Siasa

Nenda Sophia Yamola, nenda mpekenyuzi ukidai haki yako

Katika kipindi cha wiki moja, tasnia ya habari imepata pigo kubwa kwa kuwapoteza wapiganaji wake wawilikatika tasnia hii. Kwanza alikuwa ni Samwel Chamulomo, aliyekuwa Mtangazaji wa TBC Kanda ya Kati, mauti yalipomkuta akiwa mkoani Dodoma. Pili ni Sophia Yamola, mwandishi wa habari za siasa na uchunguzi, aliyefariki Mei 21, mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Kijeshi Lugalo, Dar es Salaam. ...

Read More »

Tumelogwa kuwa wanafiki

Awamu ya kwanza ya harambee ya ujenzi wa kituo cha yatima, shule ya sekondari na msikiti Patandi, Arumeru mkoani Arusha, imefana kwa kiwango kikubwa na kuwa miongoni mwa vielelezo muhimu vya kuuendeleza umoja na mshikamano wa Watanzania bila ya kujali madhehebu, rangi na dini. Hamasa iliyojitokeza katika viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa jijini Arusha, imenikumbusha moja ya mafunzo makuu ...

Read More »

Hatma ya Tanzania iko kwa Jaji Lubuva

Waliosoma maandishi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Jaji Mark Bomani, watakubaliana na mawazo yake. Hoja yake kuu ni kwamba Katiba mpya katika mazingira ya sasa ya nchi yetu, haiwezekani. Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa kutumia Katiba mpya. Jaji Bomani, mtu mzoefu wa shughuli za Serikali, anashauri Katiba ya sasa iendelee kutumika, lakini ...

Read More »

Yah: Laana yangu kwa hawa, baraka kwa wale

Sasa niseme rasmi kuwa mimi nakubali siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kuwa nguzo yetu ya kujitegemea na kututoa hapa tulipo na kutupeleka katika nchi ya ahadi ya kunywa maziwa na asali, nchi ya ahadi ya Eden ambayo kwa hakika ndiyo iliyokuwa Tanzania ya miaka ya 1970.  Nalaani kwa nguvu zangu zote kufuta Azimio la Arusha, nalaani wote walioshiriki kukataa Azimio ...

Read More »

Salaam wafanyakazi wote

Itakumbukwa katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei mosi mwaka huu, iliyofanyika kitaifa Uwanja wa Michezo CCM Kirumba, Mwanza, yalionekana na kusikika mambo mengi ikiwamo michezo, ngoma na nyimbo zilizosifu na kushauri utendaji bora wa kazi na kudumisha nidhamu ya kazi. Mabango yalibeba ujumbe tofauti ukiwamo wa “utani” na ukweli kwa viongozi wa nchi pamoja na salamu za wafanyakazi kwa ...

Read More »

CCM ina nia mbaya kwa makada wake?

Baada ya danadana ya muda mrefu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoendelea kukwamisha kumtangaza mgombea wao wa urais, sasa naamua kusema. Hii ni kwa sababu ni mwanachama wa kawaida na sina nafasi ndani ya vikao vya Kamati Kuu wala Halmashauri Kuu. Nimeona hivi kwa sababu hata ikitengenezwa mizengwe na majungu ya kila namna, bila ya kumsimamisha Edward Lowassa au Bernard ...

Read More »

Sababu nne za ushahidi wa kuambiwa haukubaliki kortini

Ushahidi wa kuambiwa ni nini? Ushahidi wa kuambiwa ni ule unaotolewa na mtu ambaye hakuona tukio likitendeka, hakusikia tukio likitendeka, hakuhisi wala kuonja, wala kunusa jambo lililo mbele ya Mahakama kama kosa isipokuwa aliambiwa na mtu mwingine aliyeona, kusikia, kuhisi, kunusa au kuonja. Hapa kuna watu wawili – kwanza aliyeona au kusikia na pili yule aliyeambiwa na huyu aliyeona au ...

Read More »

Mila za Wazanaki: Mwitongo na Muhunda

Baada ya makala ya juma lililopita juu ya lugha ya Kizanaki, naendeleza makala inayofafanua mila na tamaduni za kabila la Wazanaki. Eneo la Butiama linalojulikana kama “Mwitongo” linatokana na neno la Kizanaki lenye kumaanisha “mahame”, eneo ambalo lilikuwa na wakazi ambao walihamia sehemu nyingine. Kwa desturi chanzo kikuu kilichosababisha watu kuhama eneo moja kilikuwa kifo cha mkuu wa kaya na ...

Read More »

JK iwezeshe NEC, ikifika Oktoba uende Msoga

Imenichukua takribani wiki mbili kutafakari kauli ya Mwenyekiti wa NLD, Dk. Emmanuel Makaidi, ambaye ni miongoni mwa wenyekiti wenza wa vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).   Katika mkutano na waandishi wa habari, Dk Makaidi akiwa na wenzake, alidai kwamba “Oooh kuna mipango ya kumfanya Rais Kikwete akae madarakani mpaka mwaka 2017.” Kwa umri wake, Dk. ...

Read More »

Wachina wamkunja Meya Dar

Kampuni ya Ujenzi ya Tanpile Ltd ya China inalalamikiwa na wananchi waishio katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa uchafuzi wa mazingira na kelele usiku kucha, zinazosababisha washindwe kupumzika, JAMHURI inaripoti. Kampuni hiyo licha ya kupewa amri ya Mahakama (stop order) kusitisha shughuli zake za uchanganyaji wa zege katika kiwanda chake kilichofunguliwa katika makutano ya barabara za Samora, Aggrey ...

Read More »

Jimbo la Kiteto lawaniwa na watano

Jumla ya watu watano wametajwa kuwania Jimbo la Kiteto lililopo mkoani Manyara, kumrithi Mbunge Benedict ole Nangoro (CCM), anayemaliza muda wake mwaka huu. Waliotajwa kutaka kuingia katika kinyang’anyiro hicho ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Emmanuel Papian, Amina Saidi Mrisho (CCM), anayefanya kazi Tume ya Takwimu Taifa, Jonathan Kilani, mwanachama kutoka Chadema, na Goodluck Mmari (CCM) na Mashaka ...

Read More »

Ukimya wetu kwa CCM hii, unatosha

Mara baada ya kusoma makala hii, bila shaka utabaki kwenye akili ya mmoja wa wanafalsafa wa Uingereza aliyeitwa Francis Bacon (1561-1626). Alipata kunena kwamba “Anayeuliza mengi atajifunza mengi, na kubaki na mengi.”   Hii maana yake ni kwamba hakuna mtu mjinga kuliko mwingine, na hakuna mtu mwerevu kuliko mwingine. Binadamu wote wana mwanga pia wana giza. Hivyo suala la kujiuliza ...

Read More »

Brig. Jenerali Mbitta aipa siri JAMHURI

Wiki mbili tangu kufariki na kuzikwa kwa Brigedia Jenerali Hashim Idd Mbitta, gazeti la JAMHURI limeibuka na makala ya mwisho aliyofanya mpiganaji huyo na aliyekuwa mwandishi wa mwandamizi wa gazeti hili, EDMUND MIHALE.  Katika mahojiano hayo yaliyofanyika Desemba 2013, Mhariri anakuletea neno kwa neno kwa wakati ule alipozungumza na gazeti hili akianzia kusema kazi ya ukombozi ya Bara la Afrika ...

Read More »

Yah: Naipenda Tz ya wajinga wengi

Kuna wakati huwa najiuliza, hivi ni kweli kwamba ngozi nyeusi ni alama ya laana au mkosi? Sipati jibu kwa kuwa wapo ambao wana ngozi nyeusi na hawakumbwi na laana hiyo, lakini pia huwa najiuliza, ni kweli kwamba kutawaliwa ni dalili ya kuwa wajinga?   Napo pia jibu huwa ni hapana kwa kuwa ni sisi wachache tulioonja utumwa na bado tukadai ...

Read More »

Tunajivunia miaka 51 ya Muungano wa Tanzania

Jumapili iliyopita ya Aprili 26, Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar ulitimiza miaka 51 tangu ulipoasisiwa mwaka 1964 na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, na hatimaye kuungwa mkono na wananchi wa nchi hizo mbili. Muungano huo wa Jamhuri ya Tanzania, hadi kufikia ...

Read More »

Kumshitaki kwa jinai aliyevamia ardhi yako

Katika migogoro ya ardhi, yapo mambo mengi ambayo hujitokeza. Yumkini hii yote huwa ni katika kusaka haki.  Liko jambo moja ambalo ni muhimu watu kulijua hasa wale ambao tayari wamejikuta katika migogoro ya ardhi.  Mara nyingi imekuwa ikitokea pale mtu fulani ana mgogoro wa ardhi na mtu mwingine kumwendea polisi na kumshitaki kwa jinai ya kuvamia ardhi yake (criminal trespass). ...

Read More »

Kuchanganya lugha ni changamoto endelevu

Watanzania wengi wanaozungumza Kiswahili na waliojaaliwa kupata kiasi fulani cha elimu, huugua ugonjwa ambao moja ya dalili zake ni kuongea au kuandika kwa kutumia zaidi ya lugha moja. Na kwa kawaida, lugha ya pili huwa ni Kiingereza.   Akifunga Mkutano wa Bunge Septemba 8, 2004, Waziri Mkuu Frederick Sumaye alizungumzia tatizo hili na athari zinazojitokeza za kuzivuruga lugha zote mbili ...

Read More »

Nape asimamia msimamo Panga CCM liko palepale

Na Angela Kiwia   Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, anasema kwamba kada yeyote atakayepatikana na hatia ya kukiuka maagizo au taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), atachujwa tu.   Kadhalika, amesema kwamba kwa watakaokatwa majina, wakatathmini na kuona kuwa hawakutendewa haki, wanaruhusiwa kuondoka kuhamia vyama vingine au kuacha siasa.  “Siku zote nimekuwa nikisema na ...

Read More »

CCM ni ya kuzikwa tu Oktoba 2015

Watanzania, mabadiliko ni leo si kesho; mabadiliko ni wiki hii si wiki ijayo; ni mwezi huu si ujao, mabadiliko ni mwaka huu si mwakani. Kesho hujaiona na hujui itakuaje, lakini uamuzi wako wa leo unaweza kuharibu kesho yako au unaweza kujenga kesho yako. Jenga leo yako vizuri ili kesho yako iwe nzuri. Ninawahamasisha Watanzania wa kada zote — wanaume kwa ...

Read More »

JAMHURI latikisa tuzo za Ejat

Waandishi wa habari wa Gazeti la JAMHURI, Deodatus Balile na Victor Bariety, mwishoni mwa wiki iliyopita walijinyakulia tuzo za umahiri wa uandishi wa habari nchini (EJAT), zinazotolewa kila mwaka na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Balile aliongoza katika kundi la wazi ambalo hushindaniwa na kazi yoyote iliyofanywa vyema wakati Bariety alishika nafasi ya pili katika habari za Utawala Bora akizidiwa ...

Read More »

Mpinzani gani hana vinasaba vya CCM?

Weledi wa Sayansi ya Siasa wanaitambulisha siasa kuwa ni mfumo wa maridhiano unaohusisha kikundi cha watu walioafikiana kuwa na uamuzi wa pamoja (politics involves the making of a common decision for a group of people).  Kadhalika, uamuzi wa aina hiyo unahusisha wanachama wote wa kikundi hicho bila kubaguana. Na kwamba ili kikundi cha siasa kiweze kujitosheleza kiuamuzi, ni lazima kitayarishe ...

Read More »

Magari mengi nchini ni utajiri au ulofa?

Kwa muda mrefu sasa nina dukuduku la kuuliza Wanatanzania wenzangu hasa wale wachumi waliobobea kama akina Profesa Ibrahim Lipumba au Profesa Simon Mbilinyi vile.   Suali langu; ni vigezo gani katika Taifa linaloendelea vinaonesha kukua kwa uchumi katika Taifa?   Wako wachumi wengi hapa nchini lakini hapa nimewataja hawa maprofesa wawili kwa vile kila mmoja kwa muda fulani aliwahi kuwa ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons