Nyundo ya Wiki

Jaji anyang’anywa jalada la mauaji Moshi

Na Charles Ndagulla, Moshi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Aishiel Sumari, amenyang’anywa jalada la kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Scolastica, Humphrey Makundi (16), JAMHURI limebaini. Hatua hii imekuja siku chache baada ya JAMHURI kupata taarifa za kiuchunguzi zenye kuonyesha kuwa Jaji Sumari alikuwa analalamikiwa, gazeti likachapisha taarifa ...

Read More »

Moyo wa hisani unatupiga chenga Watanzania

Majuma mawili yalilopita nilishiriki hafla ya kuchangisha pesa za hisani iliyofanyika Ojai, kwenye Jimbo la California nchini Marekani. Ni hafla inayoandaliwa kila mwaka na Global Resource Alliance, shirika lisilo la kiserikali linalosimamia utekelezaji wa miradi ya kusaidia jamii mkoani Mara. Ojai ni mbali. Nimeanza safari Alhamisi na kufika Jumamosi. Kwa ndege, siyo kwa basi la Zuberi. Siyo rahisi kusafiri zaidi ...

Read More »

Uhuru wa habari uanzie kwenye vyumba vya habari

DODOMA. EDITHA MAJURA. Serikali na Vyombo vya habari, wametuhumiana kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini. Wakati serikali ikituhumiwa kutofanya vizuri katika kudhibiti usalama wa wanahabari wanapotekeleza majukumu yao, serikali nayo imesema vyombo vya habari vinaminya maslahi ya wanahabari kiasi cha kusababisha washindwe kutekeleza majukumu yao kwa weledi unaohitajika. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akijibu ...

Read More »

Ndugu Rais, amani kwanza mengine tutayapata kwa ziada

Ndugu Rais, lengo la maandiko yetu siku zote siyo kukosoa. Udhaifu wa kuandika kwa sababu unampenda mtu au unamchukia mtu, Mwenyezi Mungu katuepusha nao. Hatuandiki kwa ushabiki wa kumshabikia mtu au chama fulani. Wala hatuandiki hapa kwa lengo la kusifia au kupongeza. Tunaandika kile ambacho tunaamini kuwa ni ukweli mtupu, kwa lengo la kushauri tu. Tunaamini kuwa kwa hizi busara ...

Read More »

Uvunjaji Chako ni Chako wageuka kitanzi DODOMA

EDITHA MAJURA Imebuka sintofahamu kubwa kutokana na uvunjaji wa jengo la Chako ni Chako mjini Dodoma, baada ya kuwapo harufu ya eneo hilo kuviziwa na “wakubwa”, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imevunja jengo lililokuwa maarufu kwa jina la Chako ni Chako, ambalo kwa miaka mingi limekuwa likitumiwa kwa biashara ya kuuza nyama ya kuku waliochomwa – ‘Kuku choma’. ...

Read More »

Pingu Yaibua `Zengwe’ kwa Mtuhumiwa wa Mauaji Moshi

Na Charles Ndagulla,Moshi Hatua ya kutofungwa pingu kwa mmoja wa Wakurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica, Edward Shayo (63), anayetuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Humphrey Makundi imezua utata na kuhojiwa na baadhi ya mahabusu wa gereza la Karanga mjini Moshi. Shayo alikuwa miongoni mwa watuhumiwa 11 waliokamatwa kufuatia mauaji ya mwanafunzi huyo aliyetoweka shuleni hapo ...

Read More »

Msimamo wa AG Mpya Kuhusu Makinikia

Andiko hili ni la Mwanassheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi. Aliliandika mwaka jana akiwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Tawi la Arusha. Dk. Kilangi kitaaluma ni mwanasheria ambaye miongoni mwa maeneo aliyobobea ni kwenye sheria za madini. Aliandika makala hii ukiwa ni mtazamo wake binafsi akichangia kwenye mjadala wa makinikia baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya ...

Read More »

Heri ya Mwaka Mpya na Muhogo

Balile

Mpendwa msomaji nakutakia heri ya mwaka mpya 2018. Mungu alipo hakuna cha kuharibika. Nikiri kuwa katika kuumwa nimepata fursa ya kufahamu Watanzania wanavyofuatilia kazi ya mikono yangu na hasa hili suala la muhogo. Nimegundua kuwa Watanzania wengi wana nia ya kujiondoa katika lindi la umaskini. Sitanii, kwanza niwie radhi msomaji wiki iliyopita, makala hii ilikuwa na makosa ya hijai (spelling ...

Read More »

PROF ABDALLAH SAFFARI: Haja ya Kuwa na Mahakama ya Juu Tanzania

Tarehe 9 Desemba mpiga solo mahiri Tanzania kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Nguza Viking, kwa lakabu ya muziki, Big Sound alitoka Gereza la Ukonga, Dar es Salaam ambako alikuwa akitumikia kifungo cha maisha. Aliachiwa baada ya kunufaika na msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa kwa baadhi ya wafungwa wapatao elfu nane katika hotuba aliyoitoa mjini Dodoma kusherekea siku ...

Read More »

Waziri Lukuvi Nisaidie

Mimi ni Mtanzania ambaye kwa sasa nipo nchini Marekani nikijiendeleza  na kufanya shughuli mbalimbali kwa ajili ya kujikimu kimaisha. Mwaka 2008 nilikuja nyumbani (Tanzania) na kuelekea mkoani Mbeya kutafuta kiwanja cha makazi. Nilifanikiwa kupata kiwanja na kukabidhiwa hati miliki namba 12477 iliyotolewa Julai 10, 2008 na Msajili wa Hati Mbeya. Mwaka jana nilirudi tena hapa nyumbani na kutembelea mkoani Mbeya ...

Read More »

CUF wabemenda demokrasia

Na Thobias Mwanakatwe   MGOGORO wa kiasiasa unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) umedhihiriha jinsi viongozi wanavyofinyanga sharia na demokrasia ya vyama vingi ilivyo na mwendo mrefu kabla ya kufikiwa. Chama hicho ambacho ni cha tatu kwa ukubwa nchini, mgogoro wake ulianza baada ya Prof. Ibrahimu Lipumba kujizulu nafasi ya uenyekiti wa taifa wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba ...

Read More »

Mtetezi wa uhifadhi afungwa Loliondo

Mtetezi wa uhifadhi katika Pori Tengefu la Loliondo, Gabriel ole Killel, amefungwa gerezani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni chuki kutoka kwa viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambao amekuwa akiwapinga. Killel ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya KIDUPO, amefungwa gerezani katika kesi mbili tofauti, kati ya tatu zilizofunguliwa dhidi yake. Akiwa amehukumiwa kesi ya kwanza kutumikia jela miezi sita, ...

Read More »

Lukuvi aweka historia

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amevunja historia katika kutatua migogoro ya ardhi nchini na zamu hii ametumia zaidi ya saa 20 kusikiliza kero za wananchi akiwa ofisini Dar es Salaam. JAMHURI limemshuhudia Lukuvi siku ya Ijumaa kuamkia Jumamosi iliyopita akitoka ofisini saa 08:30 baada ya kusikiliza kero za ardhi kutoka kwa wananchi 189 wa Kanda ...

Read More »

Kenya wafurahi Harbinder kuswekwa rumande

Wakati mfanyabiashara maarufu Harbinder Singh Sethi akiendelea kusota rumande kutokana na kesi inayomkabiri kuhusu sakata la akaunti ya Escrow, yenye mashtaka 12, vyombo vya habari nchini Kenya vimeandika kashfa kadhaa zilizowahi kufanywa na mfanyabiashara huyo. Mtandao wa Standard Digital wa nchini Kenya, umechapisha katika tovuti yake tuhuma zilizowahi kufanywa na Sethi miaka zaidi ya 20 iliyopita. Kashfa hizo zimechapichwa katika ...

Read More »

Polisi washiriki magendo Moshi

Askari wa Jeshi la Polisi, mgambo na baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanatajwa kutumiwa na genge la wafanyabiashara wa mahindi kuwezesha usafirishaji mahindi kwa njia za panya kwenda nchi jirani ya Kenya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Magari yote yanayovuka mpaka wa Tanzania kwenda Kenya yamekuwa yakivuka kwa usaidizi wa askari polisi waliopo katika vituo vya polisi ...

Read More »

Nani kasema Bodi ya Wakurugenzi Acacia ndiyo timu yao ya majadiliano?

Tutofautishe timu ya majadiliano na Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni. Kawaida timu ya majadiliano haiundwi na wakurugenzi wa kampuni, bali wakurugenzi wa kampuni ndio huwa wanateua watu wa kuunda timu ya majadiliano na hao walioteuliwa huripoti matokeo ya majadiliano kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya utekelezaji. Bodi ya Wakurugenzi husubiri taarifa ya timu ya wataalam kwa ajili ya utekelezaji. ...

Read More »

Utetezi wa Acacia huu hapa

Naomba kuweka wazi kuwa, pamoja na juhudi za mazungumzo kati yetu na Serikali ya Tanzania, hakuna makubaliano yoyote ya kulipa kama vyombo vya habari vinavyoendelea kuripoti. Kile kilichowasilishwa katika ripoti za kamati ya kwanza na ya pili siyo matokeo sahihi, licha ya kile kinachoelezwa na kuaminika na wengi. Hatujawahi kuiba, hatujawahi kukwepa kodi, hatujawahi kughushi nyaraka kukwepa kulipa mirabaha na ...

Read More »

Sijasikia ACCACIA wakijitetea, namsikia Mtanzania Tundu Lissu akiwatetea!

Sijasikia ACACIA wakijitetea, bali namsikia Mtanzania mwenzetu Tundu Lissu katika maandishi na video zinazoenezwa mtandaoni kwa kasi ya ajabu akiwatetea kwa nguvu na kwa pumzi zake zote. Ni kuhusu mchanga wenye madini uliozuiwa na Serikali bandarini. Amezungumzia mambo ambayo nitayajibu hapa kwa lengo kubwa kabisa la kutaka Watanzania wafahamu.   Je, sheria inasema mchanga ni mali ya ACACIA? Lissu anasema ...

Read More »

Utajiri Mhasibu Takukuru watisha

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, imetoa amri ya zuio la mali za Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai. Amri ya Mahakama ya Kisutu ilitolewa Mei 8, mwaka huu; na Gugai anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa na mengine kulingana na tuhuma zinazomkabili. Kuzuiwa kwa mali hizo kumetokana na maombi yaliyowasilishwa ...

Read More »

Ugaidi waifilisi Benki FBME

Kufungwa kwa benki ya FBME, hapa nchini, kumetokana na tuhuma za benki hiyo kutakatisha fedha na kupitisha fedha za kufadhili ugaidi ambazo zimekuwa zikipitishiwa kwenye matawi yake ya Nicosia, Cyprus na Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam, JAMHURI limebaini. Julai, 2014 Benki Kuu ya Cyprus, pamoja na Benki Kuu ya Tanzania, waliingilia kati na kuanza kuchunguza, uchunguzi huo ...

Read More »

Anne Makinda yamfika

Uamuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, wa kuwafurusha wakurugenzi na watumishi kadhaa wa Mfuko huo, unaelekea kuitia Serikali hasara ya Sh bilioni 9. Kiasi hicho cha fedha huenda kikalipwa kwa watumishi hao ambao uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa wamesimamishwa na wengine kufukuzwa kazi kinyume cha sheria. Muda mfupi baada ya ...

Read More »

‘Bureau de Change’ zafungwa Dar

Vyombo vya dola vimefunga maduka kadhaa ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) jijini Dar es Salaam, yanayohusishwa na utakatishaji na usafirishaji fedha zinazotokana na biashara ya dawa za kulevya. Vyanzo vya habari vya uhakika vimelithibitishia JAMHURI kuwa tayari maduka matano yamefungwa kwenye operesheni hiyo inayohusisha Kikosi Kazi kinachoundwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Jeshi la ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons