Marekani inaitaka Korea Kaskazini kuangamiza silaha ifikapo 2020

Marekani ina matumaini ya kuanza kuona shughuli ya kuangamizwa silaha nchini Korea Kaskazini ifikapo mwaka 2020, mwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Mike Pompeo.

Matamshi yake aliyoyatoa alipofanya ziara nchini Korea Kusini, yanafuataia mkutano kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Walisaini makubaliano ya kufanya kazi katika kuangamiza kabisa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Lakini nakala hiyo imekosolewa kwa kukosa taarifa za kina kuhusu ni lini na ni vipi Korea Kaskazini itaachana na silaha zake.

Bw Pompeo alisafiri kutoka Singapore kwenda Seoul ambapo alikuwa akihifahamisha serikali ya Korea Kusini kuhusu matokeo ya mkutano huo.

Alsema bado kuna kazi nyingi ya kufanywa na Korea Kaskazini, “ya kuangamiza silaha … Tuna matumaini kuwa tutaweza kutimiza hilo ndani ya miaka miwili unusu.”

Alisema ana uhakika kuwa Pyongyag ilikuwa inafahamu kuwa shughuli yoyote ya kuangamiza programu yake za nyuklia itahitaji hakikisho.

Rais Trump mapema alitangaza kuwa Korea Kaskazini sio tena tisho la nyuklia akisisitiza kuwa kila mtu sasa anaweza kuhisi salama.

Viongozi hao walisema watashirikana katika kujenga uhusiano mpya huku Marekani ikiihakikishia usalama Korea Kaskazini.

Pyongyan nayo itajitolea katika kuangamzia silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea.

Kisha kwenye mkutano na waandishi wa habari Trump akasema kuwa ataiondolewa Korea Kaskazini vikwazo wakati suala la silaha za nyuklia litatatuliwa.

Alisema anaamini kuwa Bw Kim atatekeleza yale ambayo ameyasema.

Alitangaza kusitishwa mazoezi ya kijeshi ambayo hufanyika mara kwa mara kati ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini katika rasi wa Korea

Hatua hiyo imekuwa ikiitishwa kwa muda na Pyongyang na ilitangazwa bila matarajio kutoka kwa washirika wa Marekani na iliwapata kwa mshangao.

Makao rasmi ya rais wa Korea Kusini ya Blue House baadaye yalisema yalitaka kufahamu maana kamili ya matamshi ya Trump kuhusu kusitisha mazoezi ya kijeshia ya pamoja.