Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem (wa kwanza kulia) akizindua kisima cha maji katika shule Gezaulole. akiwa na mwalimu Mkuu Maryam Shaban (wa tatu kulia), na Sheikh Kaporo ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa kisima wa kwanza kushoto 
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem akihutubia baada ya uzinduzi wa kisima, kulia kwake ni Diwani wa Sumangila Fransis Chichi na kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu Waryam Shabani.
Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi akizungumza jmbo mara baad ya Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem kuzindua kisima 
Wanafunzi wakiwa wamebeba vifaa maalumu vya kuhifadhi maji vilivyotolewa msaada na Ubalozi wa Kuwait Nchini
Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh.Jasem Al-Najem akiwa amekaa na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya Gezaulole ambapo amewaahidi kuwapati mdftari na mikoba
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh.Jasem Al-Najem katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo
Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh.Jasem Al-Najem ajumuika na wanafunzi darasani na kukagua madftri yao
Wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kumkaribisha mgeni rasmi Mh, Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem.

 

Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe, Jasem Al-Najem azindua kisima cha 61 katika shule ya msingi ya Gezaulole, Wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam machi 7, 2018, Ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa ”Kisima cha Maji katika kila Shule”.

Ulio anzishwa na Ubalozi wa Kuwati mwishoni mwa mwaka 2016, Hafla ya uzinduzi wa kisim hicho kilihudhuliw na Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Maziku Luhemeg, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Gezaulole, Masiku Lupa, Mwalimu Mkuu Maryam Shabani pamoja na walimu na wanafunzi wa shule hiyo,kilicho zindiuliwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mh. Jasem Al-Najem.

Ambapo kitanufaisha shule ya Msingi ya Gezaulole iliyoanzishwa mwaka 1962 yenye wanafunzi 868 na madarasa kumi na shule jirani ya Sekondari ya Ibnu Rushyyenye wanafunzi 250 iliyo anzishwa mwaka 2007.

Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh. Jasem Al-Najem katika hotuba yake baada ya uzinduzi huo amesema kuwa Ubalozi wa nchini mwake umeanzisha mradi wa “Kisima cha Maji” ilikuitikia wito na kuunga mkono sera ya Rais wa Tanzania, Mh. Jonh Magufuli ya kutoa Elimu bure .Balozi Mhe, Jasem Al-Najem ameeleza kuwa kuwa atashirikiana na viongozi wa eneo hilo katika kutatua changamoto zitakazo kabiliana na shule hiyo,

Aidha aliahidi kuwapatia wanafunzi wa shule hiyo, madaftari , , mikoba na vifaa vya kuhifadhia maji kwa kila darasa ili wanafunzi wasihangaike kuchukua maji katika kisima mara kwa mara huku akiwataka wanafunzi hao kujihimu katika masomo yao ili wawe mdaktari, wanahabari, walimu.

Diwani Sumangila kwa upande wake Francis Chichi ameishukuru Kuwait kwa kuwachimbia kisima cha maji katika shule hiyo huku akimuomba Balozi, Jasem Al-Najem kusaidia Kata yake gari la kubebea wagonjwa ili kuwaondolea akina mama wajawzito na watu wazima ambao hulazimika kutembea masafa marefu kufika Hospitali na katika vituo vya Afya ambapo baadhi yao wakati mwingine hulazimika kukodi Pikipiki ili kufika huko, jambo ambalo linahatarisha uhai wao.

By Jamhuri