiugua, nikapatwa na homa kidogo na mafua, ingawa hali hiyo mbaya haikuendelea kwa siku nyingi. Niliamini kwa uhakika kabisa wakati huo kuwa ni kuvuta kwa hewa iliyoathiriwa na ...

Read More »

Prof. Kairuki Anaishi Baada ya Kifo

Na Mwandishi Wetu   Februari 6, mwaka 2018 ilitimia miaka 19 tangu Prof. Hubert Kairuki alipofariki dunia. Katika kipindi kama hicho, wapo maprofesa wengi waliofariki hapa nchini na nje ya nchi siku hiyo. Ni kwa bahati mbaya kuwa siku walipofariki maprofesa hawa, hata majina yao yakafa. Hili halikutokea kwa Prof. Kairuki. Prof. Kairuki bado anaishi hadi leo. Jina la Prof. ...

Read More »

Pingu Yaibua `Zengwe’ kwa Mtuhumiwa wa Mauaji Moshi

Na Charles Ndagulla,Moshi Hatua ya kutofungwa pingu kwa mmoja wa Wakurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica, Edward Shayo (63), anayetuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Humphrey Makundi imezua utata na kuhojiwa na baadhi ya mahabusu wa gereza la Karanga mjini Moshi. Shayo alikuwa miongoni mwa watuhumiwa 11 waliokamatwa kufuatia mauaji ya mwanafunzi huyo aliyetoweka shuleni hapo ...

Read More »

Tanesco-Mbezi `Wanamtafuta’ Makonda

Serikali ya Rais John Magufuli imejidhihirisha kwa umma, kwamba azma yake ni kuhakikisha wananchi wanyonge wanapata huduma wanazozistahili bila ukiritimba. Kutokana na dhana hiyo, Mpita Njia anaamini kuwa raia hawapaswi kuombwa rushwa, ‘kuzungushwa’, kunyanyaswa ama kufanyiwa kitendo chochote kinachokiuka haki zao za msingi. Kwa muda mrefu sasa wananchi hasa wa hali ya chini, wamenyanyasika kutokana na watumishi wa umma wasiokuwa ...

Read More »

CCM, CHADEMA Jiandaeni Kisaokolojia

Wiki hii unafanyika uchaguzi mdogo katika majimbo ya Kinondoni, Dar es Salaam na Siha, Kilimanjaro. Uchaguzi huu umeitishwa kutokana na waliokuwa wabunge Godwin Mollel (CHADEMA) na Maulid Mtulia (CUF) kuhama vyama vyao wakajiunga na CCM baada ya kuvutiwa na utendaji wa Rais John Magufuli. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewateua Mollel kuwa mgombea wake Siha na Mtulia kuwa mgombea wake Kinondoni. ...

Read More »

Mauricio asema Kane ni ‘jembe’ la Spurs

Ushindi wa goli moja la Tottenham dhidi ya Arsenal wiki iliyopita, linamshawishi Meneja wa timu hiyo, Mauricio Pochettino kumtaja mfungaji wake, Harry Kane kuwa ni ‘jembe’ la sasa na baadaye kwa timu hiyo. Akitumia urefu wake, Kane aliiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa 1-0  kwenye uwanja wa Wembley dhidi ya washindani wao wa soka kaskazini mwa jijini Londoni nchini ...

Read More »

KUNA MAMBO PAUL MAKONDA ANAPATIA

Naungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Komredi Kingunge Ngombale-Mwiru, kutokana na kifo cha mwamba huo wa siasa katika Taifa letu. Mzee Kingunge atakumbukwa kwa umahiri wake wa kujenga hoja na weledi aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu, hata akaweza kuwa lulu na moja ya injini muhimu katika ustawi wa Taifa letu. Bahati mbaya watu wa aina yake wanapofariki dunia ...

Read More »

Siku Afrika ikiwa kama Marekani itakuwaje?

Na Deodatus Balile   Kwa muda sasa nafuatilia siasa za Afrika na sehemu nyngine duniani. Leo nitajadili mataifa mawili; Marekani na Kenya. Nafuatilia kinachoendelea nchini Marekani. Nafuatilia kinachoendelea nchini Kenya. Narejea misingi ya uhuru wa mawazo na uhuru wa vyombo vya habari. Nchini Marekani tangu umalizike uchaguzi mkuu wa Novemba, 2016, Rais aliyeshinda, Donald Trump amekuwa kwenye chetezo. Kutokana na ...

Read More »

Rasilimali za Tanzania na Umaskini wa Watanzania

Na William BHOKE Mwanza   Mjadala huu ninaoenda kuuzungumza ni mtazamo na maoni yangu. Nitashukuru kama mjadala huu utagonganisha fikra na mitazamo ya Watanzania wengi. Binafsi ninaamini falsafa ya mgongano wa kifkra kwani unazaa mawazo mapya na ambayo hayakuwapo. Mwezi Agosti 386 akiwa katika bustani, mwanateolojia mashuhuri wa Kanisa Katoliki, Agustino, alisikia sauti ikimwambia, “twaa na usome, twaa na usome.’’ ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons