Nyundo ya Wiki

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 12

IDARA YA UHAMIAJI 257. Uhamiaji ni idara ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani yenye majukumu na wajibu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Uhamiaji (The Immigration Act, 1995). Majukumu ya Idara ya Uhamiaji yanajumuisha kuzuia uingiaji nchini Tanzania wa watu ambao si raia wa Tanzania ambao kwa mujibu sheria hawatakiwi nchini (prohibited immigrants), pamoja na kudhibiti utokaji na uingiaji nchini ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 11

Polisi wanalea dawa za kulevya   Mapendekezo 244. Tume inatoa mapendekezo yenye madhumuni ya kupunguza na hatimaye kuondoa wimbi la rushwa inayotokana na vitendo ndani ya Jeshi la Polisi kama ifuatavyo: a) Ziwepo jitihada za makusudi zitakazoelekezwa kwenye kuelimishana kuhusu umuhimu wa Jeshi la Polisi katika maendeleo ya taifa letu. Semina na warsha ziwajumuishe pamoja viongozi na watendaji wakuu wa ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 9

Polisi waliiharibu TAKUKURU   YALIYOJITOKEZA   154. Tume imetafakari kwa undani muundo wa taasisi na shughuli za kurugenzi zote. Katika kufanya hivyo, umuhimu wa Kurugenzi ya Mafunzo, Utafiti na Elimu kwa Umma umetiliwa maanani hasa kwa kuzingatia jukumu lake zito la kuzuia rushwa. Aidha, umuhimu wa kugundua na kufuatilia asilimia kubwa ya tuhuma za rushwa pia unazingatiwa. Ufanisi wa taasisi ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 7

Uteuzi unanuka upendeleo serikalini   Ukiukwaji taratibu na udhaifu katika usimamizi  80. Sheria na taratibu za utumishi zilizowekwa na Serikali kimsingi ni nzuri na endapo zinatekelezwa ipasavyo, utendaji wa Serikali utakuwa mzuri. Kinyume na matakwa ya sheria na taratibu hizo, imekuwa jambo la kawaida kwa shughuli za Serikali kuendeshwa bila kuzingatia kanuni.  81. Kwa mfano, sheria za utumishi zimeeleza hatua ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 6

Rais asiachiwe zigo la rushwa MAADILI YA NYONGEZA KWA MAWAZIRI NA WAKUU WA MIKOA 50. Sehemu ya Nne ya Sheria inaweka masharti maalumu kwa mawaziri na wakuu wa mikoa. Wakuu wa wilaya hawakuhusishwa ingawaje wameorodheshwa kama viongozi wa umma. Maadili yaliyotajwa katika sehemu hii ni yale ambayo yanafahamika na kuzingatiwa na nchi zote zinazofuata mfumo wa Baraza la Mawaziri. Maadili ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 5

Majaji, mahakimu ni shida V:  WAJIBU WA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI 1. Umma wa Tanzania umekuwa unakerwa sana na kuenea kwa rushwa nchini, hasa ile inayodaiwa na watumishi wa umma katika ngazi za chini kutokana na hali ngumu ya maisha. Rushwa ya aina hii imeufikisha umma pahala pagumu kiasi kwamba umeshawishika kukata tamaa ya kupata haki yoyote ile bila ...

Read More »

Wafanyabiashara wahojiwe, mali zitaifishwe

Sehemu ya tatu ya ripoti hii ya Jaji Joseph Warioba iliyochapishwa wiki iliyopita, kwa kiasi kikubwa ilizungumzia maadili ya viongozi na hatua ya viongozi kufanya biashara wakiwa madarakani kwa kuuza hadi vidani vya wake zao kwa wafanyabiashara. Wiki hii, tunakuletea sehemu ya nne yenye mambo na mapendekezo muhimu. Endelea…   1. KUSAFISHA UONGOZI ULIOPO NA KUJENGA MAADILI YA VIONGOZI WA ...

Read More »

Uongozi mbovu unachochea rushwa

Wiki iliyopita tulichapisha sehemu ya pili ya Ripoti ya Rushwa ya Jaji Warioba. Pamoja na mambo mengine, iligusia ukaribu wa viongozi kwa wafanyabiashara nchini ulivyochochea ukuaji wa rushwa nchini. Leo tunakuletea sehemu ya tatu. Endelea…    (iii) Ukosefu wa uwazi (Transparency) katika utendaji  Miaka ya hivi karibuni taifa limeshuhudia kutoweka kwa uwazi katika uendeshaji wa shughuli za umma katika ngazi ...

Read More »

Ripoti ya Warioba ya Rushwa inatisha (2)

Katika sehemu ya kwanza ya ripoti hii, tulikuletea hadidu rejea alizopewa Jaji Joseph Warioba na wajumbe wenzake wa Tume ya Kuchunguza Kero ya Rushwa Nchini na sehemu ya vyombo vya dola vilivyotajwa kuwa wanakula rushwa. Katika sehemu ya pili leo, tunakuletea mwendelezo wa ripoti hiyo. Endelea…   VYOMBO VYA HABARI: (i) Waandishi  hupokea rushwa ili kuandika au kutoandika, kutangaza au ...

Read More »

Ripoti ya Warioba ya Rushwa inatisha

Mwaka huu, Tanzania inaye Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli. Rais Magufuli, ameonyesha nia ya dhati ya kupambana na vitendo vya rushwa nchini, na hasa baada ya kuanzisha rasmi mchakato wa Mahakama ya Mafisadi kwa kuitengea bajeti katika mwaka huu wa fedha. Katika kuunga mkono juhudi zake, Gazeti la JAMHURI, linaloanzia wanapoishia wengine, limeamua kuchapisha Ripoti ya ...

Read More »

Mawaziri wakikwepa kiwanda cha saruji

Wakazi wa kata za Boko na Bunju jijini Dar es Salaam ambao wamekilalamikia kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement (Wazo) kwa kuharibu mazingira wamewalalamikia Mawaziri wa Wizara ya Muungano na Mazingira kwa kushindwa kuchukua hatua kwa kiwanda hicho. Pamoja na Mawaziri hao kufikishiwa taarifa za uharibifu wa mazingira unaosababishwa na kiwanda hicho ambao umeathiri makazi na uharibifu wa mali za ...

Read More »

Kashfa ya nyumba NIC

Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeingia katika kashfa ya kuhujumu mali za shirika hilo, ikiwamo ya kuuza nyumba bila kuzingatia maagizo yaliyotolewa na Serikali Oktoba, 2009. Nyumba zilizopangishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo zilizoko eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam katika viwanja namba 75-78, Block 45B ziliuzwa kwa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), bila kuingizwa kwenye orodha ...

Read More »

Barua ya elimu kwa Rais Magufuli – 2

Wiki iliyopita mwandishi wa makala hii ndugu Kalisti Mjuni, alizungumzia umuhimu na mbinu bora za kuandaa walimu. Katika sehemu ya pili, leo Mjuni anazungumzia mahitaji ya msingi kwa utoaji wa elimu bora. Endelea… Mazingira bora. Ili kazi yoyote iweze kufanyika kwa ufanisi, hatuna budi kuweka vizuri mazingira ya kufanyia kazi hiyo, hali kadhalika, ili tuweze kutoa elimu bora, hatuna budi ...

Read More »

Mabilioni yatafunwa NIP

Mradi wa uendelezaji viwanja viwili vilivyoko Mtaa wa Ohio (Plot 775/39 na 776/39) vya Shirika la Tija la Taifa (NIP), unaonekana kuwa ni ‘hewa’ kutokana na kutokamilishwa kwa mujibu wa makubaliano ya wabia wawili waliojitokeza kuendeleza viwanja hivyo kwa nyakati tofauti. Ujenzi wa mradi huo ulilenga kujenga ghorofa 35 ambazo ujenzi wake ungegharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 50 ...

Read More »

Takukuru wachunguza Saccos Moshi

Ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni 6 katika Chama Cha Akiba na Mikopo (Wazalendo Saccos) mkoani Kilimanjaro, umeendelea kuibua mapya kwa utoaji wa mikopo kwa watu ambao si wanachama wakiwamo marehemu. Wizi wa fedha zilizokopwa kutoka taasisi mbalimbali za fedha ulihusisha fedha taslimu na kuwalipa watu ambao hawakuwa wanachama wa chama hicho, na kukiuka taratibu za uendeshaji wa vyama vya ushirika. ...

Read More »

Waliotafuna Sh bilioni 6 watamba mitaani Moshi

Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk. Audax Rutabanzibwa, kwa miaka mitano sasa, ama ameshindwa, au amepuuza kuandaa mashitaka dhidi ya viongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Wazalendo cha mjini Moshi wanaotuhumiwa kuiba Sh bilioni 6. Miongoni mwa watuhumiwa wa utafunaji fedha hizo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Profesa Faustine Bee. Pamoja ...

Read More »

Kanisa la Wasabato linapodhulumu …

Mimi Baraka Mukundi, mkazi wa Arusha niliajiriwa na Kanisa la Wasabato Makao Makuu Arusha, Tanzania mwaka 1986. Niliendelea kufanya kazi na kanisa hilo katika vitengo vyake mbalimbali kwa kadri walivyokuwa wakinipangia kazi kulingana na taratibu za Kanisa za ajira. Kipindi cha mwaka 1999 nilihamishiwa katika kiwanda kilichokuwa kinamiikiwa na kanisa, kilichojulikana kama INTERNATIONAL HEALTH FOODS OF SDA CHURCH, ambacho kilikuwa ...

Read More »

Katibu Mkuu asalimu amri

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya, hatimaye amesalimu amri na kurejesha gari, mali ya Serikali alilojimilikisha akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa, Kanda ya Mbeya. Gari hilo – Toyota Land Cruiser VX V8 – lenye namba STK 8299, ni mali ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, lakini ...

Read More »

Wananchi 3,000 wasotea fidia Mbeya

Wananchi 3,113 wa Mbarali mkoani Mbeya, waliohamishwa kutoka katika vijiji wilayani humo kupisha upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kabla ya kupunjwa fidia za maeneo yao, wamesema Serikali imeshindwa kuwalipa fidia licha ya kutathmini upya maeneo yao mwishoni mwa mwaka 2015. Wakati harakati za Uchaguzi Mkuu zilipoanza mwaka jana, walitishia kuachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu za ...

Read More »

Sumaye ahusishwa ‘uporaji’ kampuni

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sincon, Peter Siniga amemwandia barua Rais Dk. John Magufuli akimtaka kuingilia kati sakata la dhuluma dhidi yake iliyodaiwa kusukwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye. Barua yenye Kumb. Na. SN/PRE/2015/11/01 kwenda kwa Rais Dk. Magufuli iliyoandikwa na kusainiwa na Siniga, Novemba 26, 2015 inazungumza dhuluma katika biashara ya ubinafsishaji wa Shirika la vyuma-National Steel Corporation ...

Read More »

Wafanyakazi wachapwa viboko

Wafanyakazi wa Kampuni ya Usangu Logistics wanatarajia kuiburuza kampuni hiyo kortini kutokana na kuchapwa viboko, kufukuzwa kazi kinyume cha sheria na kunyimwa stahiki. Wanasema mwajiri wao mwenye asili ya Kiarabu, amekuwa akiwachapa bakora na kuwakata mishahara bila sababu za msingi, akiwarejesha kwenye historia ya utawala wa kikoloni, jambo ambalo halina nafasi kwenye Serikali ya kutetea wanyonge ya Rais Dk. John ...

Read More »

Wakubwa wahujumu tanzanite

Mwekezaji katika mgodi wa uchimbaji wa madini ya tanzanite na mmiliki wa Kampuni ya TanzaniteOne Mining Ltd, anadaiwa kufanya hujuma katika biashara ya madini nchini. Mwekezaji huyo ambaye anamiliki asilimia 50 ya mgodi huo anaelezwa kufanya hujuma ya kutorosha madini katika mgodi huo na kuyasafirisha nje ya nchi bila kuishirikisha Serikali ambayo ni mbia wake kupitika Shirika la Taifa la ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons