“Kujitegemea maana yake ni kwamba
hatuna budi kutumia kwa juhudi zetu zote
rasilimali yetu tuliyonayo.”
Nukuu hii imetolewa kwenye kitabu cha
nukuu za Kiswahili za Rais wa Kwanza wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mwalimu Julius Nyerere.

Ubaguzi – Mandela
“Ninapinga ubaguzi wa rangi kwa sababu
ninauchukulia kuwa jambo la kipuuzi, iwe
linatoka kwa mtu mweusi au mweupe.”
Kauli hii ilitolewa na Rais wa Kwanza wa
Afrika Kusini, Nelson Mandela.

Uongo – Papa Yohane Paulo II
“Visingizio ni vibaya zaidi na vinatisha kuliko
uongo, kwani visingizio ni uongo uliopakwa
mafuta.”
Kauli hii ilitolewa na Papa Yohane Paulo wa
II alipokemea tabia ya kutoa visingizio

badala ya kutenda.
Oprah Winfrey na maisha
“Kwa kutazama tu ulichonacho maishani,
kila siku utahisi una zaidi, ila kwa kutazama
unachokosa maishani, kamwe hautakuwa
na zaidi.”
Nukuu hii ilitolewa na Oprah Winfrey,
mwongozaji wa maonyesho ya televisheni
anayemiliki kipindi nchini Marekani.
Mwigizaji huyo wa filamu mwenye umri wa
miaka 63 amewahi kushinda tuzo
mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘The
Oprah Winfrey Show’. Alizaliwa Januari 29,
1954, Mississippi nchini Marekani.

Mwisho

1245 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!