KIPA wa zamani wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kurejea kucheza tena nchini katika timu yoyote ya Ligi Kuu Bara ikiwemo Yanga kwa kuwa anataka kufika mbali zaidi katika upande wa soka la kulipwa.

Dida ambaye anacheza katika Klabu ya Chuo Kikuu cha Pretoria ‘Tucks FC’ inayo­shiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini, amekuwa akihusishwa kurejea nchini kujiunga na timu yake hiyo ya za­mani ambayo kwa sasa ipo kwenye wakati mgumu wa kiuchumi.

Kipa huyo ambaye yupo nchini ka­tika mapumziko, amekuwa akihusishwa kurejea Yanga ili kuweza kuziba pengo la kipa Mcameroon, Youthe Rostand ambaye ameshindwa kuonyesha ubora uliotara­jiwa.

 Dida amesema kuwa hana mpango wa kurejea kucheza soka Bongo kwa kuwa mipan­go yake ni kuhakikisha anaendelea kucheza nje kwa kupata changamoto mpya.

“Hizo taarifa kwamba Yanga wanataka nirudi, bado sijazipata lakini mashabiki si ndiyo waliokuwa hawatutaki vipi leo watake tu­rudi! Ila siwezi kushangaa kwa sababu mai­sha ya soka yapo hivyo, leo wanawe­za kukuona hufai ila kesho wakakush­angilia.

“Lakini niseme wazi kwa sasa sipo tayari kurejea nyumbani kucheza katika timu yoyote kwa sababu nataka niendelee kucheza nje zaidi ya hapa nilipo na siyo kurudi nilipotoka, hayo ndiyo malengo yangu kwa sasa na siyo vinginevyo,” alisema Dida.

Source: Gazeti la Championi

By Jamhuri