Liverpool imeitandika AS Roma kwa Mabao 5-2 na kujiweka sehemu nzuri ya kutinga hatua ya fainali, mabao ya Liverpool yalifungwa na Mshambuliaji Mmisri Mohamed Salah aliyefunga mabao 2 dakika ya 36 na 45 Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Msenegal Sadio Mane dakika ya 56 na Mbrazil, Roberto Firmino (kushoto) mawili pia dakika za 62 na 69 wakati ya Roma yamefungwa na Edin Dzeko dakika ya 81 na Diego Perotti kwa penalti dakika ya 84 kufuatia James Milner kuushika mpira kwenye boksi. Roma itahitaji ushindi wa 3-0 kwenye mchezo wa marudiano Mei 2, Uwanja wa Olimpico ili kusonga mbele

 

https://youtu.be/aB2eyN0TInU

1414 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!