Dk Tulia apokea msaada kwa watoto wenye uhitaji maalumu

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson,akipokea alama ya Tasisi ya Human Relief Foundation kutoka kwa Mkurugenzi wa Human Relief Foundation Sheikh Khalid Butchery.

 

NAIBU Spika Tulia Akson amepokea msaada wa vifaa mbalimbali kutokea kwa Taasis ya Human Relief kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum wa ya Katumba ya mkoani Mbeya.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Tulia alisema, aliitembelea shule hiyo mapema mwezi huu na kusikia changamoto zao mbalimbali.Alisema, shule hiyo ina watoto wenye ulemavu wa Ngozi na ulemavu wa viungo huku wote hao wakikabiliwa na changamoto kadhaa za vifaa vitakavyowawezesha kusoma.

Alisema: “Msaada huu ni muhimu kwa wanafunzi kwa kuwa utawawezesha kujisomea kwa Amani na furaha zaidi, wamekuwa kwenye mazingira magumu ya kujisomea na nilichukua uamuzi wa kuwatafuta hawa wafadhiri ambao nao wameitikia kwa wakati”.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akipokea Msaada wa kofia kwa ajili ya Watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule ya Walemavu Katumba kutoka kwa Mkurugenzi wa Human Relief Found.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Januari 26, 2018 wakati wa hafla ya kupokea Msaada wa Vifaa kwa ajili ya shule ya Walemavu.

Mkurugenzi wa Human Relief Foundation, Sheikh Khalid Butchery  akizungumza alisema Taasisi yake imeguswa na harakati za Tulia katika kuisaidia jamii na imeguswa zaidi na changamoto zinazoikabili shule hiyo na ndiyo maana imeamua kuisaidia.

Alisema Taasisi yake imetoa baiskeli 15 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu, mafuta maalum ya kupaka kwa wanafunzi wenye ulamavu wa Ngozi katoni mbili, kofia 40 kwa ajili ya watoto hao, pia karatasi maalum za kuandikia kwa watoto wenye ulemavu wa macho.

Pia Taasis hiyo imetoa mifuko 250 ya saruji kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya kujisomea hasa kwa kujenga darasa jingine la watoto hao shuleni hapo.