Baada ya siku ya uvumi wa siku nyingi, imethibitishwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China.

Ziara hiyo, ambayo ilithibitishwa na China na Korea Kaskazini, ndiyo ya kwanza inayofahamika ya Bw Kim nje ya taifa lake tangu alipochukua mamlaka mwaka 2011.

Bw Kim alifanya “mazungumzo ya kufana” na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Beijing, shirika la habari la China, Xinhua liliripoti.

China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kiuchumi na baadhi ya wachambuzi wanasema uwezekano wa wawili hao kabla ya mkutano mkuu wa Bw Kim na viongozi wa Korea Kusini na Marekani ulitarajiwa.

Bw Kim amepangiwa kukutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in mwezi Aprili na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei.

#BBC

By Jamhuri