Jeneza lenye mwili wa marehemu likifikishwa makaburini.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, mapema leo ameungana na baadhi ya wapenzi na wanachama  wa Klabu ya Yanga kuuzika mwili wa aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Athumani Chama kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu.

Mbali na Kikwete maziko hayo pia yamehudhuriwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao Clement Sanga na viongozi wa Serikali ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba alihudhuria.

Mwanachama maarufu wa Simba, Mzee Dalali akiweka mchanga kwenye kaburi.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akiweka mchanga.

Viongozi hao wakiomba dua wakati wa shughuli ya mazishi.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mkwasa.
1493 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!