Marekani Yaionyeshea Ubabe wa Kivita Korea Kaskazini

Jeshi la Marekani limerusha ndege yake aina ya B-1B bomber katika anga ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini.

Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani.

Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu kuonyesha ubabe baada ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini au majaribio ya mabomu ya nyuklia.

Zaidi ya ndege 200 na maelfu ya wanajeshi wanashirikia katika mazoezi hayo ya kijeshi ambayo yatakamilika siku ya Ijumaa.

Pyongynag ambayo mara nyini hukashifu mazoezi ya pamoja ya Marekania na Korea Kusini, imeyataja mazoezi ya sasa kuwa uchokozi wa vita vya nyuklia.

Misukosuko imekuwa ikiongezeka tangu lifanyike jaribio la kombora mwezi uliopita lililosababisha lawama za kimataifa na onyo kutoka Marekani kuwa Korea Kaskazini itaharibiwa aabisa ikiwa vita vitatokea.