HATUA YA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO “AZAM SPORTS ”KUANZA IJUMAA IJAYO

Hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ‘Azam Sports Federation Cup’ inatarajia kuendelea Ijumaa ya Machi 30 2018 kwa mchezo mmoja kupigwa.

Stand United itakuwa nyumbani kupambana na Njombe Mji katika Uwanja wake wa nyumbani, CCM Kambarage, mchezo utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Baada ya mchezo huo siku ya Ijumaa, michezo hiyo itaendelea tena Jumamosi ya Machi 31 2018 kwa mechi mbili, Tanzania Prisons itacheza na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya majira ya saa 8 mchana.

Na Azam FC itacheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, mchezo utaanza saa 2 kamili usiku.

Hatua hiyo ya robo fainali itakamilika Jumapili, April 1 2018 kwa mchezo mmoja kuchezwa Uwanja wa Namfua kati ya walima alizeti, Singida United watakapowakaribisha Yanga.

 

1122 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!

Comments

comments

Show Buttons
Hide Buttons