page za ndani

Taifa limefikaje hapa? (1)

Kutokana na ile makala yangu “Pilipili usizozila zakuwashiani?” nimepokea mrejesho wa kushangaza kutoka wasomaji wa JAMHURI. Moja ya SMS hizo ilisomeka hivi nainukuu: “Brigedia Jenerali Mstaafu Francis Mbenna, shikamoo mzee wangu na hongera kwa makala zako nzuri na zenye kuelimisha na kutufundisha kwa vijana kama mimi. Baba Mungu akubariki sana. Mimi naitwa (jina limehifadhiwa). Kwa sasa napatikana Tanga ambako niko ...

Read More »

Tarime kwawaka

Tarime kwawaka *Vijana wachachamaa Zakaria kukamatwa usiku *Namba gari la ‘TISS’, la raia Tarime zafanana *Shabaha yamwokoa Zakaria, aliwindwa siku 7 *TISS waliojeruhiwa yadaiwa walitoka D’ Salaam   TARIME   NA MWANDISHI WETU   Utata umezidi kuibuka kwenye tukio la mfanyabiashara, Peter Zakaria, kuwapiga risasi maofisa wawili wa Usalama wa Taifa (TISS). Taarifa zilizosambaa wilayani Tarime zinadai kuwa watu wawili ...

Read More »

Huduma za Mwendokasi ziboreshwe

DAR ES SALAAM ALEX KAZENGA Watanzania tulio wengi tu wazuri kuzungumza, lakini kwenye kutenda baso tunasuasua. Linapokuja suala la kutenda mipango tunayozungumza huwa tunakwama-kwama. Sijajua nini tatizo na kwanini tuwe kwenye hali hiyo au kwanini hatupati suluhisho la kudumu. Nikiutazama mradi wa Mabasi ya Mwendokasi (BRT) unaosimamiwa na UDART katika Jiji la Dar es Salaam, napata mtanziko. Kwa namna usafiri ...

Read More »

Mabula abaini uzembe ukusanyaji kodi

NA MUNIR SHEMWETA, LINDI   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amefanya ziara katika mikoa ya Lindi na Ruvuma kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi, kuhamasishaji ulipaji kodi hiyo na kusikiliza kero za migogoro ya ardhi.   Wengine kwenye ziara hiyo walikuwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini, Gasper Luanda, Kaimu Kamishna wa ...

Read More »

Maskini Akwilina: Ndiyo basi? (2)

Sehemu ya kwanza ya makala hii ilitoka katika toleo na. 347. Tangu wakati huo hapakuwa na nafasi kwa makala hii na safu nyingine nyingi kutokana na nafasi zake kuwekwa hotuba za bajeti za wizara mbalimbali. Tunaomba radhi kwa usumbufu huo. Sehemu ya kwanza, mwandishi alitetea hatua ya Mwendesha Mashitaka (DPP) kufuta kesi ya mauaji iliyokuwa ikiwakabili polisi waliotuhumiwa kumuua mwanafunzi ...

Read More »

Uhusiano wa Kombe la Dunia na umeme

Kombe la soka la FIFA (Kombe la Dunia) limeanza kwa wiki zaidi ya moja sasa. Lilianza kwa kuwakutanisha wenyeji Russia dhidi ya Saudi Arabia kwenye uwanja wa Luzhniki jijini Moscow. Nimekumbuka jamaa yangu mmoja ambaye, tofauti na mimi, hana ushabiki hata kidogo wa soka. Miaka michache iliyopita nilimsikia akishangaa wenzake wakizungumzia kwa hamasa kubwa wachezaji wa timu mashuhuri za Ulaya. ...

Read More »

Ndugu Rais ‘National Breakfast Prayer’ itufunze

Ndugu Rais ni kweli kwamba ukiwa mkweli sana unaweza ukafika mahali ukasema, bora baba yangu angekuwa ni huyu mzee jirani yetu kuliko huyu baba niliyenaye! Kuna baba wengine ni kero kwa watoto wao. Na wengine kama mkosi! Tunaziona nyumba nyingi na kina baba tofauti tofauti. Utakuta baba wengine ni walevi wa kupindukia. Wengine wamepagawa kwa michepuko huku wengine kwenye uzezeta ...

Read More »

Ndani ya Wapinzani yamo yenye manufaa

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayofuata mfumo wa siasa wa vyama vingi. Tangu kurejeshwa kwa mfumo huo mwaka 1992, yamekuwapo manufaa mengi. Tutakuwa watu wa ajabu endapo tutabeza kazi nzuri na ya kutukuka iliyofanywa na baadhi ya wapinzani makini katika baadhi ya maeneo nyeti nchini. Pengine ni kwa sababu hiyo, Rais John Magufuli, amekuwa akiwasifu baadhi yao. Miongoni mwao ni ...

Read More »

Mfumo dume chanzo cha ukeketaji Ngorongoro

Watoto wa kike wanalazimishwa kuolewa Sheria za kimila zinawabeba wanaume   NGORONGORO NA ALEX KAZENGA Kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika jamii ya Kimaasai kunachochea ukeketaji watoto wa kike katika jamii hiyo wilayani Ngorongoro, Arusha. Chanzo cha kuota mizizi kwa mila hiyo kinatajwa kuwa ni mfumo dume unaotawala katika jamii hiyo. Sheria za kimila za Wamaasai zimeruhusu mwanaume kuoa wanawake ...

Read More »

Mniruhusu nimseme Mchechu akingali hai

Wiki hii nilikusudia kuandika makala fupi kueleza yale niliyoyaona kwa majirani zetu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Kama ilivyo ada ya mtembezi, yapo mabaya, lakini yapo mazuri pia anayoyaona awapo matembezini. Naomba kazi hiyo niifanye kwenye matoleo yajayo. Nimeguswa na uamuzi uliotangazwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, uliomlenga aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika ...

Read More »

Bajeti yetu, kilimo na viwanda

Balile

Na Deodatus Balile, Abuja, Nigeria Wiki hii nimekuwa hapa jijini Abuja, Nigeria. Nimepata fursa ya kukutana na Rais Mohamed Buhari wa Nigeria. Nimekutana na mawaziri wa Habari, Fedha, Viwanda na Biashara. Kukutana kwetu kumekuwa kama zari. Kilichonileta hapa Nigeria ni kuhudhuria mkutano wa mwaka wa taasisi ya International Press Institute (IPI). Kumbe Serikali ya Nigeria iliposikia kuna waandishi kutoka nchi ...

Read More »

Kasoro uhawilishaji mashamba Kusini

SONGEA NA MUNIR SHEMWETA   Uwekezaji ni jambo muhimu hasa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano ambayo msisitizo wake mkubwa ni Serikali ya Viwanda na kuelekea katika uchumi wa kati.   Hali hiyo inatokana na uwekezaji kuwa kitu kinachoweza kusaidia upatikanaji huduma muhimu sambamba na kutoa fursa ya ajira kwa wananchi na kubiresha maisha yao.   Katika ...

Read More »

Les Mangelepa alivyounda bendi ya Baba Gaston

NA MOSHY KIYUNGI Hapana shaka wadau wa muziki wanazikumbuka baadhi ya nyimbo mashuhuri zilizotamba wakati huo za Embakasi na Nyakokonya, zilizopigwa na bendi ya Orchestra Les Mangelepa. Les Mangelepa ilikuwa na wanamuziki wengi wao wakiwa ni raia toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ilikuwa na makazi yake katika jiji la Naiorbi nchini Kenya. Bendi hiyo ilitikisa vilivyo sehemu nyingi za ...

Read More »

Upangaji kabla ujenzi wa jengo kukamilika

NA BASHIR YAKUB Sehemu nyingi za mijini utaona majengo marefu na makubwa ambayo yamekuwa yakijengwa, mengi ya majengo hayo huwa yanapangishwa hata kabla ya ujenzi wake kukamilika. Mengine hupangwa hata kabla ya ujenzi kuanza, watu hutizama tu ramani ya jengo na huingia mkataba wa upangaji. Kadhalika na kodi hulipwa kutegemea na maelewano ya wahusika wenyewe. Pia kumekuwepo na ujenzi wa ...

Read More »

Sekta binafsi isionekane kuwa ni maadui wa taifa

Wadau wameisikia bajeti kuu ya Serikali. Imepokewa kwa mitazamo tofauti. Wapo waliopongeza, na wapo waliokosoa. Huo ni utaratibu wa kawaida kwani hakuna jambo linaloweza kupendwa au kuchukiwa na wote. Pamoja na kutoa unafuu kwa maeneo mbalimbali, bado tunaamini Serikali inapaswa kuendelea kujenga mazingira rafiki zaidi kati yake na sekta binafsi. Sekta binafsi ndiyo injini ya uchumi wa taifa lolote katika ...

Read More »

Polisi futeni aibu hii

Na Alex Kazenga   Kwa kipindi kirefu yamekuwepo malalamiko kutoka sehemu mbali mbali nchini watu wakilituhumu Jeshi la Polisi kutumia nguvu zilizopitiliza kwa raia wanapotuhumiwa kuwa na makosa. Hali hiyo kwa mara nyingi imeacha taharuki kwenye jamii huku baadhi ya watuhumiwa wakipata ulemavu, wengine wakipoteza uhai kutokana na kushindwa kuhimili nguvu hiyo. Uwepo wa tuhuma hizo za muda mrefu umedhihiri ...

Read More »

Serikali yabisha hodi Epanko

Serikali yabisha hodi Epanko *Wachimbaji wa sasa, wa zamani kikaangoni *Tume yapelekwa kuchunguza ukwepaji kodi *Mwekezaji avuna, wananchi waambulia soksi   MAHENGE NA ANGELA KIWIA Serikali inakusudia kuunda tume ya uchunguzi baada ya kuwapo taarifa za utoroshwaji madini ya spino (spinel) unaofanywa na baadhi ya wachimbaji na wafanyabiasha mkoani Morogoro. Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania, Profesa Shukuru Manya, ...

Read More »

Timu za Afrika sikio la kufa

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM   Wakati michezo kadhaa ya Kombe la Dunia ikiwa imepigwa katika viwanja mbalimbali nchini Urusi, timu kutoka barani Afrika hazioneshi kulitetea vema bara hili kama baadhi yake zilivyotamba wakati zikielekea Urusi.   Hadi Jumapili iliyopita, timu za Misri, Morocco na Nigeria zilikuwa zimecheza mechi zake za kwanza kwenye makundi yao huku zote zikipoteza michezo ...

Read More »

Maji yaunganisha Serikali, upinzani

*Serikali yafungua mlango uwekezaji  katika viwanda *Mbowe ataka elimu, gesi itumike kuzalisha umeme *Zitto apendekeza kodi ya maji Sh 160 kama umeme REA *Wabunge wapendekeza tozo ya maji miamala ya simu Na Waadishi Wetu, Dodoma   Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, Serikali na vyama vya upinzani wameungana kifikira kutafuta mwarobaini wa kuondoa umaskini kwa Watanzania. Serikali kwa ...

Read More »

Unyama polisi

Unyama polisi *Mahabusu aliyejifungulia polisi hatimaye azungumza *Polisi wawa ‘miungu-watu’, wananchi wakosa mtetezi *Mbunge afichua rushwa, unyanyasaji, kubambikia kesi   KILOMBERO, NA CLEMENT MAGEMBE “Mungu ndiye kimbilio hatuna tena mwingine”, haya ndiyo maneno yaliyoandikwa kwenye kanga iliyotumiwa na mahabusu Amina Mbunda (27), aliyetelekezwa akiwa na uchungu na hatimaye kujifungua bila msaada nje ya Kituo cha Polisi Mangula mkoani Morogoro. Mtoto ...

Read More »

Tusiruhusu migogoro ya kidini

Ni wiki kadhaa sasa sakata la usajili wa taasisi za dini limekuwa katika vichwa vya habari vya magazeti, huku serikali ikionesha udhaifu uliopo katika baadhi ya taasisi hizo, huku zenyewe zikikiri udhaifu na kuahidi kurekebisha. Wakati hayo yakiendelea mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba amejitokeza hadharani, kwanza kukana barua iliyosambaa mitandaoni ikiwa ...

Read More »

Waziri Mkuu ‘alinunua’ shule kihalali – Meneja

Na Waandishi Wetu, Lindi na Dodoma   Familia ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ilifuata taratibu zote halali katika kununua Shule ya Sekondari ya Nyangao, iliyopo mkoani Lindi, JAMHURI limefahamishwa. Meneja wa Shule ya Nyangao, Mathias Mkali ameliambia JAMHURI kuwa licha ya taratibu zote kufuatwa aliyenunua shule si Waziri Mkuu Majaliwa, bali aliyenunua ni mkewe Mary Benjamin Mbawala kwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons