Mabomu Mbagala siri zavuja

Uthamini wa pili
Baada ya malalamiko kuwa mengi kupitia vyombo vya habari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, chini ya William Lukuvi, iliamuru uthamini ufanywe upya. Uthamini wa pili ulitumia wiki tatu na ilipofika Juni 30, 2009 ripoti ya pili ilikamilika.

Uthamini huu sasa ulibaini kuwa nyumba 9,467 zilikuwa zimeathirika kwa viwango tofauti na ndipo sarakasi za kupunjana zilipoanza.