Makala

Je, kesi haiendelei kwa kukataa kupokea ‘summons’?

Summons ni wito maalumu wa mahakama. Mara zote unapofunguliwa mashitaka (unaposhitakiwa) hasa mashitaka ya  madai, basi ili uweze kufika mahakamani na kujua mashitaka yanayokukabili yaipasa mahakama kutuma wito maalumu  ambao kwa jina la kitaalamu huitwa ‘summons’. Mara nyingi wito huu unapotumwa baadhi ya watu hukataa kabisa kuupokea na wengine huupokea lakini hukataa  kuusaini.  Zipo sababu tatu ambazo huwafanya watu wasipokee ...

Read More »

Palipo na upendo kuna maisha (2)

Ulimwengu wa leo unahitaji kuhubiriwa namna mpya ya kuishi maisha ya upendo. Ni hatari watu wa ulimwengu kuishi bila upendo. Bila kuishi maisha ya upendo, dunia yetu itageuka kuwa jehanamu. Mungu hutabasamu pale anapoona mwanadamu anaishi maisha ya upendo. Nafsi yako haiwezi kuwa na amani kama haipendi wala kupendwa. Njia bora ya kuishi ni kuishi maisha ya upendo. Namna bora ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (39)

Ukitumia dakika 60 kulalamika, umepoteza saa 1 Kulalamika ni mtihani. Unaweza kulalamika kuwa maua aina ya waridi yana miiba au kusifu kuwa miiba ina maua. Ukitumia dakika sitini ukilalamika, umepoteza saa moja. Kama una muda wa kulalamikia jambo, una muda wa kulitatua. Chukua hatua, ukiua muda ukilalamika muda unaishia kukuua. Chukua hatua, yashughulikie mambo unayoyalalamikia. Tafuta suluhisho. “Usilalamike bali chapa ...

Read More »

Rais Magufuli aandika historia Rufiji

Rais Dk. John Magufuli amezindua rasmi ujenzi wa mradi wa umeme wa maji Mto Rufiji. Mradi huo utakapokamilika utazalisha megawatt 2,115 za umeme. Akizungumza katika uzinduzi huo uliohusisha uwekaji wa jiwe la msingi, Rais Magufuli amesema kufanikishwa  kwa mradi huo ni ukombozi wa Tanzania kiuchumi. Ujenzi wa mradi huo utatekelezwa ndani ya miezi 36 na Sh trilioni 6.5 zote zikiwa ni ...

Read More »

Manabii wa viberenge vya Mlima Kilimanjaro…

Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano wa mwaka unaoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kuwakutanisha wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka pande zote nchini. Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TANAPA wameweka utaratibu huu kwa kutambua kuwa wanahabari wana nafasi ya kipekee kwenye uhifadhi. Kwa kutumia magazeti, majarida, redio, televisheni na mitandao ya ...

Read More »

Istilahi za kisiasa zitumike vema – (2)

Usiku  na  mchana, usalama na utulivu wa nchi unatoweka kwa sababu milio ya risasi na mabomu inarindima. Makazi salama yanavunjwa na miundombinu inabomolewa. Zahanati na vituo vya afya vinapokea majeruhi na wagonjwa wengi kuliko kawaida. Maiti wanazagaa barabarani na hospitalini, maji na vyakula vinapatikana kwa shida, sababu vita ya wananchi wenyewe kwa wenyewe. Baadhi ya nchi duniani zimepata kutumbukia katika madhira ...

Read More »

Yah: Huyu Julius wa Burigi anatafakarisha

Nimelala nikaota njozi mbaya sana kwa kuonyeshwa mtu ambaye namfahamu lakini siye, kuna mtu kasema amka umuangalie Julius yuko mbele yako, nami kwa haraka nikaamka ili nimsimulie tumefikia wapi katika kuenzi yale ambayo alituusia kama taifa. La kwanza kabisa ni kumwambia ile hifadhi ambayo ilikuwa bado haijapandishwa hadhi ndiyo hii tumeipandisha hadhi na leo tunaizindua. Nilipoamka na kukutana na mwalimu ...

Read More »

Gamboshi: Mwisho wa dunia (8)

Wiki iliyopita katika sehemu ya 7 hadithi hii iliishia katika aya inayosema: “Je! Kutabasamu walijifunza wapi? Au unadhani kuna jamii fulani ilitoka huko ilikotoka na kuwafundisha ishara hizi? Jamii zote walijifunza ishara hizo kabla ya lile gharika la zimwi na walipokimbia wakatoka na ishara hizo ambazo zinaendelea hadi leo miongoni mwa jamii zote duniani. Akaniangalia tena kisha akaendelea:” Endelea…  “Masalakulangwa ...

Read More »

Fuvu la Zinj ni zaidi ya tanzanite

Mhadhiri wa Utalii na Mambo Kale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Noel Lwoga; na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla, wanazungumzia ugunduzi wa Zinj miaka 60 iliyopita na faida zake kwa Tanzania, Afrika na ulimwengu. Endelea… Dk. Lwoga: Zinj ni kama tanzanite Zinj ana faida katika makundi matatu ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Zinj ...

Read More »

NINA NDOTO (27)

Weka malengo Ndoto inahitaji malengo. “Ndoto bila malengo ni ndoto tu, vinginevyo utaishia kupata mambo usiyoyategemea, hivyo kuwa na ndoto na kuwa na malengo,” anashauri Denzel Washington. “Malengo ni maono na ndoto vikiwa katika nguo za kazi,” anasema Dave Ramsey. Malengo ndiyo humfanya mtu aweke jitihada ya kutimiza ndoto zake, hivyo kuwa na malengo katika maisha ni jambo la msingi ...

Read More »

Fursa ya kipekee kiuchumi kwako na familia (2)

Mifano ya ujasiriamali yenye uthubutu lakini ikakwamishwa   Mwaka 2004 hadi Mei 2006 nilikuwa nimetumia uwezo wangu wa masoko kusajili dawa ya kiasili ya Dental Formula Power (DFP), ambayo inasaidia kutibu na kukinga meno yasipate magonjwa na kuzuia wazee wabaki na meno yao kinywani yakiwa imara hadi wanaingia kaburini. Basi nikatumia ushawishi kwenye mamlaka za nchi nyingine na Dental Formula ...

Read More »

TPA: Mizigo ya wateja iko salama bandarini

Bandari ya Dar es Salaam ni lango kuu la biashara kwa nchi yetu na nchi zote zinazotumia bandari hiyo. Kutokana na umuhimu wake, bandari inahitaji ulinzi madhubuti na wa kiwango cha hali ya juu.  Kutokana na umuhimu katika nyanja za kiuchumi na kibiashara, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeimarisha na inaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa bandari ikiwemo ...

Read More »

Ndugu Rais waliotutangulia walisema ukimtuma mpumbavu…

Ndugu Rais, yawezekana katika maisha yetu tulishawatuma wapumbavu wengi tu. Kwa maisha yetu ya hapa duniani hao sasa ndio wanaozishikilia funguo za milango ya magereza yetu. Kama kuna pepo na moto baada ya sisi kupita, hao ndio wanaotusafishia njia yetu iendayo Jehanamu. Kuingia katika mji ule itakuwa ni vigumu, sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano. Mpaka Mwenyezi Mungu ...

Read More »

Dawasa: Tunawaletea maji Dar na Pwani

Wakati wizara na taasisi za serikali zikiendelea kupambana kukamilisha matarajio ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020, katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa, Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) inatekeleza miradi mitano mikubwa ambayo imelenga kuwaondolea kero ya maji wakazi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja ...

Read More »

Yapo madhara ya kuiga kila kitu

Binadamu anajiendeleza kwa kujifunza au kuiga kutoka kwa vizazi vilivyotangulia. Haipo jamii itakayojihakikishia maendeleo ya uhakika bila kujifunza kutoka jamii nyingine ilimradi wanajamii wanaafikiana juu ya maana ya maendeleo na yapi yawe ya kuiga ili kujiletea maendeleo. Teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) imeleta mabadiliko na maendeleo makubwa kwa binadamu duniani kote. Sababu moja ya maendeleo haya ni kuunganisha matumizi ...

Read More »

Namna ya kugawa mali za marehemu

Tanzania kuna sheria nne ambazo hutumika kugawa mirathi. Kwanza,  sheria za  kimila; pili,  sheria  za Kiislamu;  tatu, sheria ya urithi ya India ( Indian Succession Act) na nne, sheria ya mirathi ya watu wenye asili ya Asia. Swali la sheria gani kati ya hizo itumike katika kugawa mirathi hutegemea na mambo yafuatayo:  Kwanza, maisha aliyoishi marehemu. Marehemu kama aliishi maisha ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (38)

Malezi ya mama ni mtaji wa watu mashuhuri Umama ni mtihani. Kila nyuma ya mtu mashuhuri kuna mama makini. Mama ni mzaa chema, lakini kila nyuma ya mshika mkia kuna mama mzembe au hakuna mama. “Mungu asingeweza kuwa kila mahali, hivyo aliumba kina mama.” Ni methali ya Wayahudi ikisisitiza umuhimu wa mama. Kina mama ni watengenezaji wa historia, cha kusikitisha ...

Read More »

Asante sana Rais Magufuli

Kwenye safu hii, toleo Na. 391, niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari: “Rais Magufuli wasaidie wanyonge hawa”. Nilichoandika kilihusu mateso yanayowafika maelfu ya Watanzania katika magereza nchini mwetu. Nilianza na kisa cha kweli cha mama mmoja niliyemkuta akitoka kumwangalia mwanae katika mahabusu ya Gereza la Kisongo, Arusha. Mwanae, Gerald Silvanus Sambayuka (23) ni dereva wa bodaboda. Inadaiwa kuwa alikamatwa ...

Read More »

Diaspora wa kwanza duniani walitoka Ngorongoro

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Profesa Audax Mabulla na Meneja Idara ya Urithi wa Utamadani katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) katika Bonde la Olduvai, Mhandisi Joshua Mwanduka; wanazungumzia ugunduzi wa Zinj miaka 60 iliyopita na faida zake kwa Tanzania na ulimwengu. Mhandisi Mwankunda Kuadhimisha miaka 60 tangu alipopatikana Zinj ni nafasi muhimu na adhimu katika ...

Read More »

NINA NDOTO (26)

Nyuma ya pazia   Nyuma ya makala za nina ndoto kuna makala nyingi zilizowahi kuandikwa na hazijawahi kusomwa na mtu yeyote isipokuwa mimi mwandishi. Nyuma ya nyimbo wanazoimba wasanii wengi na tunazisikia zikichezwa redioni na nyingine tumepakua na kuweka katika simu zetu, kuna nyimbo nyingi ambazo ziliimbwa miaka ya nyuma na hatujawahi kuzisikia. Nyuma ya video nyingi za kuchekesha za ...

Read More »

Fursa ya kipekee kiuchumi kwako na familia

Naitwa Dk.  Joseph Kankola Buberwa au Dk. JK Buberwa. Ni Mtanzania mwenye umri wa miaka 50. Ni  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya JKBRS International Co Ltd yenye ofisi zake jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam. Hivi karibuni nimependekezwa kuwa Mwenyekiti wa Muunganikano wa Wana Maono (Visionaries) duniani, tukiwa ni waanzilishi wa chama hiki. Nimekuwa mtu mwenye maono makubwa kuhusu ...

Read More »

Chuo cha Bandari chemchemi ya wataalamu

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na kumiliki bandari nchini, pia inamiliki Chuo cha Bandari (Bandari College) kilichopo katika Wilaya ya Temeke. Chuo hiki ndicho chemchemi au hazina ya kutoa utaalamu au maarifa ya kuwa na uwezo au umahiri wa kuhudumia meli na mizigo, usimamizi wake na utoaji wa huduma zinazohusiana na shughuli za bandari. Historia ya chuo ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons