Kwa mujibu wa vyanzo vya sky sports ya nchini Uingereza vinaeleza kuwa mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Fred anayechezea klabu ya Shakhtar Donesk ya nchini Ukraine anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya jumatatu hii ili kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Manchester United

Fred aliingia uwanjani dakika 8 kabla ya mpira kumalizika kwenye mechi ya kirafiki kati ya Brazil vs Croatia iliyocheza Jana katika dimba la Anflied na anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Jose Mourinho katika kipindi hiki cha majira ya joto : : :

Fred mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Shakhtar Donesk mwaka 2013 akitokea klabu ya International ya nchini Brazil na tangu ajiunge na miamba hiyo ya Ukraine tayari ameshaichezea timu hiyo zaidi ya michezo 150

1642 Total Views 1 Views Today
||||| 1 I Like It! |||||
Sambaza!