Uchumi

JUKWAA LA WANAWAKE SOMANGILA, KIGAMBONI, LAZINDULIWA

Wanawake wajasiariliamali wametakiwa kutengeneza au kuuza bidhaa zenya ubora wa viwango vinavokubalika ili kuvutia wateja kununua bidhaa zao na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi.   Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa ...

Read More »

DK.KAMANI AWAONYA VIONGOZI VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI

MWENYEKITI wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Dk.Titus Kamani amesema Serikali kupitia tume hiyo ni awaelekeza viongozi wa Vyama vya Ushirika kutojihusisha kuuza mali za vyama hivyo pasipo kuzingatia sheria.   Hivyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuuza mali za vyama hivyo na kufafanua ili kudhibiti hali hiyo Ofisi za Mrajisi wa vyama vya ushirika imekuwa ikichukua ...

Read More »

‘BUNDI’ WA MGOGORO WA ARDHI ATUA ARUSHA

Na Charles Ndagulla, Arusha Halmashauri ya Jiji la Arusha imezidi kuandamwa na tuhuma za ugawaji holela wa ardhi inayomilikiwa na watu wengine, hivyo kuzidisha kero na malalamiko kutoka kwa wananchi. Hali hiyo imebainika ikiwa ni takribani wiki moja baada ya gazeti hili kuandika mkanganyiko wa umiliki wa kiwanja kilichopo kitalu ‘J’ namba 116, eneo la Njiro. Mgogoro huo unawahusisha watu ...

Read More »

MAJALIWA: NISHATI JIRIDHISHENI NA UBORA WA VIFAA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati ijiridhishe na ubora wa vifaa vinavyotumiwa na wakandarasi katika miradi ya umeme. Pia iwasimamie wakandarasi hao kwa ukaribu ili kuhakikisha thamani ya miradi inayotekelezwa inalingana na kiasi cha fedha wanacholipwa wakandarasi hao. Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Januari 13, 2018) wakati akizungumza katika kikao cha maendeleo ya usambazaji umeme kilichofanyika , Ofisini kwake, Dodoma. Waziri ...

Read More »

WAZIRI MKUU: TUMIENI TAMASHA LA BIASHARA KUKUZA BIASHARA YA UTALII

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Zanzibar kuhakikisha inatumia Tamashara la Biashara la Zanzibar kama chachu ya kukuza biashara ya Utalii kama ilivyo kwa Dubai Shooping Festival na matamasha mengine Duniani. “Natambua kwamba kazi ya kulipandisha hadhi zaidi tamasha letu hili si ndogo , hata hivyo ninayo imani kubwa kwamba  si tu uwezo wa ...

Read More »

WAZIRI MKUU AHIMIZA KILIMO CHA KAHAWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wajikite kwenye zao la kahawa ili wawe na zao mbadala la biashara. Ametoa wito huo leo Januari 5, 2017 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lipokela na vijiji jirani, wilayani Songea mara baada ya kukagua shamba la kahawa la Aviv Tanzania lenye ukubwa wa hekta 1,990. “Limeni ...

Read More »

BOT: BENKI ZILIZOFUNGIWA ZITAKUWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU

Benki Kuu ya Tanzania(BOT) imezifutia leseni benki 5 baada ya kukosa mtaji na fedha za kutosha kujiendesha. Benki hizo ni Covenant Bank for Women, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank, Meru Community Bank na Kagera Farmers’ Cooperative Bank. Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof Beno Ndulu amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya BOT kujiridhisha kuwa Benki hizo hazina mtaji ...

Read More »

SERIKALI YATANGAZA MCHAKATO WA ZABUNI YA UNUNUZI WA VICHWA VYA TREN YA UMEME

Serikali kupitia Kampuni Hodhi ya Reli (RAHCO) imetangaza mchakato wa awali wa zabuni ya ununuzi wa vichwa na mabehewa kwa ajili ya treni ya umeme itakayotumika katika reli ya kisasa (Standard Gauge) ambayo ujenzi wake unaendelea. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Masanja Kadogosa ameithibitishia Idara ya Habari (MAELEZO) kuanza kwa mchakato huo ambao unafuata taratibu za kimataifa za ununuzi kwa ...

Read More »

ASKOFU KAKOBE: NINA UTAJIRI ZAIDI YA SERIKALI ZOTE DUNIANI

Askofu mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship (FGBF) Zakary Kakobe amesema haofii kuchunguzwa na serikali kuhusiana na ukwasi anaoumiliki na kuongeza kuwa fedha alizonazo ni Zaidi ya fedha zinazomilikiwa na serikali nyingi Duniani. Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili kanisani hapo Askofu Kakobe amesema kuwa, hana wasiwasi wa kuchunguzwa utajiri wake na kuongeza kuwa kwa sasa anamiliki pesa ...

Read More »

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MIKOROSHO BORA RUANGWA, LINDI

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa zao la korosho Kuhakikisha wanapunguza na kuondoa Miti ya Mikorosho ambayo Inamiaka mingi shambani ambayo Inasababisha Kutoa mavuno hafifu na Yenye Ubora usiohitajika katika soko lakimataifa.    Majaliwa ameyasema hayo katika uzinduzi wa wa kampeni ya kitaifa ya upandaji wa Mikorosho Bora na Mipya Million10 katika Wilaya ya Ruangwa ...

Read More »

WAZIRI MPANGO: FEDHA ZA KIGENI MWISHO 31 DISEMBA 2017 HAPA NCHINI

Serikali imeweka zuio la matumizi ya fedha za kigeni katika manunuzi ya huduma na bidhaa mbalimbali nchini ili kulinda nguvu ya fedha ya Tanzania. Hatua hii imekuja kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni katika biashara na huduma hapa nchini ili ...

Read More »

Waziri Jafo Aitaka TBA Kufanya Kazi kwa Wakati

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI ,SELELAM JAFO amesema i WAKALA WA MAJENGO TANZANIA –TBA  umekuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya Serikali. Ametoa kauli hiyo wilayani IKUNGI mkoani SINGIDA baada ya kutembelea miradi inayotekelezwa na wakala huyo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisusua licha ya serikali kulipa ...

Read More »

BENK KUU YAITAKA AIRTEL KUWASILISHA TAARIFA ZAKE ZA KUANZIA 2000

Kufuatia sakata la umiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Disemba 28, 2017 iliziandikia benki zote na taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikisimamia akaunti za iliyokuwa Celtel, Zain au Airtel kuwasilisha taarifa hizo. BoT imezitaka taasisi hizo ama benki kueleza kama zimewahi kuendesha ama zinaendesha akaunti zinazohusiana na kampuni tajwa. Aidha, taasisi zote ambazo zitakuwa ...

Read More »

ZITTO KABWE AANIKA MALI ZAKE MTANDAONI

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe leo ameweka taarifa za mali zake zote zikiwemo, madeni anayodaiwa, mshahara na mali alizonazo kwa mwaka 2016, kama sheria inavyoagiza viongozi wa umma. Zitto pia ametoa rai kuwa ni vyema Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma likawekwa wazi mitandaoni kwa ajili ya umma ili kufahamu kila mtu anamiliki mali alizo nazo ...

Read More »

SERIKALI YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUWASILISHA MALI ZAO NDANI YA MWAKA HUU

KAMISHNA wa Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu, Harold Nsekela, amesema sheria ya maadili ya viongozi wa umma kupitia kifungu cha 9 (1) (b) inamtaka kiongozi wa ummma kila ifikapo mwisho wa mwaka kupeleka kwa kamishna wa maadili tamko la maandishi katika hati rasmi inayoorodhesha mali au rasilimali zake na za mwenza wake, watoto wake wenye ...

Read More »

Hivi Ndio Viwango Vya Makato ya Kodi ya Mishahara ya Waajiriwa

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imefafanua kuhusu viwango vya kodi, anavyopaswa kukatwa mtu binafsi aliyeajiriwa. Akizungumza kwenye kipindi cha Kodi kwa Maendeleo kinachorushwa na Shirika la Utangazaji nchini (TBC1) wiki hii, Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Makao Makuu, Gabriel Mwangosi alisema kuwa mwajiri atakata kodi, pale tu ambapo mfanyakazi au mwajiriwa anapata mshahara, kipato au ...

Read More »

Waziri Kigwangalla Aunda kamati ya Kuongoza “TANZANIA HERITAGE MONTH”

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla ameunda kamati ya kuongoza maandalizi ya namna watanzania na wageni wa Tanzania watakavyosherehekea Utanzania wao kwenye mwezi maalum utakaojulikana kama “TANZANIA HERITAGE MONTH” Akielezea wakati wa kutangaza kamati hiyo iliyojumlisha wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari, wanamichezo na wadau wengine mbalimbali na wafanyabishara, amesema: “Kwenye mwezi huu kila kitu kitakuwa cha kitanzania na tutataka kwenye ...

Read More »

MAAGIZO 5 YA WAZIRI MHAGAMA KWA PROGRAMU YA MIVARF KUOGEZA THAMANI YA BIASHARA ZA MIFUGO WILAYANI LONGIDO

Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama ameielekeza Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), kuongeza Thamani Biashara za Mifugo wilayani Longido kwa kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo. Mhagama ametoa maagizo hayo baada ya kukagua  Soko ...

Read More »

Ummy Mwalimu Asifia Benk ya NMB Kwa Kutoa Elimu ya Fedha kwa Watoto, Wazazi na Vijana

  Waziri Wa afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto,Ummy mwalimu amesema Benki ya NMB katika kipindi hiki cha serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha na kuendeleza elimu ya fedha katika ngazi zote hususan katika wanajamii Wa Tanzania. Hayo ameyaeleza Wakati akizindua rasmi kampeni ya kutoa elimu ya fedha kwa watoto, wazazi ...

Read More »

Magufuli: Naombeni Kampuni ya Total Mharakishe Ujenzi Bomba la Mafuta

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na viongozi wa kampuni ya Total ambayo ni mwekezaji mkubwa wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania na kuwahakikishia kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kwa kampuni hiyo na washirika wengine katika ujenzi wa ...

Read More »

RC Wangabo ashauri gereza la Mollo kujikita kwenye uzalishaji wa mbegu za mahindi na kuuza.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amelishauri gereza la kilimo la Mollo kuona umuhimu wa kujikita kwenye uzalishaji wa mbegu ili kuuza na gereza hilo kuweza kujiendesha na kupambana na changamoto mbalimbali zilizopo katika gereza hilo. Amesema kuwa katika mikoa ya nyanda za juu kumekuwa na shida ya uuzwaji wa mbegu feki na kupelekea malalamikomengi toka kwa ...

Read More »

Chama Cha Maofisa Uhusiano Chazinduliwa Dar

CHAMA Cha Maofisa Uhusiano wa Umma (PRST) kimezinduliwa jijini Dar es Salaam, ambapo maudhui makubwa ya kuundwa kwa umoja huo ni kutambulika rasmi kama taasisi na kupanuana mawazo ya utumishi miongoni mwa wanachama, ikiwa ni pamaoja na kuendesha shughuli zao kwa utaratibu maalum. Akihutubia katika uzinduzi huo, mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons