Nyundo ya Wiki

Mawaziri wakikwepa kiwanda cha saruji

Wakazi wa kata za Boko na Bunju jijini Dar es Salaam ambao wamekilalamikia kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement (Wazo) kwa kuharibu mazingira wamewalalamikia Mawaziri wa Wizara ya Muungano na Mazingira kwa kushindwa kuchukua hatua kwa kiwanda hicho. Pamoja na Mawaziri hao kufikishiwa taarifa za uharibifu wa mazingira unaosababishwa na kiwanda hicho ambao umeathiri makazi na uharibifu wa mali za ...

Read More »

Kashfa ya nyumba NIC

Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeingia katika kashfa ya kuhujumu mali za shirika hilo, ikiwamo ya kuuza nyumba bila kuzingatia maagizo yaliyotolewa na Serikali Oktoba, 2009. Nyumba zilizopangishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo zilizoko eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam katika viwanja namba 75-78, Block 45B ziliuzwa kwa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), bila kuingizwa kwenye orodha ...

Read More »

Barua ya elimu kwa Rais Magufuli – 2

Wiki iliyopita mwandishi wa makala hii ndugu Kalisti Mjuni, alizungumzia umuhimu na mbinu bora za kuandaa walimu. Katika sehemu ya pili, leo Mjuni anazungumzia mahitaji ya msingi kwa utoaji wa elimu bora. Endelea… Mazingira bora. Ili kazi yoyote iweze kufanyika kwa ufanisi, hatuna budi kuweka vizuri mazingira ya kufanyia kazi hiyo, hali kadhalika, ili tuweze kutoa elimu bora, hatuna budi ...

Read More »

Mabilioni yatafunwa NIP

Mradi wa uendelezaji viwanja viwili vilivyoko Mtaa wa Ohio (Plot 775/39 na 776/39) vya Shirika la Tija la Taifa (NIP), unaonekana kuwa ni ‘hewa’ kutokana na kutokamilishwa kwa mujibu wa makubaliano ya wabia wawili waliojitokeza kuendeleza viwanja hivyo kwa nyakati tofauti. Ujenzi wa mradi huo ulilenga kujenga ghorofa 35 ambazo ujenzi wake ungegharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 50 ...

Read More »

Takukuru wachunguza Saccos Moshi

Ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni 6 katika Chama Cha Akiba na Mikopo (Wazalendo Saccos) mkoani Kilimanjaro, umeendelea kuibua mapya kwa utoaji wa mikopo kwa watu ambao si wanachama wakiwamo marehemu. Wizi wa fedha zilizokopwa kutoka taasisi mbalimbali za fedha ulihusisha fedha taslimu na kuwalipa watu ambao hawakuwa wanachama wa chama hicho, na kukiuka taratibu za uendeshaji wa vyama vya ushirika. ...

Read More »

Waliotafuna Sh bilioni 6 watamba mitaani Moshi

Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk. Audax Rutabanzibwa, kwa miaka mitano sasa, ama ameshindwa, au amepuuza kuandaa mashitaka dhidi ya viongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Wazalendo cha mjini Moshi wanaotuhumiwa kuiba Sh bilioni 6. Miongoni mwa watuhumiwa wa utafunaji fedha hizo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Profesa Faustine Bee. Pamoja ...

Read More »

Kanisa la Wasabato linapodhulumu …

Mimi Baraka Mukundi, mkazi wa Arusha niliajiriwa na Kanisa la Wasabato Makao Makuu Arusha, Tanzania mwaka 1986. Niliendelea kufanya kazi na kanisa hilo katika vitengo vyake mbalimbali kwa kadri walivyokuwa wakinipangia kazi kulingana na taratibu za Kanisa za ajira. Kipindi cha mwaka 1999 nilihamishiwa katika kiwanda kilichokuwa kinamiikiwa na kanisa, kilichojulikana kama INTERNATIONAL HEALTH FOODS OF SDA CHURCH, ambacho kilikuwa ...

Read More »

Katibu Mkuu asalimu amri

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya, hatimaye amesalimu amri na kurejesha gari, mali ya Serikali alilojimilikisha akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa, Kanda ya Mbeya. Gari hilo – Toyota Land Cruiser VX V8 – lenye namba STK 8299, ni mali ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, lakini ...

Read More »

Wananchi 3,000 wasotea fidia Mbeya

Wananchi 3,113 wa Mbarali mkoani Mbeya, waliohamishwa kutoka katika vijiji wilayani humo kupisha upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kabla ya kupunjwa fidia za maeneo yao, wamesema Serikali imeshindwa kuwalipa fidia licha ya kutathmini upya maeneo yao mwishoni mwa mwaka 2015. Wakati harakati za Uchaguzi Mkuu zilipoanza mwaka jana, walitishia kuachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu za ...

Read More »

Sumaye ahusishwa ‘uporaji’ kampuni

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sincon, Peter Siniga amemwandia barua Rais Dk. John Magufuli akimtaka kuingilia kati sakata la dhuluma dhidi yake iliyodaiwa kusukwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye. Barua yenye Kumb. Na. SN/PRE/2015/11/01 kwenda kwa Rais Dk. Magufuli iliyoandikwa na kusainiwa na Siniga, Novemba 26, 2015 inazungumza dhuluma katika biashara ya ubinafsishaji wa Shirika la vyuma-National Steel Corporation ...

Read More »

Wafanyakazi wachapwa viboko

Wafanyakazi wa Kampuni ya Usangu Logistics wanatarajia kuiburuza kampuni hiyo kortini kutokana na kuchapwa viboko, kufukuzwa kazi kinyume cha sheria na kunyimwa stahiki. Wanasema mwajiri wao mwenye asili ya Kiarabu, amekuwa akiwachapa bakora na kuwakata mishahara bila sababu za msingi, akiwarejesha kwenye historia ya utawala wa kikoloni, jambo ambalo halina nafasi kwenye Serikali ya kutetea wanyonge ya Rais Dk. John ...

Read More »

Wakubwa wahujumu tanzanite

Mwekezaji katika mgodi wa uchimbaji wa madini ya tanzanite na mmiliki wa Kampuni ya TanzaniteOne Mining Ltd, anadaiwa kufanya hujuma katika biashara ya madini nchini. Mwekezaji huyo ambaye anamiliki asilimia 50 ya mgodi huo anaelezwa kufanya hujuma ya kutorosha madini katika mgodi huo na kuyasafirisha nje ya nchi bila kuishirikisha Serikali ambayo ni mbia wake kupitika Shirika la Taifa la ...

Read More »

Walioitumbua Ngorongoro waanza kutumbuliwa

Kusimamishwa kazi kwa wahasibu watano na watumishi wengine 15 wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa tuhuma za ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi za Mamlaka hiyo, kunatajwa kuwa hakujamaliza wimbi la ufisadi katika Mamlaka hiyo. JAMHURI imethibitishiwa kuwa kuna mtikisiko mwingine mkubwa utakaoikumba NCAA ambao utashuhudia wengine wakitimuliwa. Ngorongoro, Mamlaka inayokusanya mabilioni ya shilingi kila mwaka huku kiasi kikubwa ...

Read More »

Mkuu wa Mkoa K’njaro atangaza operesheshi sita

Mkuu wa Mkoa (RC) wa Kilimanjaro, Amos Makalla, ametangaza operesheni sita kabambe zikilenga kukomesha uhalifu, kuhimiza uwajibikaji, kulinda afya za wananchi na kutunza mazingira.  RC Makalla alitangaza operesheni hizo kwenye kikao cha kazi kilichowahusisha wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro, wakurugenzi, wakuu wa idara na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa wilaya za mkoa huo. Operesheni ...

Read More »

Wakenya wanavyoziua Serengeti, Loliondo

Baadhi ya wageni hao wamediriki kuendesha shughuli za ufugaji katika Hifadhi ya Taifa Serengeti (SENAPA), na kilimo katika vijiji vya Tarafa ya Loliondo. Matrekta mengi yanayotumiwa katika kilimo eneo la Loliondo yanatolewa Kenya. JAMHURI limepata majina zaidi ya 280 ya Wakenya wanaoishi Ngorongoro, ambao baadhi yao wamekimbia wakihofu uongozi mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli. ...

Read More »

Jipu la ujangili

Kazi ya kudhibiti ujangili katika mbuga na hifadhi za Taifa ni ngumu, kwani askari waliokabidhiwa kazi ya kulinda wanyama ndiyo wanaofanya ujangili, uchunguzi umebaini. Vyanzo mbalimbali vya habari vimesema ikiwa Rais Magufuli anataka kunusuru wanyama nchini, inamlazimu kusitisha ajira za askari karibu wote wanaolinda mbunga na hifadhi kisha kuajiri upya baada ya kuwachekecha vilivyo.  Askari wa wanyamapori katika Mamlaka ya ...

Read More »

‘Yaliyonikuta Precision Air’

Sauti nyororo ya mwana mama inapokea simu, na kabla sijasema lolote, nakaribishwa kwa maneno: “Precision Air, Can I Help You?” Baada ya kujua nazungumza Kiswahili, ananiuliza: “Nikusaidie…” Namjibu: “Naam, naomba kununua tiketi ya kwenda Musoma Jumanne tarehe 19, 2016…” Baada ya maswali mafupi na kwa sauti iliyojaa ukarimu, naambiwa naweza kulipa tiketi kwa kutumia njia ya M-Pesa au tIGO Pesa. ...

Read More »

Ufisadi mwingine Uhamiaji

Ikiwa zimepita wiki mbili tangu Rais Dk. John Magufuli awasimamishe kazi Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile, na Kamishna wa Fedha na Utawala, Piniel Mgonja, mambo mapya yameanza kuibuka. Vyanzo vya habari kutoka ndani ya idara hiyo vinasema Serikali imefanya ukaguzi maalumu na kugundua ubadhirifu wa fedha, jambo ambalo limeanza kuzua taharuki. Ukaguzi huo unafanywa huku kukiibuliwa taarifa za makamishna ...

Read More »

Madudu zaidi Leopard Tours

Tuhuma za ukwepaji kodi za Serikali na uonevu dhidi ya wafanyakazi zimeendelea kuibuliwa dhidi ya kampuni ya utalii nchini ya Leopard Tours yenye makao yake jijini Arusha. Kampuni hiyo inatajwa kuwa ni nambari wani kwa ukubwa na usafirishaji wageni katika hifadhi na mapori mbalimbali nchini. Inakisiwa kuwa na Land Cruiser zaidi ya 280. Nyaraka ambazo Gazeti la JAMHURI zimelipata zinaonyesha ...

Read More »

Matajiri 3 mbaroni kwa mauaji Moshi

Hatimaye watuhumiwa watatu kati ya watano wa mauaji ya John Massawe, katika Kijiji cha Kindi, Kibosho mkoani Kilimanjaro, wamekamatwa. Masawe aliuawa kikatili Juni 9, 2009 kijijini hapo, lakini baadaye watuhumiwa wa mauaji hayo wakaachwa. Waliokamatwa na kuwekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Moshi ni John Kisoka (Magazeti) na mkewe ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja. Mwingine ni ...

Read More »

UDA kumtumbua Iddi Simba

Serikali imeanza taratibu za kufufua kesi ya ufisadi wa uuzwaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambalo ni mali ya umma. Vyanzo vya habari vya uhakika vimelithibitishia JAMHURI kuwa Serikali ya Awamu ya Tano tayari imeshaanza kufuatilia Shirika hilo ambalo uuzwaji wake unatajwa kugubikwa na rushwa ya hali ya juu. Duru za uchunguzi zinaonyesha kuwa hata kufutwa kwa ...

Read More »

Bandari, TRA wanavyohujumu kodi

Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inayo kazi ya ziada kudhibiti uvujaji wa mapato, kwani imebainika kuwa waliokabidhiwa kazi ya kukusanya kodi, wamejipanga kuhujumu mapato ya nchi, uchunguzi wa gazeti JAMHURI kwa mwaka mmoja umebaini. Imebainika kuwa makontena yanayoleta sintofahamu kuanzia Novemba, mwaka jana pale Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini, mtandao wake ni mpana kuliko ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons