Siasa

FIKRA YA HEKIMA

 

Wabunge hawa hawatufai

 

Nianze kwa kuwapa pole mawaziri Shamshi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Dk. Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), waliopitiwa na rungu la Rais Jakaya Kikwete la kuvuliwa nyadhifa hizo, wiki iliyopita. Huo ndiyo uwajibikaji wa kisiasa.

Read More »

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (9)

Katika sehemu ya nane, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema Rais ndiye aliyekiri kosa la Zanzibar kuingia katika OIC na pili ndiye aliyelazimika kukiri kule Dodoma kwamba utaratibu wa kushughulikia hoja ya Utanganyika ulikosewa lakini mawaziri wake mara zote mbili walitulia tu nakumuacha Rais ndiye akiri kosa na kubeba lawama. Ifuatayo ni sehemu ya kitabu cha Mwalimu Nyerere alichokiandika mwaka 1994 cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Endelea...

 

Katiba ya nchi yetu, na utaratibu tunaojaribu kujenga, vinataka kuwa katika hali kama hiyo, Mawaziri ndiyo wawajibike, na hivyo kumlinda Rais, si Rais awajibike, na kuwalinda Mawaziri wake, na tena  kwa kosa ambalo si lake. Watu walioshindwa uongozi Bungeni, hata tukafikishwa hapa tulipo leo, ni Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM.

Read More »

FASIHI FASAHA

Lissu ni malaika, waziri au mwanasiasa?


Ni takriban wiki tatu sasa tangu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kipate mtikisiko mkubwa, mithili ya pata shika na nguo kuchanika, baada ya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kuwavua nyadhifa zote viongozi wake watatu.

Read More »

KONA YA AFYA

Sababu za kupungua nguvu za kiume -5


Wiki iliyopita, Dk. Khamisi Ibrahim Zephania alizungumzia kwa kina homoni ya kiume na umuhimu wake katika tendo la ndoa. Sasa endelea kumfuatilia zaidi…

Panahitajika ubongo, neva, homoni, mishipa ya damu, tezi [glands], utendaji mzuri wa figo, ini, baadhi ya misuli na viungo chungu nzima ndani ya mwili kama tutakavyoona katika makala zetu za mbele.

Read More »

Milima, mabonde ya Nelson Mandela

 

Mpigania haki za weusi na alama kuu ya udhalimu wa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Mzee Nelson Madiba Mandela, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu, kutokana na maambukizo ya mapafu kushindwa kutengamaa.

Read More »

Nyerere na Uhuru wa Tanganyika

Nazungumzia Uhuru wa Tanganyika. Sizungumziii Uhuru wa Tanzania Bara.

Majuzi niliona mabango yaliyosambazwa jijini Dar es Salaam. Mabango hayo yalisomeka “SHEREHE ZA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA BARA”.

Read More »

Zuma: Nelson Mandela amepumzika kwa amani

Alhamisi usiku Desemba 5 mwaka huu, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini,  alitangaza kifo cha Rais wa kwanza mweusi nchini humo, Nelson Mandela, ambaye amefariki dunia  akiwa na umri wa miaka 95.

Read More »

FIKRA YA HEKIMA

Kikwete kwa hili lazima nikupongeze


Jakaya Mrisho Kikwete (JK), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Kuna taarifa kwamba umewaongezea muda wa kazi viongozi wa ngazi ya juu katika vyombo vya ulinzi na usalama waliopaswa kustaafu kipindi hiki.

Read More »

NUKUU ZA WIKI

Julius Nyerere: Kufikiri unajua kila kitu ni hatari

“Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja ya kujifunza tena. Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo.”

 

Read More »

Serikali iondoe sheria kandamizi kwa vyombo vya habari

Ndugu Mhariri

Natamani Watanzania kwa ujumla wetu tuwe na uelewa wa nguvu wa vyombo vya habari. Ikiwezekana tuingie barabarani kuishinikiza serikali iondoe sheria nzima ambayo ni kandamizi dhidi ya vyombo vya habari hivi.

Read More »

Prince Charles, JK wateta ujangili

Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Uingereza, Prince Charles, ambaye pia ni mtoto wa Malkia wa nchi hiyo, Elizabeth, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua zake za dhati za kulinda wanyamapori na kupambana na ujangili dhidi ya tembo na faru, taarifa ya Ikulu imesema.

Read More »

Maswi: Gesi imeanza kuwatajirisha Mtwara

“Kazi ya kuunganisha na kusambaza mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam imefikia hatua ya kuridhisha. Kazi hiyo inafanywa na  mashirika yenye uzoefu mkubwa kimataifa, ambayo ni Shirika la Teknolojia na Mendeleo ya Petroli la China (CPTDC), Kampuni ya Kutengeneza Mabomba ya China (CCP), Worley Parsons Limited na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Tayari mpaka sasa kilomita 142 kati ya 542 zimekamilika. Mradi huo unaotarajiwa kukamilika Desemba mwakani na utakuwa na mitambo ya kisasa.”

Read More »

Kinachonifanya nimpende Lowassa, hitimisho

Wakati naandaa makala niliyosema “Kinachonifanya nimpende Lowassa ni hiki” na kuichapisha katika gazeti hili la JAMHURI wiki iliyopita, hayakuwa mategemeo yangu kama makala hiyo ingeigusa jamii kwa kiasi nilichokishuhudia. Nimepigiwa simu nyingi mno, nimetumiwa ujumbe mfupi wa maandishi mwingi,  na bado mpaka sasa naendelea kupokea simu na ujumbe!

Read More »

FASIHI FASAHA

Vyama vya upinzani ni vichanga? -4

Katika sehemu ya tatu ya makala haya wiki iliyopita, nilizungumza uchanga wa vyama vya siasa na malengo yao. Pia niligusia kauli iliyotolewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wakati wa Uchaguzi Mkuu 1995 kuhusu uwezo wa vyama vya upinzani kushinda katika uchaguzi mkuu wa 2015. Leo tunaendelea…

Hivi tunavyozungumza CCM na vyama vya upinzani kila kimoja kimo katika harakati ya kupanga mipango ya kushinda uchaguzi huo. CCM itafikisha miaka 38 na baadhi ya vyama vya upinzani vitafikisha miaka 23. Hapatakuwa tena na suala la uchanga wala watoto. Labda suala la utoto!

Read More »

FIKRA YA HEKIMA

Kagame, Museveni, mkataa wengi ni mchawi

Ndoto za Rais wa Rwanda, Paul Kagame, na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kutaka kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimeyeyuka.

Sasa ushindi uko mikononi mwa UTATU MWAMINIFU (Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya).

Read More »

Kibanda alistahili Tuzo ya Mwangosi

Ni siku ya historia ya pekee hapa Tanzania, siku ambayo mwandishi wa habari Absalom Kibanda na mjane wa Daudi Mwangosi, Itika, wamemwaga machozi mbele ya umati wa waandishi wa habari ukumbini.

Read More »

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

 

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (6)

Wiki iliyopita tulikuletea sehemu ya tano ya mtiririko wa maandiko ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere juu ya Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Katika kitabu alichokiandika mwaka 1994, Mwalimu alisema: “Ati Chama hakiwezi kupinga Bunge lake, lakini kwa mantiki ya ajabu ajabu wabunge wanaweza kupinga chama chao! Hiyo ndiyo demokrasia halisi ya mageuzi. Nilirudi Butiama nikalipa ada yangu ya CCM na nikaandika utenzi wa Tanzania Tanzania!” Endelea...

Jukumu la kueleza taarifa hii ya Serikali katika Halmashauri Kuu ya Taifa aliachiwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mheshimiwa Samuel Sitta. Baadaye, baada ya kikao nilimtafuta Ndugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki.

Read More »

Katiba ya nchi siyo ya CCM

Mhariri JAMHURI,

Nachukukua nafasi hii kwanza kulipongeza Gazeti la JAMHURI kwa kujitolea kuweka wazi kuhusu dawa za kulevya na pia kuhusu  uwindaji haramu.

Read More »

Chadema sasa wajiandaa kutumia nguvu Ukerewe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, kimetamba kwamba kitatumia nguvu ya umma kuishinikiza Mahakama imtoe rumande Mbunge Salvatory Machemli. Mahakama ya Wilaya iliamuru Mbunge wa Ukerewe apewe adhabu ya kwenda jela siku 14 kuanzia Novemba 6 hadi 20, mwaka huu, kutokana na kudharau amri iliyomtaka ahudhurie mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi namba 19/2013 inayomkabili.

Read More »

Sababu za kupungua nguvu za kiume -2

Udumavu wa kufika kileleni: Huu ni upungufu wa nguvu za kiume. Ni hali ya kufika kileleni ambayo hutokea kwa polepole sana au kushindwa au kutokuwa na uwezo kabisa wa kufika kileleni kutokana na ukosefu wa shahawa. Ufikaji kileleni unaorudi: Huu pia ni upungufu wa nguvu za kiume. Ni hali ambayo ule mshindo wa raha (unaotokana na ufikaji kileleni) hulazimishwa kurudi ...

Read More »

Kikwete: Kagame, Museveni, Kenyatta wamenishangaza

 

Asema wamevuja Mkataba, Itifaki ya Afrika Mashariki

Asisitiza Tanzania inaipenda Jumuiya, haitatoka kamwe

Aonya wasahau ardhi, ajira, kuharakisha shirikisho

Alhamishi wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza mambo manne ya msingi. Amezungumzia mchakato wa Katiba mpya, Operesheni Tokomeza,  ushiriki wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na hatima ya Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kutokana na umuhimu wa hotuba hii, na historia inayoweza kuwa imewekwa na hotuba hii katika siku za usoni, Gazeti JAMHURI limeamua kuchapisha hotuba hii neno kwa neno kama sehemu ya kuweka kumbukumbu na kuwapa fursa Watanzania, ambao hawakupata nafasi ya kuisikiliza hotuba hii, kuisoma na wao pia kuhifadhi kumbukumbu. Endelea…

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons