Siasa

Yah:  Uongozi sasa ni kama kazi na siyo karama, uwezo

Juzi jioni, mtoto wangu wa mwisho nilisikia anataka kugombea udiwani uchaguzi ujao, nikamuuliza maswali machache na aliweza kuyajibu kwa ufasaha.  Nikajua kweli huyu mtoto kawa mwanasiasa mkomavu katika umri mdogo. Nilipomuuliza sababu za kutokugombea katika uchaguzi uliopita, alijitetea kuwa umri wake ulikuwa haujatimia. Wakati wa maisha yetu ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea masuala ya uongozi yalikuwa ni karama na ...

Read More »

Kangi Lugola ameeleweka

Mgonjwa afikapo kwa tabibu – iwe wa kienyeji, tiba za asili au wa kisasa – hakurupukiwi kupewa dawa.   Mtaalamu wetu wa jadi atapiga ramli kubaini chanzo cha kuumwa na upande wa yule wa tiba za kisasa atautanguliza uwezo wake mkubwa wa kusikiliza vyema kwa muktadha wa kiitwacho ‘doctor-patient relationship’ ili kuweza kumtibu mgonjwa wake bila mawaa. Nimeanza na maneno haya katika ...

Read More »

Wingi wa watu: Athari, faida zake

Uzazi wa mpango umekosolewa na baadhi ya watu kuwa ni njama za nchi za Magharibi ambazo zinakabiliwa na tatizo la, ama kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa, au kuwa na familia ambazo hazina watoto kabisa. Kwa upande mmoja wingi wa watu ni suala linaloweza kuipa nchi nguvu dhidi ya nchi nyingine. Kwa mantiki hiyo, kushawishi nchi zinazoendelea kupunguza kasi ya ...

Read More »

Punguzo jipya la kodi, tozo, ada za ardhi

Hivi karibuni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipowasilisha hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka fedha 2015/16 mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizungumzia mambo mengi ambayo ni muhimu kwa mdau au mmiliki yeyote wa ardhi kuyafahamu. Kati ya mambo muhimu aliyozungumza, mawili yaligusa hisia za wengi. Kwanza ni ...

Read More »

CCM iruhusu ushindani wa haki urais

Kwa wiki takribani nne hivi, sijaonekana katika safu hii. Sikuonekana kutokana na matatizo ya msiba, lakini pia nikalazimika kufanya kazi mikoani. Huku niliko nakumbana na tunachopaswa kupambana kukiondosha. Sehemu nyingi za mikoani hakuna huduma ya data (Internet), simu zipo ila ukitaka kuingia kwenye Internet ili utume barua pepe ni sawa na kushuka mchongoma. Yapo baadhi ya maeneo kuna mtandao, lakini ...

Read More »

Nini kimewachochea wasaka urais ?

Mara baada ya ratiba ya ndani ya CCM kutolewa, kumekuwapo na mfumuko wa wagombea waliojitokeza kuchukua na kurudisha fomu ya kuwania urais.     Swali la kujiuliza ni je, utitiri huu umechochewa na nini? Hoja hii ni mtambuka ambayo inagusa maeneo mengi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hata hivyo, nitajaribu kubainisha baadhi ya mambo muhimu ninayohisi yamechangia wagombea wengi kujitokeza hadi kufikia 30 ...

Read More »

Tunamhitaji Rais Mtendaji Mahiri, Jasiri

Wanaowania urais wa Awamu ya Tano Tanzania, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), walianza kuchukua fomu mjini Dodoma Jumatano Juni 3, 2015. Inaonekana wengine waliokuwa wanatajwatajwa, wanasita, hawajajitokeza kugombea, hawajachukua fomu! Labda watajitokeza baadaye, au wanaona hawana nafasi nzuri. Lakini jambo la kusikitisha ni ile hali ya kupakana matope iliyojitokeza wakati baadhi wagombea hao watarajiwa, walipokuwa wanatangaza nia. Badala ...

Read More »

Adui wa Tanzania yupo Tanzania

Mwandishi wa Gazeti la JAMHURI, Manyerere Jackton, katika makala yake iliyokuwa na kichwa cha habari, ‘Kutokufanya kitu nako ni kufanya kitu’, toleo Na. 190 aliandika hivi, ‘Ukiyatafakari mengi yanayolikabili Taifa letu, hata kama ulikuwa na nia ya kugombea urais, unaweza kughairi.’ Kwanza niseme kabisa kwamba maneno haya ya Manyerere si ya kuwakatisha tamaa wanaowania nafasi ya urais. Ni angalizo kwa rais ...

Read More »

Hii ni vurugu ndani ya CCM – Msuya

Waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, Cleopa David Msuya, anaamini kwamba Uchaguzi Mkuu wa tano baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, utafanyika Oktoba kama ulivyopangwa. Bosi huyo wa nchi aliyeshika wadhifa huo uliokwenda sambamba na umakamu wa rais kwa vipindi tofauti vya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na Ali Hassan Mwinyi, anasema: “Rais Jakaya Kikwete ataondoka ...

Read More »

Vijana wapewe nafasi Uchaguzi Mkuu (1)

Nchi imekuwa katika hali ya wasiwasi na ya sintofahamu juu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Aidha, pamekuwapo minong’ono au ati kuwa huenda uchaguzi usifanyike mwaka huu wa 2015. Huko nyuma kama tunakumbuka Waziri Mkuu aliwahi kusema bungeni kuwa Uchaguzi Mkuu mwaka huu upo kama ilivyopangwa. Mheshimiwa Rais wa Jamhuri akiwa katika sherehe za kilele cha Siku ya Wafanyakazi (Mei ...

Read More »

Pinda angepumzika tu

Miaka kadhaa iliyopita, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwaita wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake, Dar es Salaam. Akazungumza mambo mengi. Nilipata bahati ya kualikwa, na ya kumuuliza swali. Swali langu, ukiacha ule mgogoro alioshindwa kuutatua- mgogoro wa ardhi Kwembe-Kati, lilihusu ukwasi alionao. Akatoa maelezo marefu kwa kusema ana nyumba za kawaida- Pugu, Dar es Salaam na Kibaoni, Katavi. Kwenye ...

Read More »

Yah: Kuna koo za uongozi, koo za biashara

Nakumbuka zamani wakati wa machifu, waliokuwa viongozi wetu wa kijadi, walikuwa wanamiliki mashamba kidogo, wake kidogo, na mali ya jamii inayowazunguka. Mali iliyomilikiwa na chifu na ambayo kimsingi ilikuwa ya jamii ni pamoja na mashamba, chakula, busara, na uamuzi mzito wa jamii husika. Nchi hii wakati tunautafuta uhuru, tuliheshimu utawala wa kijadi, yaani machifu waliokuwapo na waliotangulia mbele ya haki. ...

Read More »

Miaka 39 imetimu, tuendelee kuomboleza mauaji Soweto

Leo ni Juni 16, 2015. Tarehe kama hii mwaka 1976 katika mji wa Soweto nchini Afrika Kusini, watoto wa shule wapatao 600 waliuawa na utawala wa Wazungu (makaburu) kwa kumiminiwa risasi za moto wakiwa katika maandamano ya amani kupinga mtaala mpya na lugha ya Afrikaan kutumika katika kufundishia. Kwanza naomba nieleze sababu zilizonishawishi kushika kalamu na kuandika kwa ufupi tukio hilo la ...

Read More »

Siasa zinaishia getini

Moja ya majukumu yangu nikiwa Butiama ni usimamizi wa kutangaza Kijiji cha Butiama kama kivutio cha utalii ndani ya programu ya Utalii wa Utamaduni inayoratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania. Butiama inajumuisha vivutio vya utalii vya aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vile vya utamaduni wa kabila la Wazanaki, vivutio vya mazingira, na – pengine muhimu kwa wageni wengi – ...

Read More »

Ada ya kutafuta hati ya nyumba, kiwanja

Watu wengi wanaonunua ardhi wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa katika kubadili majina yaani kutoka mmiliki wa mwanzo kwenda kwa mmiliki mpya aliyenunua. Upo usumbufu ambao husababishwa kwa makusudi na maafisa wanaohusika, lakini pia upo usumbufu ambao husababishwa na watu wenyewe wanaotaka kubadili majina. Wengi huanza muamala huu bila kuwa na taarifa kamili za nini kinahitajika kwa maana ya nyaraka, ikiwamo ada ...

Read More »

Msuya asisitiza: Kila mtu atabeba msalaba wake

Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa David Msuya, amesema ajenda kuu ya sasa kwa Mtanzania ni kupata elimu bora, lakini anasikitika kuona Rais Jakaya Kikwete akidanganywa, naye anakubali kudanganyika. Pia amesema hajutii kauli yake aliyoitoa akiwa Waziri wa Fedha kuwa “Kila mtu atabeba msalaba wake.” Katika mwendelezo wa mahojiano na kiongozi huyo yaliyoanza kuchapishwa wiki iliyopita, Msuya ambaye pia alikuwa Makamu wa ...

Read More »

Nilivyomfahamu Brigedia Jenerali Hashim Mbita (3)

Wakati Mbita anaanza kazi katika Kamati ile ya Ukombozi, dunia iligawanyika katika pande mbili ki-mawazo na mitazamo. Hii kisiasa tuliita enzi za vita baridi kati ya mataifa ya Ulaya (upande wa Magharibi na upande wa Mashariki). Hili nalo lilileta changamoto ya aina yake miongoni mwa wapigania ukombozi katika Bara la Afrika. Vilikuwapo vishawishi vikubwa tu. Hapo kiongozi asiyekuwa mwadilifu angeweza ...

Read More »

CCM tunayoiona ni uhunzi wa Kikwete

Kuna ule msemo wa “vita ya panzi, furaha ya kunguru”. Vyama vya siasa vya upinzani, kama kweli vina dhamira ya dhati ya kupata uhalali kutoka kwa Watanzania, mwaka huu wa 2015 ni mwaka sahihi kabisa wa kutimiza azma hiyo. Endapo vyama hivyo, kupitia umoja wao wa Ukawa vitashindwa kutumia fursa hii, basi huenda Watanzania wakaendelea kushuhudia miaka mingine mingi ya ...

Read More »

Yah:  Sasa ni mwendo wa msoto kutafuta kula, si kura

Najuta kuzaliwa maskini na katika familia ya ukulima, ningelipenda nizaliwe katika familia ya uanasiasa au ufanyabiashara, na kuwa na nafasi ya kuweza  kuwa na maisha bora kama ilivyo kwa familia hizo nyingi pasi na familia zetu za wakulima. Napenda kuwa  tajiri, tajiri wa mali na si moyo, tajiri wa kujilimbikizia mimi lakini si wao, tajiri wa kurithi na kurithisha lakini ...

Read More »

Msumbiji, Tanzania tuenzi undugu wetu

Msumbiji na Tanzania, ukweli ni nchi ndugu tangu zama. Msumbiji tangu hizo zama ni sumbiji. Tanzania ni nchi mpya iliyoundwa kutokana na nchi mbili huru, Tanganyika na Zanzibar. Katika ukweli huo nchi hizo ndizo hasa ndugu wa Msumbiji. Ndipo ninapothubutu kusema Msumbiji na Tanzania ni ndugu tangu enzi na enzi. Ingawa kwa miaka ipatayo mia tano Msumbiji ilitawaliwa na ukoloni ...

Read More »

Raia kukataa kukamatwa taratibu zikikiukwa

Siku zote wananchi wamekuwa wakililalamikia Jeshi la Polisi kwa namna linavyoendesha shughuli zake hasa wakati wa ukamataji (arresting). Matumizi ya nguvu, ubabe na kutofuata sheria na utaratibu maalum vimekuwa ndiyo tatizo kubwa kwa wananchi dhidi ya askari. Siyo siri, askari wamekuwa wakitumia nguvu na ubabe mno katika kukamata raia. Hata pale pasipo na haja yoyote ya kutumia nguvu, bado wao ...

Read More »

Dhana ya Demokrasia yetu inakumbana na changamoto

Pamoja na hatua zilizofikiwa kukuza demokrasia chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, bado ziko changamoto zinazoathiri hali ya kukua na kushamiri kwa demokrasia nchini. Ile tafsiri asilia ya demokrasia inasema hivi: Serikali inayoongozwa na watu. Aidha ni aina ile ya serikali ambayo hatamu juu yake imo mikononi mwa watu, na uwezo huo unatekelezwa au moja kwa moja nao ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons