Siku nilipoitwa ofisini kwa Mwalimu…
Mwalimu anaumwa? Ni swali linalotuumiza. Hatuamini. Walio karibu wanazo taarifa, lakini wanatakiwa wawe watulivu maana kusambaza taarifa za ugonjwa wa Mwalimu kungeweza kuibua taharuki kwa maelfu na kwa mamilioni ya Watanzania waliompenda. Mwalimu ametoka Butiama Septemba 23, 1999. Amewasili Msasani usiku. Amepumzika. Usiku wote ninawaza namna ya kufanya, maana tumenong’onezwa kuwa kesho atakwenda kwenye matibabu…