LISOME GAZETI LETU LA JAMHURI LA KILA WIKI HAPA

Habari Mpya

MISITU & MAZINGIRA

Misitu inavyokinufaisha Kijiji cha Nanjilinji 'A' (2)

Sehemu ya kwanza, Dk. Felician Kilahama, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya MCDI, anaeleza ziara yake katika Kijiji cha Nanjilinji ‘A’, akiwa na wajumbe wa Bodi. Pia anaeleza kuwa wafadhili kutoka Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Viumbehai na Mimea Ofisi za Denmark na Tanzania, walikuwapo.

Read More »

JAMHURI YA WAUNGWANA

Wakati mwingine Wakristo
wanaanzisha chokochoko

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imewasilisha mapendekezo, ikitaka kubadilishwa kwa siku ya kupiga kura ya maoni kutoka siku ya ibada - Jumapili. Mapendekezo ya CCT yamewasilishwa kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala. Mwakilishi wa CCT, Mchungaji Lazaro Rohho, anasema mabadiliko hayo yanatakiwa kuwekwa kwenye muswada wa kura ya maoni unaotarajiwa kuwasilishwa katika kikao kijacho cha Bunge.

Read More »

Mfanyabiashara afanya unyama Geita

* Akodi vijana, wavunja nyumba, watembeza mkong'oto

* Baba mwenye nyumba atekwa, atelekezwa porini

* Watu 17 wakosa makazi

Vilio, simanzi na huzuni vimetawala katika Kitongoji cha Shinde, Kijiji cha Buhalahala, Kata ya Kalangalala wilayani Geita, kufuatia familia moja katika eneo hilo yenye watu 17 wakiwamo watoto wachanga, kukosa makazi baada ya makazi yao kubomolewa.

Read More »

FIKRA YA HEKIMA

Tindikali imetuchafua,  kauli za polisi ni zilezile

Wiki iliyopita, nchi yetu ilipata doa lenye taswira ya kuichafua mbele ya uso wa Dunia. Raia wawili wa Uingereza, Kate Gee (18) na Kirstie Trup (18) walikumbwa na mkasa wa kumwagiwa tindikali huko Mji Mkongwe, Zanzibar.

Read More »

KONA YA AFYA

Vidonda vya tumbo na hatari zake (8)

Wiki iliyopita, tuliona Dk. Khamis Zephania pamoja na mambo mengine, akizungumzia milo mbalimbali ya watu na urithi wa vidonda vya tumbo. Sasa endelea kumfuatilia katika sehemu hii ya nane…

Read More »

KAULI ZA WASOMAJI

CCM Rukwa tunataka serikali tatu

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa wamekwenda kinyume na msimamo wa chama chao na kutaka uwepo wa serikali tatu maana katiba ni kwa maslahi ya Taifa na sio wana CCM.

Read More »

Ndugu wa Barlow wataka IGP Mwema awajibu

Ndugu wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow aliyeuawa kwa kupigwa risasi, wamesema wanataka majibu ya kina kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema.

Read More »

MPOROGOMYI:

Waziri mstaafu aliyeanzisha kanisa

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Dk. Kilontsi Mporogomyi, ameanzisha kanisa. Kanisa hilo lenye Makao Makuu Makongo, linatambulika kwa Jina la Kanisa la Miujiza, Uponyaji, Kufunguliwa na Mafanikio.

Read More »

Habari za Kitaifa

Maoni ya Mhariri

Nyundo ya Wiki