JAMHURI YA WAUNGWANA

Wamarekani, Waafrika Kusini watuache

Taifa linahitaji fedha. Haya mambo makubwa ya kimaendeleo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano yatawezekana tu endapo ari ya kubuni, kuendeleza na kusimamia vyanzo vya mapato ya ndani vitatambuliwa na kulindwa kwa nguvu zote. Kama ambavyo Rais John Magufuli amekuwa akisema mara kwa mara, Tanzania ni tajiri kiasi kwamba tukijipanga vema tunaweza kujitosheleza kwa mapato yetu. Dalili zimeanza kuonekana. ...

Read More »

Wavamizi hawa si wa kuchekewa

Nimesoma tamko la serikali linalohusu uamuzi ‘mgumu’ ilioamua kuuchukua dhidi ya wavamizi wa hifadhi mkoani Kigoma. Tathmini iliyofanyika mkoani humo imeonyesha hifadhi za misitu na mapori ya akiba yamevamiwa kwa shughuli za kilimo, ufugaji, ukataji miti na baadhi ya vijiji vimesajiliwa ndani ya maeneo hayo. Uvamizi huu umesababisha athari nyingi zikiwamo za kupotea kwa uoto wa asili na viumbe hai, wakiwamo ...

Read More »

Wanyama wanamalizwa Loliondo

Hadi naandika makala hii, mizogo ya tembo wanane imeonekana katika Kijiji cha Maaloni, Arash, Ngorongoro mkoani Arusha. Miezi miwili, katika Kitongoji cha Karkamoru, Loliondo pekee twiga wanane wameuawa. Watuhumiwa wa ujangili wamekwisha kukamatwa, japo kuna taarifa kuwa wahusika wenyewe bado wamo mitaani. Mauaji hayo ya twiga ni tofauti na haya ya tembo. Tembo wanakufa kwa namna inayotia shaka. Mizoga hii ...

Read More »

Uongozi Hospitali ya Amana haukumtendea haki marehemu

Kumetokea jambo ambalo nimejitahidi nibaki nalo moyoni lakini nafsi imegoma kabisa. Nafsi imegoma kwa sababu naamini kulinyamazia kutahalalisha matukio mengine mengi ya aina hii yaendelee kufanywa. Wiki iliyopita tulipata taarifa ya msiba wa mtu tunayemfahamu. Hana umaarufu, lakini ni binadamu mwenzetu. Huyu alikuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Jina lake ...

Read More »

Mbowe: CCM wamevuruga Uchaguzi

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Uchaguzi Mdogo wa Madiwani 43 uliofanyika Jumapili umevurugwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimkakati, hivyo baadhi ya maeneo wamemua kujitoa ikiwamo Mkoa wa Manyara. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (pichani) ameliambia JAMHURI kuwa zamu hii CCM wametumia mbinu ya kuanzisha utaratibu wa kuwapa barua maalum za utambulisho mawakala wa vyama, ambapo wale wa ...

Read More »

 Serikali ikiwa mbaya, CCM itakuwaje nzuri?

Vinara wawili, kati ya wale wanaotuhumiwa kuifanya Loliondo isitawalike, wamewatumia wanasheria wao kuniandikia barua wakitaka ‘nisiwaguse’ kwa chochote kinachoendelea Loliondo. Edward Porokwa na Maanda Ngoitiko, wanaamini kwa kuninyamazisha mimi na Gazeti la JAMHURI, ‘sifa na utukufu’ wao katika Loliondo, vitaendelea kudumu! Maandishi ya wanasheria wao yameandikwa kwa lugha ya mbwembwe nyingi, lakini sikuona mahali walipokanusha yaliyoandikwa juu ya Loliondo na ...

Read More »

Sioni faida za kuwakamata

Wale wanaofanya rejea ya hali ya kisiasa nchini mwetu watakumbuka Augustino Mrema alivyokuwa na nguvu kubwa kisiasa mwaka 1995. Wapo ambao wanaamini hadi leo kuwa kama si mbinu na ushawishi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, historia ya leo ya nchi hii ingekuwa tofauti. Mrema alikuwa na nguvu kubwa kisiasa. Alipendwa na alipata wafuasi wengi kuanzia kwa makabwela ...

Read More »

Funzo kutoka kwenye kodi ya majengo

Mamia kwa maelfu ya wananchi, wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kulipa kodi ya majengo. Muda uliopangwa ulipungua. Umeongezwa kwa wiki kadhaa, lakini bado idadi ya watu wanaojitokeza kulipa ni kubwa mno. Maombi ya wananchi ya kuomba kuongezewa muda yameitikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Muda wa malipo bila faini umeongezwa hadi Julai 31, mwaka huu. Nchini kote kumeripotiwa misururu ya ...

Read More »

Tumuunge mkono Waziri Mkuu Majaliwa

Akiahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julai 5, mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na mambo mengine, alizungumzia sekta ya wanyamapori. Kwa wahifadhi wengi, kauli ya Waziri Mkuu imewapa matumaini mapya yenye kuwawezesha kuona mwanga katika suala zima la uhifadhi nchini. Kama alivyosema, asilimia 28 ya eneo la nchi yetu limetengwa ...

Read More »

Walijaribu ushoga wakafeli, wamegeukia mimba za wanafunzi

Rais John Magufuli ameutolea uamuzi mjadala wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaopata mimba. Rais Magufuli, akiwahutubia wananchi mkoani Pwani, amesema bayana kuwa hayuko tayari kuona wanafunzi wanaotiwa mimba wakiendelea na masomo katika shule za Serikali. Akayaambia mashirika yasiyo ya Serikali kwamba kama yanatetea hao ‘wazazi’ kuendelea na masomo, basi yawaandalie shule, lakini yeye hatokuwa tayari. Msimamo huo ...

Read More »

Tuwaogope waporaji kwa kuwa ni Wazungu?

Wamarekani wanaweza kuwa na tofauti zao za ndani, lakini linapokuja suala linalohusu maslahi ya taifa lao huungana na kuwa wamoja. Ndivyo nchi inavyopaswa kuwa. Waasisi wa taifa letu walitambua thamani ya umoja na mshikamano wa wananchi. Wakautambua umoja kama moja ya tunu adhimu katika kulijenga taifa imara. Awamu ya Kwanza ya uongozi wa Taifa letu ilifanya kazi kubwa sana ya ...

Read More »

Maendeleo hayaji kwa kuchekeana

Bajeti Kuu ya Serikali tayari imesomwa bungeni Dodoma. Imesheheni mambo mengi. Wataalamu wa uchumi wamejitokeza kusema waliyoyaona. Wapo wanaopongeza, kadhalika wapo wanaoikosoa. Wakosoaji wanahoji ukubwa wa tarakimu za bajeti hiyo. Wanasema kama iliyopita imeyekelezwa kwa kiwango kisichozidi asilimia 50; kwanini hii ya mwaka huu wa 2017/2018 nayo iwe na tarakimu nyingi zaidi. Jibu wanalo waandaaji. Pamoja na yote yanayosemwa, walau ...

Read More »

Hakuna mtalii wa kuja kuwaona punda-vihongwe

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, wakati wowote wiki hii, anatarajiwa kuwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018. Kama ilivyo ada, Wizara ya Maliasili na Utalii ni miongoni mwa wizara chache zenye mvuto, na kwa maana hiyo hupata orodha ndefu ya wabunge wanaochangia. Mvuto wa wizara hii unatokana na sababu kadhaa. Mosi, hii ...

Read More »

Mfumo wa kuwapata wabunge EALA haufai

Tumewapata Watanzania kenda ambao kwa miaka mitano ijayo watatuwakilisha kwenye Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Waliochaguliwa ni Fancy Nkuhi (CCM), Happiness Legiko (CCM), Maryamu Ussi Yahya (CCM), Dk. Abdullah Makame (CCM), Dk. Ngwaru Maghembe (CCM), Adam Kimbisa (CCM), Habib Mnyaa (CUF), Josephine Lemoyan (CHADEMA) na Pamela Massay (CHADEMA). Sina shaka na uwezo wa baadhi ya wabunge wetu hawa kutuwakilisha katika ...

Read More »

Hivi hadi leo hatujamwelewa Magufuli?

Kwanza naomba nitumie fursa hii kuungana na wazazi, ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na watoto wetu – wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha – katika ajali iliyotokea Karatu. Taarifa ya awali iliyotolewa na Ikulu ilithibitisha kuwa wanafunzi 32 na walimu wawili walikuwa wameaga dunia katika ajali hiyo. Huu ni msiba mkubwa, si ...

Read More »

‘Woga ndio silaha dhaifu kuliko zote’

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amezungumza jambo la maana sana. Amewataka wananchi wasilalame tu, badala yake wachukue hatua dhidi ya ukiukwaji wa haki pale unapojitokeza. Amewataka watumie vyombo kama Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mahakama na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kutatua yale yanayowasibu kwa upande wa haki. Profesa Kabudi amesema: ...

Read More »

Nimeelimisha, nimehadharisha na nimeonya kuhusu Loliondo

Kuna taarifa zisizo na shaka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amehakikisha anapeleka taarifa ya ‘kutungwa’ kwa Waziri Mkuu. Amependekeza Pori Tengefu la Loliondo lifutwe, badala yake kuanzishwe Hifadhi ya Jamii (WMA). Haya ni mapendekezo yake, wala si ya wajumbe wa Kamati. Hili jambo hatuna budi kulisema mapema kwani endapo ulaghai wake utaaminiwa na viongozi wakuu wa Serikali, ...

Read More »

Wakenya wajue funguo za Bologonja ziliondoka na Mwalimu Nyerere

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kwa kusaidiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka, wameendelea na sanaa yao Loliondo. Wameandika ripoti ndefu iliyojaa hadaa na kuipeleka kwa Waziri Mkuu wakitaka kumwaminisha kuwa ndio makubaliano ya wadau waliounda Kamati ya Kutatua Mgorogoro wa Loliondo. Magazeti kadhaa yakaibuka na vichwa vya habari ‘Mgogoro wa Loliondo waisha’! Si kweli hata ...

Read More »

Watetezi wa uhifadhi wasichoke

Kwa mwongo zaidi ya mmoja, nimekuwa miongoni mwa waandishi waliosimama kidete kutetea uhai wa wanyamapori na misitu. Mathalani, tumeamini kuwa bila Loliondo, Hifadhi ya Taifa Serengeti (SENAPA) haipo! Bila Loliondo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) haipo; wala Masaai-Mara iliyopo Kenya, haiwezi kubaki salama. Loliondo ndiyo roho ya hifadhi hizi zote. Kwa miaka zaidi ya 10 yamesemwa mengi na watu ...

Read More »

Kuwafukuza, kuwashusha vyeo walimu ni kuwaonea

Ualimu ni kada muhimu kweli kweli kwa maendeleo ya jamii yoyote. Taifa linaloipuuza kada hii halina mwisho mwema. Matokeo ya kidato cha nne nchini yaliyotolewa wiki iliyopita, yamepokewa kwa mitazamo tofauti. Shule binafsi zimeendelea kung’ara dhidi ya shule za umma. Hili ni tatizo. Duniani kote, taasisi za umma – shule, vyuo, hospitali – ndizo zinazong’ara kwenye matokeo mazuri. Zama zetu ...

Read More »

Umaskini umekuwa mtaji wa ‘manabii wa uongo’

Kwanza, naomba nitangaze maslahi yangu kwenye makala hii. Nayo ni kwamba naamini Mungu yupo. Sijawahi kutilia shaka uwepo wa Muumba kwa sababu ni vigumu mno kuamini kuwa haya yote tunayoyashuhudia, kuanzia kwenye uumbaji, ni mambo yaliyojitokeza yenyewe tu! Haiwezekani. Mungu yupo. Mungu ametujalia wanadamu maarifa na vipawa mbalimbali. Ni kwa sababu hiyo, kuna watu wenye huruma, ilhali wapo wengine ambao ...

Read More »

Amri hizi ni za uonevu

Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kadhaa wamepiga marufuku matumizi ya nafaka kutengenezea pombe. Wengine wameenda mbali zaidi kwa kuwaamuru wakulima kutouza mahidi mabichi. Mwishoni mwa mwaka juzi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipiga marufuku matumizi ya chakula cha msaada kutumika kutengenezea pombe.  Hapa kuna upigaji marufuku unaofanana, ingawa mmoja unaweza kuwa na mantiki. Huu wa Waziri Mkuu una mantiki ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons