Nyerere: Tushirikishe watu katika maendeleo

“Kama maendeleo ya kweli ni kuchukua mahali, watu wanapaswa kushirikishwa.”

Hii ni sehemu ya maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo, 1973.

Wangari: Waafrika tujikubali jinsi tulivyo

“Itakuwa vizuri kwetu sisi Waafrica kujikubali jinsi tulivyo na kurudia baadhi ya vipengele chanya vya utamaduni wetu.”

Haya ni maneno ya mwanaharakati maarufu wa mazingira wa Kenya, Maathai Wangari.

 

Reagan: Tupime mafanikio ya uastawi

“Lazima tupime mafanikio ya ustawi kwa jinsi watu wengi wanavyoishi kwa ustawi, siyo kwa jinsi wanavyoongezeka.”

Maneno haya ni ya Rais wa 40 wa Marekani, Ronald Reagan, wakati akihimiza ustawi wa jamii.

 

Kibaki: Wakenya tuoneshe tumekuwa kidemokrasia

“Hebu tutume ujumbe mzuri duniani kwamba demokrasia yetu imekuwa. Kura ya amani ni kura ya usalama, mafanikio na Kenya imara.”

Hii ni kauli ya Rais Mwai Kibaki wa Kenya anayemaliza muda wake, wakati akiwaasa Wakenya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu, Machi 4, 2013 kwa amani na kukubali matokeo yake.

1552 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!