Mkutano huo unaofanyika katika kijiji cha Panmunjom ambapo mazungumzo yao yanahusu uwezekano wa Korea Kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatakayofanyika Korea Kusini mwezi wa pili.

Waziri wa muungano wa Korea Kusini , Cho Myoung-Gyon amesema mazungumzo hayo yanajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kuimarisha uhusiano.

“Tutahudhuria mkutano huu ili kuzungumzia suala la korea kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatayofanyika korea kusini na kuimarisha uhusiano wan chi hizi mbili.Ninaelewa kuwa matarajio ya wengi juu ya mkutano huu ,kwanza ni kuhusu mawasiliano baina ya nchi hizi mbili ambayo yalisitishwa kwa muda.Tuna lengo la kufanya mashindano haya ya Olimpiki kuwa ya hatua ya kwanza ya kuboresha Amani baina ya nchi hizi mbili hivyo hii ni hatua nzuri na hatuna haraka.”Cho Myoung-Gyon aeleza.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili uliporomoka baada ya Korea Kusini kukatisha mradi wa pamoja wa kiuchumi huko eneo la kiuchumi la Kaesong Korea Kaskazini, na kufuatiwa na majaribio ya nyuklia yaliofanywa na Korea Kaskazini.

By Jamhuri