Aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa (wa pili kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe,  wakimjulia hali  Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.

MWANASIASA mkongwe , Kingunge Ngombale Mwiru, ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili kufuatia kung’atwa na mbwa amemkumbuka na kutaka kujua haliya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye amesafirishwa kutoka hospitalini Nairobi, Kenya,  kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

 

Kigunge ameulizia hali ya Tundu Lissu baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa aliyekuwa amefuatana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,  Edward Lowassa,  walipomtembelea leo Januari 8, 2018 katika hospitali ya Muhimbili.

 

“Vipi hali ya  Tundu Lissu? Nimeona mimi jinsi wanavyonifanyia hapa (madaktari),  nimewauliza mimi tu niliyeng’atwa na mbwa mnanifanyia hivi, je Lissu mmemfanyaje maana majeraha yake yalikuwa makubwa?” amehoji Kingunge

 

Baada ya Mbowe kumueleza mkongwe huyo juu ya hali ya Tundu Lissu kwa sasa, alipata faraja na kusema  ‘Aluta Continua’ ikimaanisha (kwa lugha ya Kireno) ‘Mapambano Yanaendelea’.

By Jamhuri