Kashfa mpya Maliasili

Kagasheki

Watakaoomba wataliwa fedha zao
Wafanyabiashara wasio kwenye mtandao kama ule wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii Tanzania (TAHOA), wanakabiliwa na hatari ya kupoteza fedha za maombi ya vitalu. Kwa kawaida fedha zinazolipwa wakati wa maombi hazirejeshwi (non-refundable) kwa waliopata au waliokosa vitalu.

Hadhari hiyo inatokana na ukweli kwamba tayari vitalu vyote vimeshapata wenyewe, na kilichofanywa kupitia matangazo kwenye magazeti ni kukamilisha taratibu tu. Ada ya chini ya kuomba kitalu ni dola 1,000 za Marekani; ilhali ya juu ni dola 5,000.