Lwandamina amewataka mashabiki wa timu hiyo mambo ya kombe la Mapinduzi na kuangalia michuano inayowakabili mbele yao

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina, amemtetea mshambuliaji wa timu hiyo Obrey Chirwa, kuwa mkwaju wa penalti aliokosa ilikuwa na bahati mbaya na hakufanya makusudi kama mashabiki wanavyodai.

Lwandamina amesema, vitu kama hivyo hutokea kwa mchezaji mwenye uwezo wa kupiga penati kama Chirwa hivyo haoni sababu ya mashabiki kumlaumu kwasababu hakukusudia.

“Hatupaswi kumpa lawama kwasababu siku nyingine anaweza kukataa kufanya hivyo, na vitu kama hivyo ni kawaida kutokea kwa mchezaji mwenye kiwango kama cha Chirwa, amesema Lwandamina.

Kocha huyo amesema niwakati sasa wa kujipanga na kuangalia michuano inayowakabili mbele yao kuliko kubaki kumtupia lawama mchezaji kwa michuano ya wiki mbili ambayo nikama mazoezi.

1070 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!