EU yaongeza ushuru kwa bidhaa kutoka Marekani

Jumuiya ya Ulaya EU imeanzisha ongezeko jipya la tozo kwa bidha zinazotoka Marekani kama hatua ya kulipa kisasi dhidi ya sera ya kibiashara ya Rais Trump iliyotangaza ongezeko tozo ya uingizwaji wa bidhaa za chuma na bati nchini humo.

Ongezeko hilo jipya la tozo lililotangazwa na EU linazilenga bidhaa za Marekani kama vile vinywaji vikali,Pikipiki zinzotengenezwa Marekani pamoja na maji ya matunda ya machungwa.

Ongezeko hili la tozo mpya ya EU kama hatua ya kujibu mapigo dhidi ya Marekani dhidi ya Marekani itaziathiri bidha kama tumbaku,piki piki maarufu za Harley Davidson,siagi ya karanga bidhaa ambazo kwa sasa zitakumbana na ongezeko la asilimia 25 sawa na kiasi cha yuro bilion 2.8 ambapo utekelezwaji wake unaanza rasmi leo.

Rais wa jumuiya ya Ulaya Jean-Claude Juncker amesema tozo iliyoanzishwa na Marekani dhidi ya umoja huo inakwenda kinyume na hali halisi na historia ya uhusiano uliokuwepo kibiashara kati ya EU na Marekani.

Mwezi marchi mwaka huu utawala wa Marekani ulianzisha ongezeko la tozo ya asilimia 25 kwa chuma na asilimia 10 kwa kwa bati kwa lengo la kutoa fursa kwa makampuni ya ndani ya Marekani yanayoingiza bidhaa kama hizo.

Hata hivyo utekelezaji wa sera hiyo mpya ya biashara ya Marekani ilianza kutekelezwa june mosi na kuathiri mataifa kama vile Canada,Mexico na washirika wengine wa karibu kibiashara na Marekani.

Rais Jean-Claude Juncker,ambaye awali alikosoa hatua ya Marekani na ongezeko lake hilo jipya la tozo akizungumza hapo jana bungeni mjini Dublin nchini Ireland,amesema watafanya kila linalowezekana kuweka mambo sawa na kuilinda EU.

Hata hivyo hatua hii ya EU huenda ukawa pigo Zaidi kwa Marekani ambayo bidhaa zake kama vile viatu na nguo kwa sasa zitatozwa ongezeko la asilimia 50.

Mapema wiki hii Rais Trump katika hatua nyingine alitishia kuwa na ongezeko la asilimia 10 sawa na dola bilino 200 dhidi ya bidhaa za China na kuongeza kuwa zitaanza kufanya kazi iwapo Chuina itakaa kubadili mfumo wake wa kibisahara dhidi ya Marekani,lakini China nayo ikajibu mapigo kwamba itachukua hatua kali kibiashara zinazo jibu mapigo.

584 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons