Michezo

Tukatae mamluki soka

Kuvamiwa kwa mchezo wa soka na mamluki katika ngazi ya klabu na timu za taifa ni miongoni mwa sababu zinazochangia kudorora kwa mchezo huo nchini. Akizungumza na JAMHURI, mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Mohamed Hussein (Chinga One), amesema mchezo wa soka umevamiwa na mamluki wasiokuwa na dira wala mwelekeo wa kuuendeleza. Mchezaji huyo ...

Read More »

Ujio wa Everton ni fursa

Tanzania imeendelea kunufaika kiuchumi na ujio wa baadhi ya wachezaji wanaokuja kupumzika baada ya kukamilika kwa ligi katika nchi hizo. Wachezaji hao ambao wengi wanatoka katika Ligi Kuu ya Uingereza wamekuja nchini kwa mapumziko ya msimu baada ya kumalizika kwa ligi kuu nchini humo (EPL). Wachezaji waliokuja nchini ni Morgan Schneiderlin wa klabu ya Everton ya Uingereza, David Beckham, Mkenya ...

Read More »

Hekaheka uchaguzi TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linakwenda kufanya uchaguzi wake, huku aliyekuwa Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, akiwa miongoni mwa wagombea ambao mpaka wikiendi walikuwa wamechukua fomu za kugombea tena nafasi ya uongozi. Malinzi amekuwa Rais wa TFF, katika kipindi cha miaka minne iliyopita, baada ya kurithi mikoba ya mtangulizi wake, Leodegar Tenga, ambaye aliliongoza Shirikisho hilo katika ...

Read More »

Nyambui: Tuwekeze kwenye riadha

Kocha wa Riadha wa Timu ya Taifa la Brunei, ambaye pia amepata kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui, amekishauri Chama cha Riadha kuwekeza nguvu nyingi katika ujenzi wa misingi mizuri kwa watoto wenye vipaji.   Amesema mchezo wa riadha ni miongoni mwa michezo ambayo ikipata uangalizi mzuri unaweza kuzalisha ajira nyingi kwa vijana katika nchi ...

Read More »

Tuwekeze soka la vijana

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshauriwa kutafuta wadhamini wenye uwezo wa kujenga vituo vya kukuza vipaji, kuliko kuendelea kuokoteza wachezaji. JAMHURI limezungumza na wadau wa soka, ambao wamesema mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, yanayoendelea nchini Gabon, yameonesha udhaifu kwenye timu ya Serengeti Boys. Hata kutolewa kwa vijana hao katika mashindano hayo yanayoendelea nchini Gabon, ...

Read More »

Serengeti Boys mbele kwa mbele

Timu ya Taifa ya Vijana  chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, imeendelea kufanya vema katika mashindano ya AFCON yanayoendelea nchini Gabon. Serengeti Boys imefanya jambo ambalo Watanzania wamekuwa wakilisubiri kwa muda mrefu, kushiriki na kuleta ushindani katika mashindano ya kimataifa. Timu hiyo imecheza mechi mbili za ushindani mkubwa katika kundi lake, mechi ya kwanza walicheza na mabingwa watetezi timu ya vijana ...

Read More »

Tenga ajiandaa kuleta mageuzi katika soka

Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Chilla Tenga, amesema jukumu lake la kwanza katika majukumu yake mapya katika kamati ya usimamizi wa leseni za klabu za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ni kuhakikisha ustawi wa klabu na timu za taifa. Akizungumza na JAMHURI mara baada ya kupata nafasi hiyo, amesema soka katika bara la Afrika ...

Read More »

Dua zetu kwa Serengeti Boys

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeendelea na maandalizi ya mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kuanza Jumapili ya wiki hii, huko Gabon. Katika maandalizi ya kuelekea katika mashindano hayo, timu hiyo imeshinda michezo mitatu mfululizo, imeshinda mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon, mechi zilizochezwa nchini Morocco ilikokuwa imeweka kambi kabla ya kwenda nchini Cameroon. Timu ...

Read More »

Conte ajawa mchecheto EPL

Ligi Kuu nchini Uingereza imeingia katika hatua ya lala salama huku nafasi ya kutwaa ubingwa ikiwa mikononi mwa vilabu vya Chelsea yenye alama 78 kwa kucheza michezo 33 na Tottenham Hotspur yenye alama 74 ikiwa na michezo 33. Kutokana na timu hizo kukaribiana kwa kuwa na tofauti ya alama 4 kati yao Kocha wa Klabu ya Chelsea, Antonio Conte ameliomba ...

Read More »

Serikali yaiokoa TFF

Serikali imeingilia kati kulinusuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya ofisi zake kufungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kushindwa kulipa kodi ya shilingi bilioni 1 inayodaiwa kwa miaka mingi. Deni hilo lilitokana na TFF kushindwa kuwalipia kodi makocha wa kigeni, Mbrazili Marcio Maximo, Jan Poulsen na Kim Poulsem, raia wa Denmark, walioajiriwa kuzifundisha timu za ...

Read More »

Miaka minane ya kifo cha Michael Jackson

Juni 25, mwaka huu, itakuwa imetimia miaka minane tangu Michael Jackson ‘Wacko Jacko’ alipoiaga dunia. Alikuwa ni mwanamuziki mwenye vipaji vingi kutoka nchini Marekani. Alifahamika zaidi kwa jina la heshima la ‘Mfalme wa Pop’. Michael alitambulika kama mburudishaji aliyepata mafanikio zaidi kwa muda wote. Alikuwa mmoja kati ya waburudishaji wenye mvuto na hadhira kubwa katika medani ya muziki. Michango yake ...

Read More »

Kocha wa kuogelea alete manufaa

Ujio wa kocha wa mchezo wa kuogelea, Sue Purchase, kutoka Shule ya Kimataifa ya Mtakatifu Felix ya Uingereza, unatarajiwa kurejesha ari ya mchezo huo ambao umeanza kupotea nchini katika miaka ya hivi karibuni. Kocha huyo raia wa Uingereza, amekuja nchini kusaka vipaji vya mchezo huo kwenye mashindano ya Taifa yaliyofanyika wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo ya klabu ...

Read More »

Kufungwa ofisi TFF kunaathiri timu

Siku chache baada ya Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, wakala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuzifunga ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushindwa kulipa kodi, wadau wamesema hali hiyo inaweza kuchangia kudhoofisha ushiriki wa timu ya Serengeti Boys katika fainali za Afrika nchini Gabon. Viongozi na wafanyakazi wa TFF wamekuwa wanafanya kazi chini ...

Read More »

Utamaduni ulindwe

Mamlaka husika zimetakiwa kuwa makini katika kuhakikisha zinatengeneza mazingira rafiki kwa wasanii wa nyimbo za asili, ambao wapo wachache kutokana na ukosefu wa soko katika burudani hiyo. Imebainika kuwa baadhi ya wasanii wanaofanya sanaa za utamaduni ikiwamo ngoma, nyimbo za asili na mashairi, wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi kwa kuwa kipato chao kinategemea kazi kutoka taasisi mbambali pale wanapokuwa ...

Read More »

ZFA sasa tunaekelea FIFA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewatoa hofu wapenzi wa michezo nchini kwa kusema kuwa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika hakuwezi kudhoofisha uhusiano mzuri uliopo kati ya TFF na ZFA. Akizungumza na JAMHURI, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, mara baada ya kurejea nchini akitokea Addis Ababa nchini Ethiopia, ambako alishiriki katika ...

Read More »

Yanga mguu sawa

Huku ikiendelea na harakati za kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Dar es Salaam Young Africans ‘Yanga’, yenye makao yake makuu mitaa ya Twiga na Jangwani, Jijini, inaendelea na mikakati ya kushinda mechi yake na Zesco, kutoka Zambia. Mechi ya kwanza kati ya klabu hiyo na Wazambia hao inatarajiwa kuchezwa Jumamosi, jijini na kurudiana wiki moja ...

Read More »

Usalama viwanjani changamoto

Suala la usalama ndani na nje ya viwanja vya soka limebaki kuwa tishio kwa wachezaji na watazamaji wa mchezo huo, hali inayoendelea kupunguza idadi ya watu wanaokwenda kutazama mechi, barani Afrika. Mara nyingi ajali katika viwanja zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji waliokabidhiwa majukumu ya kusimamia mchezo, hali inayowaweka wachezaji na watazamaji katika hatari. Katika mwendelezo wa ajali ...

Read More »

Riadha yapata msisimko

Baada ya mchezo wa riadha kufanya vibaya kwa muda mrefu na kuanza kupoteza msisimko miongoni mwa Watanzania, sasa unaonekana kurudisha msisimko baada ya mafanikio kutoka kwa mwanariadha Felix Simbu. Ushindi wa Simbu katika mashindano ya mbio za Standard Chartered Mumbai Maradhon huko India, umeonekana kuwa tumaini jipya katika mchezo huo. Kijana huyo alimaliza mbio hizo kwa muda wa 2:09:32 na ...

Read More »

Tanzania na ndoto za Olympic 2020

Wadau wa mchezo wa soka wameishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Tanzania (TFF) juu ya kufanya maboresho yatakayo saidia timu ya taifa kupata nafasi ya kushiriki katika mashindano kadha ya kimataifa ikiwemo Olympic inayotarajia kufanyika nchini Japan mwaka 2020. Hivi karibuni TFF imeitangaza Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 23 Kilimanjaro Worriors kwa ajili ya ...

Read More »

FIFA kufanya mapinduzi ya soka

Rais mpya wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amekuja na mapendekezo mapya ya kutaka kufanya mabadiliko katika mchezo wa soka. Baada ya kuongeza timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2026 na kufikia 48, Rais huyo amekuja na mapendekezo mapya jinsi anavyotaka soka liendeshwe. Katika ujumbe alioutoa kupitia Mkurugenzi wa Ufundi wa FIFA, Maco van Basten, amependekeza sheria mpya katika ...

Read More »

EPL kuwakosa wachezaji 26

Wakati baadhi ya mataifa yakijiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), baadhi ya ligi za barani Ulaya zitawakosa nyota wake wanaotoka barani Afrika. Ligi ya Uingereza pekee itawakosa wachezaji 26. Fainali hizo za AFCON zitaanza kutimua vumbi Januari 14, mwaka huu nchini Gabon. JAMHURI inakuletea baadhi ya majina ya wachezaji watakaozikosa baadhi ya mechi za Ligi Kuu ...

Read More »

Viwanja kaburi la soka

Soka la Tanzania litaendelea kushuka endapo juhudi za makusudi hazitafanyika na mamlaka husika kurudisha viwanja vyote vya michezo vinavyotumika kinyume na taratibu. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati tofauti, wadau wa soka, wanasema japokuwa soka la Tanzania linakabiliwa na changamoto nyingi, bado kuna tatizo la ukosefu wa viwanja vya michezo. Katibu wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDRFA), ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons