Jibu la swali la pili linapatikana kwa mujibu wa maoni yaliyotolewa na mahakama ya kimataifa Mei 28, Mwaka 1948 kwa maombi ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Swali lililoulizwa na Balaza Kuu la Umoja wa Mataifa mbele ya mahakama lilikuwa na lengo la kupima uzito na endapo mwanachama wa UN anapoomba uananchama chini ya kifungu cha 4 cha katiba anakuwa na uwezo wa kupitishwa kama ilivyoaivishwa.

Majaji walio wengi katika Mahakama ile walibainisha kuwa wanachama walikuwa wakifurahia uhuru wa maamuzi ndani ya chombo kile.

Juu ya madhara ya kisheria ya maazimio yanayofanywa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tofauti lazima iainishwe kati ya uwezo wa Balaza Kuu la Umoja wa Mataifa na yale ambayo ya konje ya chombo hicho.

Goodrich na Hambro wanaeleza kama ifuatavyo;-

“Japo kuwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linaweza kutoa mapendekezo kwa wanachama wa Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Usalama ni muhimu kuzingatia kuwa mapendekezo yale hayana ulazima kama ambavyo imejidhihirisha katika suala la Palestina. Japokuwa yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa wa kisiasa wanachama wa Umoja wa Mataifa wako huru kisheria kukubalia na hayo au kuyakataa.”

 

Misingi ya ubatili wa Azimio la Umoja wa Mataifa.

Si Wapalestina wala mataifa ya Kiarabu walikubaliana na azimio juu ya kugawanywa kwa Palestina wanalichukulia kuwa ni batili na lisilo na tija mtazamo wao umejikita katika misingi ya kisiasa. Historia ya Muundo wa kisheria mjadala huu hata hivyo utatuama katika hoja za misingi kisheria ambazo zina batilisha azimio lenyewe. Misingi hii ni kama yafuatayo;-

 

1.      Udhaifu wa Umoja wa Mataifa

Msingi wa kwanza juu ya ubatili wa azimio lenyewe unajikita katika udhaifu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kushauri juu ya kugawanywa kwa Palestina au kuundwa kwa dola ya Kiyahudi ndani ya nchi.

Msimamo wa kisheria uko dhahiri katika jambo hili. Umoja wa Mataifa ni chombo ambacho kiliundwa kwa ajili ya malengo kadhaa yaliyoainishwa. Wakati wote chombo hiki kilihodhi nguvu ya Wapalestina, wala haki yoyote kwa nchi husika. Kimsingi Umoja wa Mataifa haukuwa na Mamlaka yoyote juu ya uamuzi wa kugawanywa kwa Palestina au (kuchukua) eneo lolote la Kijiografia kwa kikundi kidogo cha ki-dini cha wahamiaji wa kigeni kwa lengo la kulifanya liwe dola yao. Umoja wa Mataifa usingeweza kamwe kutoa kitu ambacho haukimiliki. Katika hali yoyote wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hawakuwa na uwezo wa kupunguza wala kuingilia uhuru wa kujiamulia mambo ya watu wa Palestina na pia wala kuvunjwa ahadi ya kimipaka ya watu husika.

Si kwamba tu Umoja wa Mataifa haukuwa na uwezo wa kuhodhi uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe hali pia haikuwa na mamlaka ya kuiongoza nchi. Muungano wa Mataifa kablah aujavunjika ulitumia mamlaka yaliyotokana na kifungu cha 22 juu ya makubaliano katika suala zima lakini punde muungano huu ulipovunjwa mamlaka haya yaki-usimamizi yalitoka na matokeo haya yaliyotambuliwa rasmi katika kikao maalumu mnao 18 April, 1946.

 

Azimio hili lilisema hivi;-

“Pia yakiwa ni matokeo ya usitishwaji wa uwepo wa muungano wa mataifa, majukumu yake pia yanakoma na mamlaka ya mipaka yaki-jiografia pia nayo yanakoma.”

Kwa upande mwingine Umoja wa Mataifa haukuwa na haki yoyote ya kusimamia mamlaka zilizokuwepo kupitia mfumo wa udhamini (trusteeship system) unaorejewa na kifungu cha 77 cha Katiba ya Umoja wa Mataifa isipokuwa kwa yale yaliyochukuliwa chini ya makubaliano ya ki-udhamini.

Duncan Hall anaweka msimamo wake kwa ufupi kama ifuatavyo;-

“Katika suala linalohusu mamlaka, Muungano wa Mataifa ulikufa bila kauli… hapakuwa na kuhamasishwa kwa haki ya kujiamulia mambo kwenda Umoja wa Mataifa…”

 

Mwandishi wa makala hii 

anapatikana kwa:-

(+255) 784 – 142 137 au

 (+255) 713 – 333 141

Barua pepe: ngayasteve@gmail.com / brilliantconsult2000@gmail.com

1397 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!