Makala

Ubakaji na utelekezaji wa watoto

Kuna jambo ambalo limezungumziwa bungeni na kunifanya nihisi furaha iliyopitiliza. Jambo hilo ni kwamba wanandugu ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kosa la watu kuwabaka hata dada zao na wakati mwingine binti zao, pia kuwatelekeza watoto wanaotokana na unyama huo wa hatari! Itakuwa ni jamii ya aina gani tuliyomo tunapoyaacha majanga ya aina hiyo yaendelee kutamalaki ndani yake! Tulizoea kusema haya ...

Read More »

Mwanadamu na fikra zake 

Mwanadamu ana uwezo wa kufikiri na kuamua kutenda jambo zuri au baya. Anaweza kujifanyia haya binafsi, kuwafanyia wanadamu wenzake na viumbe vyote vilivyomo katika ulimwengu huu, kwa nia tu ya kuridhisha nafsi yake. Na hapa ndipo yanapoanzia maelewano na mifarakano baina ya wanadamu. Uwezo alionao mwanadamu huyu unampa kiburi kutii au kutotii jambo, kukiuka kanuni na taratibu alizojiwekea na zile ...

Read More »

Yah: Dunia inakwenda kasi, naomba nishuke

Naanza na salamu kama ilivyo kawaida yangu, naamini huo ni moja ya uzalendo ambao tumekuwa nao kama watoto wa Tanganyika mpaka ikawa Tanzania huru. Salamu inakufanya umtambue mzalendo mwenzako na kumtambua kama yuko salama na uko mikono salama kama mmekutana barabarani. Nakumbuka enzi hizo tukihisi tu kama si mwenzetu kwa hatua ya salamu tu, tunaanza kwa kukuomba barua ya mwenyekiti ...

Read More »

Tuoteshe miti ya asili

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema. Ni jambo la kushukuru sana. Wakati tulipopata uhuru mwaka 1961 nchi yetu iliitwa Tanganyika, lakini baada ya kuungana na Zanzibar Aprili 26, 1964 ikajulikana kama Tanzania. Kabla ya utawala wa Waingereza eneo la Afrika Mashariki, zikiwamo Burundi, Rwanda, Tanzania Bara na Buganda; kuanzia mwaka 1885 hadi mwaka 1919 yalikuwa chini ya utawala wa ...

Read More »

Jinsi ya kuanzisha biashara Tanzania (8)

Wiki iliyopita niliahidi kujibu maswali haya: “Je, unafahamu utaratibu wa kisheria wa kusajili Jina la Biashara, gharama ya usajili, muda wa kukamilisha usajili, nyaraka zinazotakiwa, umri wa mtu anayetaka kusajili Jina la Biashara na matakwa mengine ya kisheria? Usikose nakala yako ya Gazeti hili makini la uchunguzi la JAMHURI Jumanne ijayo.” Sitanii, baada ya makala hii, nimepata maombi mengi. Nimepata ...

Read More »

Ujira wa wafunga maturubai malori ya makaa ya mawe matatani

Vibarua wa kufunga maturubai mizigo ya makaa ya mawe kwenye malori wamevurugana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri hiyo kujitwalia mamlaka ya kutunza fedha zao katika akaunti ya halmashauri. Kwa mujibu wa vibarua hao kutoka Kata ya Amanimakolo, wilayani Mbinga, ili kulipwa stahili zao ni lazima kwanza kipatikane kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na zaidi ...

Read More »

TIC, halmashauri kuvutia wawekezaji

Utekelezaji wa sera ya taifa inayoelekeza halmashauri zote nchini kutenga rasmi maeneo maalumu ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji katika kila halmashauri nchini bado unasuasua na kusababisha kero kwa wawekezaji wa nje na ndani. Sera hii ilikusudia kurahisisha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wawekezaji, kwa mkakati wa kupunguza usumbufu na  kuchelewa kupata hatimiliki kwa kutumia utaratibu wa kawaida. Serikali ...

Read More »

Maswali ni mengi hukumu ya kifo kwa Mwalimu Respicius

Siku niliposikia Mahakama Kuu (Bukoba) imetoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa Mwalimu Respicius Patrick kwa kosa la kumuua mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibeta, Sperius Eradius, niliduwaa. Katika kuduwaa, nilianza kutafakari juu ya ndoto yangu hii ya kuwa mwalimu niliyoipigania kwa nguvu zote, kwa uwezo wa Mungu, na hatimaye kufanikiwa. Ni kwamba nikiwa mwanafunzi ndoto ya kuwa mwalimu au ...

Read More »

Ndugu Rais, kati ya nguo na pasi kipi kinapigwa pasi?

Ndugu Rais, tunasoma katika kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu kuwa: “Wananchi wanataka rais awathamini raia waandamizi waliokamilisha wajibu wao na kustaafu katika ujenzi wa taifa ili wasipate shida katika wakati wao wa kutokuwa na nguvu za kuendelea kujikimu. Hivi sasa wastaafu wanaishi katika uchochole wa kutisha. Pensheni yao ni ya kijungujiko.” Tukiwa katika uelewa huu, naona ni vema nikufikishie ...

Read More »

Wanasiasa si wenzetu

Wanasiasa siyo wenzetu kwa maana nyingi tu, na siyo kwa sababu tu ya kuitwa waheshimiwa. Kwanza, ni watu wenye kujiamini, wenye imani inayoambatana na uwezo mkubwa wa kusikia maoni tofauti kabisa na ya kwao, lakini wakaendelea kushikilia msimamo kuwa wanachofanya ni sahihi, na kuamini kuwa malengo yao ndiyo muhimu zaidi. Utampambanua mwanasiasa kwa ubishi. Ubishi si jambo baya kama kusudio ...

Read More »

Epuka kuishi maisha ya majivuno

Majivuno yaliwabadili malaika wakawa mashetani. Unyenyekevu huwafanya watu wawe kama malaika – Mt. Augustino. Kitendawili: Tega! ‘Ananifanya nichukiwe na kila mtu’. Jibu ni ‘majivuno’. Kitendawili: Tega! ‘Nikimmeza najisikia sana’. Jibu ni ‘majivuno’. Majivuno ni jeraha lisiloponyeka katika maisha. Majivuno ni jeraha linalonuka kama mzoga wa porini. Ni donda ndugu. Majivuno ni dereva wa shetani. Mwaka 2013, Jarida la ‘New People’ ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (23)

Kataa kujikataa Kukataa kujikataa ni mtihani. Kujikataa ni kujihisi wewe si mtu muhimu. Ukweli wewe ni mtu muhimu. “Kukosa kitu cha kukufanya ujisikie wewe ni mtu muhimu ni jambo liletalo huzuni mkubwa sana, ambalo mtu anaweza kuwa nalo,” alisema Arthur E. Morgan. Kumbuka wewe si bahati mbaya. Wewe ni wewe. Hakuna ‘spea’ kwa ajili yako. Uliletwa duniani kwa lengo maalumu. ...

Read More »

Hongera Ridhiwani, umeonyesha njia

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amefanya jambo lenye manufaa makubwa kwa wanafunzi wa kike jimboni mwake na kwa taifa. Amesimamia ujenzi wa mabweni ya wasichana katika Shule ya Sekondari Mboga, iliyopo Kata ya Msoga mkoani Pwani. Amesukumwa na azima yake ya kuona mtoto wa kike anasoma kwa bidii katika mazingira mazuri ili afikie ndoto alizojiwekea. Tumeambiwa kuwa mabweni hayo yatahifadhi ...

Read More »

Ushabiki na ushabaki havitangamani

Shabiki na shabaki ni kama watoto wawili pacha. Ukikutana na shabiki utawaza umekutana na shabaki, na ukikutana na shabaki utaona umekutana na shabiki. Kumbe sivyo. Ni watu wawili wenye hulka na tabia tofauti. Wa kwanza ni mkweli na wa pili ni mwongo. Ushabiki ni hulka ya mtu kupenda sana kitu fulani. Ushabaki ni tabia ya kupenda fujo, ugomvi au mzozo. ...

Read More »

Yah: Mheshimiwa Rais, bado kuna mambo mengi

Salamu zangu ni za kawaida kwa sababu kwanza naamini katika upendo; pili, naamini katika undugu; Watanzania wote ni kitu kimoja na ni ndugu, tunapaswa kupendana sana. Upendo tutakaokuwa nao ndio utakaotufanya tuwe na mshikamano na hatimaye tutavuka hili tuta kubwa na lenye majaribu makubwa ya kufikia malengo ya maendeleo. Huwa nakufuatilia sana, hasa pale unapoonyesha katika uso wako kwamba kuna ...

Read More »

NINA NDOTO (12)

Ongeza thamani kwa ukifanyacho Mchezaji bora katika timu si yule mwenye umri mkubwa zaidi ya wachezaji wengine au aliyeitumikia timu kwa muda mrefu, bali ni yule mwenye thamani.  Ndiye hulipwa zaidi ya wote. Thamani ni gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake kwenye jamii.  Kila  unachokifanya kitakulipa kuendana na thamani unayoitoa. Ukiwa kazini usifikiri kwamba unalipwa ...

Read More »

Hofu ya Chadema sheria mpya ya vyama vya siasa

Katika taarifa kwa umma, Machi 22, 2019, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefanya uchambuzi wa sheria mpya ya vyama vya siasa iliyotiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kama ifuatavyo: Tumeiona Sheria mpya ya Vyama vya Siasa ambayo imesainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, Februari 13, 2019 na kuchapwa ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (22)

Hatuoni ingawa tunatazama Kuona ni mtihani. Si kila jicho lililofunguka linaona. Na si kila jicho lililofumbwa limelala. Kila mtu anatazama lakini si kila mtu anaona. Kuona ni mtihani. Je, unapotazama unaona? “Hatuoni vitu kama vilivyo, tunaviona kama tulivyo.” (Anais Nin). Kwa msingi huo, kuona ni mtihani. Mfinyanzi atauona udongo kama kitu cha kumsaidia kutengeneza vyungu, kutegemea fani yake. Mkulima atauona ...

Read More »

Ndugu Rais, Jaji Mkuu Samatta ametoa tamko

Ndugu Rais, ndivyo alivyo Mwenyezi Mungu; huwatuma watu wake wema walio kati ya watu wake kuwafikishia ujumbe watu wake walio kati yao. Wenye masikio ya kusikia husikia, bali wenye viburi Bwana huwaadhibu kwa mwisho wao wa aibu. Nukuu katika kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu inasomeka kuwa Bwana Mageuzi alisema madhara yangekuwa makubwa zaidi kama si kwa ubunifu na busara ...

Read More »

Rais Magufuli wasaidie wanyonge hawa

Jumamosi iliyopita nilikuwa jijini Arusha. Nikiwa nimeegesha gari kwa ajili ya kupokea simu, nikamwona mama aliyeonekana mwenye mawazo mengi. Hakuwa na furaha usoni. Hapa ni jirani na Uwanja wa Ndege wa Kisongo. Sikuhitaji kumuuliza maswali mengi. Nilichofanya baada ya kumtazama, nilimwita. Akasogea akionekana mwenye shaka nyingi. Nilimuuliza anakokwenda. Akajibu kuwa anakwenda Soko la Kilombero ambako anauza mbogamboga. Kwa namna nilivyomwona ...

Read More »

Mgeni mpe mchele na panza

Mgeni ni mtu aliyetembelea eneo fulani kwa mara ya kwanza. Ni mtu anayepewa dhamana ya kuwa mtu muhimu, na aghalabu hupewa jukumu la kutekeleza shughuli rasmi inayofanyika. Mgeni ni mtu asiye na uelewa wa kutosha au ueledi katika fani fulani. Tunaweza kusema ni mwanagenzi. Mimi na wewe tunamfahamu mgeni anavyopewa heshima, thamani na huba wakati wa mapokezi na mwenyeji wake. ...

Read More »

Yah: Tunabadilika kwa kasi

Nianze na salamu kama mtu muungwana, maana itakuwa si busara kukurupuka na mawazo yangu kichwani bila kuwajulia hali. Najua kuwa si kila mtu yuko sawa kichwani, hasa katika kipindi hiki cha mpito wa mabadiliko ya mambo mengi, hasa yale yahusuyo mifuko yenu, natoa pole. Salamu zangu zingine, tena za kipekee kabisa nazituma kwa wale ambao hawajatetereka katika kipindi hiki cha ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons