NAIBU WAZIRI WA MADINI BITEKO ,AMEWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUZINGATIA SHERIA YA USALAMA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI

Naibu waziri wa madini Doto Biteko,Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Buntumbili Wilayani Bukombe ambapo kulitokea tukio la mchimbaji kufukiwa na kifusi wakati alipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji. 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko,akisaini kwenye kitabu cha wageni wakati alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita. 
Afisa madini wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Ally Maganga akitoa taarifa ya shughuli za madini mbele ya Naibu waziri wa madini Doto Biteko . 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko Akizungumza na Viongozi na Watendaji mbalimbali ngazi ya Mkoa wakati wa ziara yake ya kikazi. 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko pamoja na viongozi wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye eneo ambalo ajali ya mchimbaji kufukiwa na kifusi ilitokea 
Baadhi ya viongozi na Naibu waziri wa madini Doto Biteko wakiwa kwenye shimo ambalo ndipo mchimbaji mdogo ambaye alipoteza uhai wakati akiwa kwenye shughuli za uchimbaji.
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akipatiwa maelezo ya namna ajali hiyo ilivyotokea mgodini hapo.
Mmiliki wa mgodi huo,akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa madini namna ambavyo wachimbaji hao walivyovyamia eneo hilo na kuanza shughuli za uchimbaji hali ambayo imesababisha mmoja wao kufukiwa na kifusi. 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko akitoa mkono wa pole kwa familia ambayo imekumbwa na msiba wa kuondokewa na kijana wao ambaye alifukiwa na kifusi wakati akiwa kwenye kazi ya uchimbaji. 
Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akisalimiana na kutoa pole kwa kaka yake na marehemu wakati alipofika nyumbani kwao na marehemu.(PICHA NA JOEL MADUKA)
Naibu waziri wa madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Biteko akifurahia na wananchi wa kijiji cha Ikalanga wakati alipokwenda kuzungumza nao juu ya mikakati ya maendeleo. 
 
 
Naibu waziri wa madini Doto Biteko amewataka wachimbaji ambao wanamiliki leseni kuhakikisha wanazingatia sheria ambazo wamepewa likiwemo suala la kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwenye maeneo yao ya mgodi ili kuepukana na majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye shughuli za uchimbaji.
Akizungumza wakati alipotembelea na kutoa pole kwenye mgodi mdogokijiji cha Buntubili eneo ambalo hivi karibuni mchimbaji mmoja aliangukiwa na kifusi na kufariki.Naibu waziri Doto alisema ni vyema kwa kila mwenye leseni kuhakikisha usalama unakuwa ni jambo la kwanza huku akimwagiza afisa madini kufuatilia migodi yote kama imewekwa mabango ambayo yanaelekezea suala la usalama kwenye mazingira hayo.
“Hatutaki kuona hata mtanzania mmoja anakufa katika mazingira ya uzembe tunatamani tuone watanzania wote wanachimba wanaendeleza mali na wanabaki kuwa salama kwaajili ya kulihudumia Taifa hili ,Taifa hili linawaitaji watu wote kwa hiyo nitoe wito kila mwenye leseni maali popote alipo ahakikisha kwamba mazingira yake ya kazi usalama kiwe kipaumbele na sasa kuanzia leo afisa madini ninakuagiza wote wenye leseni ambao wanaendeleza migodi waweke mabango yanayoeleza umuhimu wa usalama kila kwenye mgodi unaofanya kazi”Alisisitiza Mh,Doto.
Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Madini amewataka wananchi kutokuingia kwenye maeneo ambayo yamesimamishwa na ambayo ni hatarishi kwani kufanya hivyo wanaweza kujisabasha hatari ya kupoteza maisha kutokana na maeneo hayo kutokuwa kwenye hali nzuri ya uchimbaji.
Akisoma taarifa kwa Naibu waziri wa madini,mlinzi wa eneo hilo la mgodi ,Bw Christopha Mazige .amesema kuwa ajali hiyo ilitokana na ubishi wa vijana watatu ambao walivamia mgodini hapo kwa lengo la kutafuta mali lakini ghafla wakiwa kwenye mabishano sehemu moja ya ardhi alipokuwa amesimama kijana ambaye alifukiwa na kifusi ilikatika na kushuka naye kwenye shimo kutokana na hali hiyo wenzake walikimbia.
Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi Mhandisi Ally Maganga amesema bado kuna changamoto zinazoikabili Sekta ya madini kama baadhi ya Wachimbaji wadogo kushindwa kulipa kwa wakati tozo stahiki za madini kama vile ada za mwaka za leseni na Mrabaha wa madini.