Habari za Kitaifa

Jaji azuia waandishi kuripoti kesi ya mauaji

Jaji Firmin Matogolo anayesikiliza shauri la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ya Himo, Humphrey Makundi, ameingia kwenye mvutano na waandishi wa habari wanaoripoti kesi hiyo baada ya kuwapiga marufuku kutonukuu chochote juu ya mwenendo wa shauri hilo. Badala yake, jaji huyo kutoka Mahakama Kuu Divesheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi akawataka waandishi hao kuingia ...

Read More »

Mkakati kuing’oa CCM mwaka 2020

Mnyukano wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza. Vyama 10 vya upinzani vimeandaa mkakati wa kisayansi kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutumia Sheria mpya ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2018. Kwa upande wake, CCM imejigamba kuwa maisha ya vyama vya upinzani katika uwanja wa siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao nchini ni ‘mahututi’. Gazeti la JAMHURI linafahamu kwamba vyama ...

Read More »

Ecobank yamwibia mteja mamilioni

Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) imeitia hatiani Ecobank Tanzania Limited kwa kumwibia mteja wake, Kampuni ya Future Trading Limited, Sh milioni 66 kutoka kwenye akaunti yake. Fedha hizo zimeibwa kwenye akaunti hiyo kupitia huduma ya internet banking na kuziingiza katika akaunti iliyoko nchini Afrika Kusini. Hukumu hiyo ya kesi namba 68 ya mwaka 2014, imetolewa na Jaji Barke Sehel. Inahusu ...

Read More »

Rais ampandisha cheo aliyekataa rushwa

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo, ameteuliwa kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, imesema uteuzi huo uliofanywa na Rais John Magufuli, umeanza Machi 31, mwaka huu. Desemba, mwaka jana, Gazeti la JAMHURI liliandika habari iliyohusu Mbibo kukataa rushwa. Baadaye Januari, mwaka huu ...

Read More »

KNCU, Lyamungo AMCOS wavutana umiliki shamba la kahawa

Mvutano mkali umeibuka baina ya Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU) na Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) cha Lyamungo kuhusu umiliki wa shamba la kahawa la Lyamungo kutokana na kila upande kudai ni mmiliki halali. Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 112 lililopo Lyamungo, Wilaya ya Hai limekuwa katika mgogoro usiokwisha kwa muda wa miaka 16 hadi sasa, hivyo ...

Read More »

Serikali yashitukia ufisadi wa milioni 71/-

Serikali imeshitukia matumizi mabaya ya fedha za makusanyo ya ardhi kiasi cha Sh milioni 71. Fedha hizo zinazodaiwa kutojulikana zilipo zinatokana na malipo ya viwanja 194 vya wakazi wa mji wa Hungumalwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza. Raia hao walitoa fedha hizo ili wapimiwe na kupewa hati za maeneo yao ya makazi na biashara. Naibu Waziri wa ...

Read More »

Polisi ‘yamtimua’ askari aliyekamata mihadarati

Jeshi la Polisi limemtimua kazi askari wake, Manga Msalaba Kumbi, mwenye namba F. 5421, kwa kile kinachodaiwa ni mwenendo mbaya kazini. Askari huyo alikuwa anafanya kazi mkoani Mwanza. Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba askari huyo alikumbwa na masahibu hayo baada ya kukamata mihadarati inayohusishwa na ‘wakubwa’ ndani ya Jeshi la Polisi. Akizungumza na Gazeti la JAMHURI, askari huyo ...

Read More »

Aliyepigwa risasi Ikulu Ndogo kuburuzwa kortini

Mtu mmoja aliyepigwa risasi na polisi akiwa maeneo ya Ikulu Ndogo inayotumiwa na Makamu wa Rais jijini Mwanza atafikishwa mahakamani baada ya matibabu. Raia huyo amelazwa Hospitali ya Rufaa mkoani hapa ya Sekou Toure akiendelea kuuguza jeraha la risasi mwilini mwake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, amelithibitishia Gazeti la JAMHURI akisema tukio hilo limetokea Machi 11, 2019 ...

Read More »

Wagombea msikiti aliojenga Nyerere

Waumini wa Kiislamu katika Kijiji cha Butiama na uongozi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mara wamo kwenye mgogoro kuhusu umiliki na uendeshaji wa msikiti uliojengwa kwa msaada wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kijijini hapo. Msikiti huo ulianza kujengwa wakati Mwalimu akingali hai, na ulifunguliwa rasmi na aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Omar Ali Juma, ...

Read More »

Gari la Polisi ladaiwa kuua bodaboda Segerea

Gari la Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadaiwa kuua dereva wa pikipiki, Cosmas Swai (42), kwa kumkanyaga kichwani akiwa amembeba mkewe, Anna Swai (39) pamoja na mwanawe, David Swai (11). Ajali hiyo imetokea Machi 12, mwaka huu, eneo la Segerea Mbuyuni, baada ya mashuhuda wa ajali hiyo kudai kuwa gari hilo ...

Read More »

Magufuli kutua China

Rais Dk. John Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuvuka mipaka ya Bara la Afrika, kwa kuitembelea China kwa ziara ya kiserikali, Gazeti la JAMHURI limebaini. China imekuwa mdau muhimu wa maendeleo wa Tanzania, kupitia mkakati mahususi wa Tanzania ya viwanda, wawekezaji kadhaa kutoka nchi hiyo ya barani Asia wameitikia wito kwa kuanzisha viwanda kadhaa hapa nchini. Vyanzo vyetu vinasema ...

Read More »

Katavi, Tabora vipi?

Mpita Njia ameshitushwa na taarifa za hivi karibuni kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshika nafasi ya tatu barani Afrika katika ndoa na mimba za utotoni. Hizi si tu ni taarifa za kushitua, bali ni taarifa za aibu katika wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano inajielekeza katika kuhimiza elimu kwa wote, kiasi cha kuondoa malipo ya ada. Hili ...

Read More »

Ajali ya ndege yaua abiria wote

Watu wote 157 waliokuwa safarini katika ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia,  Boeing 737, wamepoteza maisha baada ya ndege hiyo kuanguka. Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kuelekea mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Jumapili iliyopita. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ethiopia, abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo ni 149 na watu wengine wanane ...

Read More »

Wawekezaji wamchongea DC kwa Rais

Uamuzi wa wawekezaji wilayani Hai, Kilimanjaro kumshtaki mkuu wa wilaya (DC) hiyo kwa Rais John Magufuli umepongezwa na baadhi ya wafanyabiashara na kuonekana kuwa ni mwanzo wa kumaliza vitendo vya kunyanyaswa. DC wa Hai, Lengai ole Sabaya, anatuhumiwa na wawekezaji hao kuwa anawanyanyasa kwa kuwakamata, kuwaweka ndani na kuwaomba rushwa. Kilio chao kilichowekwa kwenye maandishi, kimewasilishwa kwa Rais Magufuli, ambaye ...

Read More »

Maji ni kichocheo cha maendeleo

Wiki ya Maji ni fursa maalumu ya sekta ya maji nchini kujitathmini kwa kujilinganisha na nchi nyingine duniani katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji. Maji ni kichocheo muhimu cha maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini, ikiwemo kilimo, biashara, utalii na viwanda. Katika kutambua umuhimu na thamani ya maji katika maisha ya binadamu na uchumi wa dunia ...

Read More »

Wizara ya Maji yataka wahandisi wazalendo

Serikali inaweka nguvu katika sekta ya maji ili kuhakikisha wananchi katika maeneo yote ya nchi wanapata huduma ya maji safi, salama, ya uhakika na yenye kutosheleza. Wajibu huu wa serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kwa Watanzania wote, bila kubagua itikadi au eneo. Aidha, sera ya maji ya mwaka 2002 inaelekeza wananchi kupata huduma ya maji safi na ...

Read More »

Lowassa anena

Waziri Mkuu (mstaafu), Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea wa ushirikiano wa kisiasa wa vyama vya upinzani, maarufu kwa jina la Ukawa, amerejea CCM wiki iliyopita akitokea Chadema, ametoa neno zito. Wakati watu wengi wakijiuliza imekuwaje Lowassa, mwanasiasa aliyetoa changamoto kubwa kwa Chama tawala  CCM ameamua kuhama upinzani kurejea CCM, majibu sasa yameanza kujitokeza kuwa Lowassa ni mfia nchi. “Mzee amesema yeye ...

Read More »

Rais anadanganywa ili iweje?

Mwishoni mwa mwaka jana Mpita Njia (MN) alisoma kwenye vyombo vya habari ahadi aliyopewa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli. MN anakumbuka vema kuwa ahadi hiyo ilitolewa na ‘wakubwa’ waliokuwa kwenye ziara mkoani Mara, na kituo kilichohusika kilikuwa cha Wilaya ya Butiama. Kwenye Uwanja wa Mwenge kijijini Butiama, watendaji wa Wizara ya Ujenzi, kwa ...

Read More »

Uamuzi mbovu wachelewesha Liganga

Serikali imepiga ‘stop’ kuendelea kwa mradi wa uchimbaji chuma cha Liganga hadi uhakiki utakapofanyika pamoja na kukamilishwa mambo kadhaa, likiwemo la kurejewa kwa mkataba husika pamoja na kuangalia masilahi ya taifa yafikie kiwango cha juu. Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba kuna masuala yanafanyiwa mapitio, ikiwa ni pamoja na uhakiki wa fidia na muundo wa mkataba. Mkataba huo wa ...

Read More »

‘Watumishi wa umma msitumike kisiasa’

Serikali imewakumbusha watumishi wa umma nchini kutotumika kisiasa, badala yake watimize majukumu yao kikamilifu. Maelezo hayo kwa watumishi hao wa serikali yametolewa hivi karibuni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, akiwa wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Katika ziara yake hiyo, naibu waziri huyo licha ya kukutana na watumishi wa ...

Read More »

Mvutano waendelea ‘stendi’ Moshi

Mvutano unaendelea kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na wafanyabiashara wenye maduka katika Jengo la Biashara la Stendi Kuu ya Mabasi mjini Moshi. Mvutano huo unahusu mkataba mpya wa upangaji baada ya ule wa awali wa miaka 15 kumalizika Desemba 30, mwaka jana. Wafanyabiashara wanapinga ongezeko kubwa la kodi. Jengo hilo la ghorofa tatu lilijengwa kwa ubia na wahisani ...

Read More »

Apokwa nyumba kwa deni la mkewe

Chama cha kukopesha wanawake cha Muunganiko wa Wanawake Sekta Isiyo Rasmi Dar es Salaam (MUWASIDA) kwa kushirikiana na Kampuni ya udalali ya Namic Investment Ltd, wanatuhumiwa kuuza nyumba ya Mbegu Kangamika (72) kwa mizengwe. Nyumba hiyo Na. 255 ipo Mtaa wa Bombani, Pugu katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Iliuzwa kwa mnada Machi 4, 2009 kwa kile kilichodaiwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons