Matokeo ya Uchaguzi Siha Kutoka Vituo Mbalimbali

MATOKEO ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Siha  yameanza kubandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yakionyesha mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel akiongoza kwa mbali katika baadhi ya vituo.

 

Katika matokeo hayo, Dk Mollel  anafuatiwa kwa mbali  na mgombea wa Chadema, Alvis Mossi huku wa CUF,  Tumsifuel Mwanri  akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.

 

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo.

Kituo cha Kirua–Kawate  Kata ya Siha

Wilaya ya Siha mgombea wa CCM  kura  208

Alvis wa Chadema akipata kura 42

Mwanri  wa CUF kura  10.

Katika kituo cha  Lawate namba 2 Kata ya Siha

CCM kura 300

Chadema 21

CUF 0.

Kituo cha Lomakaa, 

CCM ilipata kura 190,

Chadema 10 na CUF haikupata chochote.

Pia kituo cha Ofisi ya Kijiji Sanya Juu,

CCM ilipata kura 284,

Chadema 54 na CUF 1.

Kwa upande wa kituo cha Sanya Juu

CCM ilipata kura 93,

Chadema 50,

CUF 0,

Huku kituo cha Kaboko Kusini 2

CCM 403

Chadema 68

CUF na Sau zikiwa hazijapata kitu.

Pia Kituo kingine cha Kaboko B;

CCM 106

CUF 76,

Sau 0 na kituo cha Ofisi ya VEO Merali Juu1;

Chadema 33,

CCM 64

CUF na Sau vikiwa havijapata kitu.

Ofisi ya VEO Merali Juu2:

Chadema 22

CCM 87.

Endelea kufuatilia matokeo zaidi hapa.